- Africa Cup of Nations Januari 14 2026 nusu fainali Mo Salah aambulia patupu
- Senegal 1-0 Misri Sadio Mane shujaa abeba tuzo ya Man of The Match
- Morocco vs Nigeria kutoa mshindi atakayecheza fainali ya AFCON 2025 vs Senegal
Senegal 1-0 Misri ni matokeo ya nusu fainali AFCON 2025. Sadio Mane ni mfungaji pekee wa goli la ushindi kwenye mchezo dakika ya 78. Mane amemfungashia virago Mo Salah wa Misri baada ya dakika 90 kwenye mchezo uliochezwa Grand Stade de Tanger.
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Senegal 1-0 Misri nusu fainali AFCON 2025

Senegal 1-0 Misri ni rekodi inayoandikwa hatua ya nusu fainali AFCON 2025 nchini Morocco. Ushindi huo unaipa tiketi timu ya taifa ya Senegal kutinga hatua ya fainali mbele ya Mo Salah ambaye amekwama kuibeba Misri. Vijana wa Senegal walionyesha morali tangu mwanzo wa mchezo kutokana na kushambulia lango la Misri kama nyuki.
Mane mchezaji bora wa mchezo

Mfungaji pekee wa goli la ushindi Sadio Mane dakika ya 78 amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo. Mane alikuwa kwenye siku nzuri kazini mbele ya Mo Salah. Anatarijiwa kukiongoza kikosi hicho kwenye hatua ya fainali.
SOMA HII: AFCON 2025: Matokeo, hawa hapa wafungaji bora kabla ya Ratiba ya 16 bora, Feisal na Msuva wamo?

Takwimu za mchezo
| Senegal | Misri | |
| 11 | Mashuti | 4 |
| 4 | Lenga lango | 1 |
| 65% | Umiliki | 35% |
| 10 | Faulo | 11 |
| 0 | Kadi nyekundu | 0 |
| 2 | Kadi za njano | 1 |
| 6 | Kona | 1 |
| 1 | Otea | 1 |
Sadio Mane rekodi
Sadio Mane amekuwa shujaa kwa kufunga bao la ushindi mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Misri. Senegal inakuwa ni mara ya nne kutinga hatua ya fainali. Inasaka taji la pili ilitwaa 2021 kwa kuifunga Misri katika changamoto za penalti. Ilipoteza mbeme ya Cameroon na Algeria 2002 na 2019.
Goli alilofunga leo AFCON 2025 Mane linamfanya awe amehusika katika mabao mengi zaidi tangu 2010. Anafikia rekodi yakuhusika katika magoli 20, akifunga 11 na pasi 9 za magoli.
Mohamed Salah wa Misri amekwama kufika hatua ya fainali. Yeye na wachezaji wenzake watajilaumu katika mchezo kwa kushindwa kutengeneza nafasi nyingi na kuzitumia. Shuti la dakika 82 lilikuwa la kwanza kwa Misri kulenga lango.
Katika dakika 45 za mwanzo Misri hawakupiga shuti hata moja ambalo lililenga lango huku Senegal wakipiga mashuti 6.
| Senagel | 1 | 0 | Misri |
Senegal anasubiri mshindi wa mchezo kati ya Morocco vs Nigeria watakutana fainali. Timu zote ambazo zimetinga hatua ya nusu fainali zimewahi kutwaa taji la AFCON. Senegal imetwaa taji hilo mara moja hivyo inapambana kulitwaa mara ya pili.
Hitimisho
Senegal 1-0 Misri ni mchezo uliokuwa na mvuto mkubwa. Mo Salah na Sadio Mane ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakivuta hisia za wengi. Fainali inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuwa bora hatua ya nusu fainali.

