Yanga SC bingwa NMB Mapinduzi Cup 2026Yanga SC bingwa
  • Yanga SC yapata milioni 150 kutoka kwa wadhamini NMB huku Azam FC ikipata zawadi ya milioni 100.
  • Yanga SC bingwa NMB Mapinduzi Cup 2026 kwa penati 5-4 Azam FC.
  • Taji la tatu kwa Yanga SC ilitwaa 2010, 2020 na 2026

Yanga SC bingwa NMB Mapinduzi Cup 2026 kwa penati 5-4 Azam FC baada ya dakika 120 kutoshana nguvu Uwanja wa Gombani. Kwenye fainali ya leo dakika 90 za mwanzo zilikamilika ubao ukisoma Azam FC 0-0 Yanga SC. Ziliongezwa dakika 30 bado matokeo yalikuwa 0-0 hivyo mshindi alipatikana kwa mikwaju ya penati.

SOMA HII: Azam FC yaivuruga Simba SC yaifunga mara mbili mfululizo/ Kariakoo Dabi hakuna tena

Vuna mamilioni sasa hivi

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri

image

Yanga SC bingwa NMB Mapinduzi Cup 2026

Yanga SC bingwa NMB Mapinduzi Cup 2026
Yanga SC bingwa NMB Mapinduzi Cup 2026. Source: Yanga SC.

Yanga SC bingwa NMB Mapinduzi Cup 2026 ikishinda mbele ya matajiri wa Dar. Mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa ulitamatisha dakika 120. Katika kipindi cha kwanza timu zote mbili zilikuwa zinashambuliana kwa kushtukiza. Dakika zote 120 hakuna timu iliyopata goli.

Mlinda mlango wa Azam FC, Aishi Manula alikuwa imara kutimiza majukumu yake. Pigo la penati ya Pacome aliokoa na kulifanya lango kuwa salama. Hiyo ilikuwa dakika ya 115. Yanga SC walipata penati hiyo baada ya mwamuzi kutafsiri kuwa mchezaji wa Azam FC ameushika mpira ndani ya 18.

Hii inakuwa penati ya kwanza Pacome kuikosa ndani ya 2026 kwenye NMB Mapinduzi Cup. Licha ya kukosa penati hiyo bado wachezaji waliendelea kupambana bila kuchoka. Mpaka dakika 120 zinakamilika hakuna goli.

SOMA HII: Azam FC vs Yanga SC fainali NMB Mapinduzi Cup Januari 13,2026/ Live Score, lineups

image

Kadi nyekundu

Azam FC walikamilisha dakika 120 wakiwa 10 uwanjani. Hiyo ilitokana na nyota wao Cheickna Diakite akionyeshwa kadi nyekundu. Ni kadi mbili za njano alionyeshwa dakika ya 55 kwa kumchezea faulo Dickson Job na dakika ya 72 kwa kumchezea faulo Kibwana Shomari.

Aboutwalib Mshery amjibu Manula

Aboutwalib
Aboutwalib mlinda mlango wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Baada ya Manula kuokoa penati dakika ya 115, kipa wa Yanga SC alimjibu Manula kwa kuokoa penati moja. Wakati wa mapigo ya penati za kusaka mshindi nyota Zouzou alikosa. Ni Mshery alitimiza majukumu yake kwa kuokoa penati hiyo.

Kipa Mshery alianza kikosi cha kwanza katika fainali. Hiyo ilitokana na kipa namba moja wa Yanga SC Djigui Diarra kuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Mali. Licha ya Diarra kutukuwepo bado kazi ilifanyika.

Mwemnyeto apiga penati ya ushindi

Nahodha wa Yanga SC, Bakari Mwamnyeto alipewa jukumu la kupiga penati ya ushindi. Kama beki huyo angekosa penati hiyo kazi ya kuhesabu penati moja moja kwa wachezaji ingeanza. Kufunga kwake mbele ya Manula ikawa mwisho wa hesabu NMB Mapinduzi Cup 2026.

Wachezaji waliokuwa timu ya taifa kazini

Prince D
Prince Dube mshambuliaji wa Yanga SC vs Azam FC. Source: Yanga SC.

Yanga SC iliwajumuisha wachezaji wake waliokuwa kwenye majukumu ya taifa. Mshambuliaji Prince Dube raia wa Zimbabwe alianza kikosi cha kwanza. Mbali na Dube Mohamed Hussen Zimbwe Jr, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca hawa walikuwa katika kikosi cha Yanga SC.

SOMA HII: Yanga SC haijapoteza mechi 2025/26 NBC Premier League / Kariakoo Dabi inanukia, matokeo, rekodi

image

Hitimisho

Yanga SC bingwa NMB Mapinduzi Cup 2026 likiwa ni taji la kwanza ndani ya mwaka mpya. Benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalves wameanza kwa ushindi. Azam FC wanakuwa washindi wa pili wakitoka kundi A lililokuwa na bingwa mtetezi Mlandege FC.

Share this: