Senegal vs EgyptSenegal vs Egypt
  • Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika AFCON 2025 yanazidi kushika kasi.
  • Mashindano hayo sasa yameingia katika hatua ya Nusu Fainali ambapo timu nne bora zitatoana jasho.
  • Nusu Fainali ya kwanza na ya mapema zaidi itawakutanisha Senegal vs Egypt.
  • Mechi hii itapigwa dimba la Grand Stade de Tanger na makala hii inakuletea taarifa muhimu kuhusu mchezo huu.

Hatimaye mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2025), yameingia hatua ya Nusu Fainali. Mechi mbili za uzito mkubwa wa hadhi ya Nusu Fainali zitapigwa leo Jumatano, katika harakati za kuisaka Fainali. Segegal vs Egypt ndio mchezo wa mapema zaidi kabla ya Nusu Fainali ya pili.

SOMA HII PIA: AFCON 2025 Algeria vs Nigeria: Ratiba Robo Fainali Live score, lineups, h2h, prediction, Habari za timu

Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

H2H, Senegal vs Egypt

Senegal vs Misri
Senegal vs Egypt

Historia ya soka la ushindani kati ya Senegal na Egypt inaonyesha timu hizi zimekutana mara 15. Senegal imeshinda mechi 6 tu, huku Egypt ikiongoza kwa kushinda mechi 7. Mechi 2 zilizosalia zilimalizika kwa matokeo ya sare.

Fomu ya Senegal kwenye mechi 5 zilizopita

WDWWW

Fomu ya Egypt katika mechi 5 zilizopita:

WWDWW

Vikosi tarajiwa Senegal vs Egypt

Senegal

Senegal vs Egypt
Mane

Kipa: Edouard Mendy

Walinzi: Krepin Diatta, Kalidou Koulibaly, Moussa Niakhate, El Hadji Malick Diouf

Viungo: Pape Gueye, Idrissa Gueye, Habib Diarra

Washambuliaji: Sadio Mane, Iliman Ndiaye, Nicolas Jackson.

Egypt

Kipa: Mohamed El Shenawy

Walinzi: Rami Rabia, Yasser Ibrahim, Hossam Abdelmaguid, Mohamed Hany

Viungo: Marwan Attia, Hamdy Fathy, Ahmed Abou El Fotouh

Washambuliaji: Emam Ashour, Omar Marmoush, Mohamed Salah.

SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 matokeo na ratiba hii hapa/ Msimamo, live scores

Habari za timu

Egypt
Egypt

Hii ni mara ya kwanza kwa Senegal na Egypt kukutana, katika mashindano ya AFCON tangu fainali ya mwaka 2021. Kumbkumbu za fainali hiyo ni Senegal kuibuka washindi kwa mikwaju ya penalti.

Senegal waliiondosha Mali katika robo fainali, huku bao pekee la Iliman Ndiaye dakika ya 27 likiwapa ushindi. Egypt wao walivuka baada ya kuwavua ubingwa waliokuwa mabingwa watetezi Ivory Coast kwa ushindi wa mabao 3-2. Katika mchezo huo uliopigwa dimba la Stade Adrar mabao kutoka kwa, Omar Marmoush na Ramy Rabia yaliitanguliza Egypt kabla ya Mohamed Salah kuifungia bao la ushindi.

Kukutana tena kwa Salah na mchezaji mwenzake wa zamani wa Liverpool Sadio Mane kumeendelea kushika vichwa vya Habari. Hii ni kutokana na historia ya wawili hao ambao waliunda safu kali ya ushambuliaji, wakiwa kwa majogoo wa jiji.

Kila mmoja ameisaidia timu yake kufika hatua waliyopo, huku Salah akihusika kwenye mabao matano, moja zaidi ya Mane. Ubora wa kila mmoja wao unatajwa huenda ukaamua pambano hili. Je nani kuuwasha moto? Dakika 90 zitatoa majibu.

Taarifa ya majeruhi

Senegal inaingia kwenye mchezo hii ikiwa haijaandikisha majeruhi yoyote, hivyo wako tayari kwa mchezo. Egypt wao wametangaza majeruhi mmoja ambaye ni Mohamed Hamdi. Nyota hiyu alipata jeraha la goti katika mchezo wao dhidi ya Benin.

SOMA HII PIA: AFCON 2025: Matokeo na Ratiba ya Robo Fainali, hizi hapa timu zilizofuzu

Hitimisho

afcon ---- Nigeria vs Morocco
afcon 2025 Robo Fainali

Senegal vs Egypt kwa kuzingatia ubora wa vikosi na historia ya vikosi vya timu hizi, mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu sana. Lakini ni wazi kila timu inaitaka Fainali, Egypt wanapewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda mchezo huu. dakika 90 zitaamua nani anatangulia Fainali kusubiri mshindi wa Nusu Fainali ya pili.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.