Clatous Chama kumalizana na Simba SCChama---
  • Mwamba wa Lusaka raia wa Zambia kiungo mshambuliaji aliyecheza Yanga SC anatajwa kurejea unyamani.
  • Clatous Chama kumalizana na Simba SC sababu zatajwa, viongozi wanaomkubali wapo.
  • Singida Black Stars wagusia simu kuita kuulizia saini ya nyota huyo mwenye miaka 34.

Clatous Chama kumalizana na Simba SC dirisha dogo la usajili. Kiungo huyo kwa sasa yupo Singida Black Stars. Alijiunga hapo mara baada ya mkataba wake na Yanga SC kuisha. Tetesi zinaeleza mnyama anahitaji huduma ya kiungo huyo kwa mara nyingine tena.

SOMA HII: Tuzo ya ufungaji bora vita yake inazidi kuchangamka/ Kariakoo Dabi kumaliza utata Juni 25 2025

Shinda mamilioni sasa hivi na aviator kwa kupaisha kindege cha SportPesa

Wakati ukihabarika na makala hii, kumbuka unayo nafasi ya kushinda mamilioni kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.

image

Kwa nini Clatous Chama anatajwa kumalizana na Simba SC?

Clatous Chama kumalizana na Simba SC
Chama Clatous ndani ya Singida Black Stars. Source: Singida Black Stars.

Sababu kubwa zinazofanya Clatous Chama kumalizana na Simba SC ni uwezo wake kuendelea kuwa bora. Kutokana na kupata nafasi ndani ya Singida Black Stars amezidi kuwa imara. Tofauti na alipokuwa Jangwani hakuwa na uhakika wa namba kikosi cha kwanza.

Akiwa na Singida Black Stars alitwaa taji la Kagame Cup. Kushindwa kuwa kwenye mwendelezo bora viungo waliopo unyamani ni sababu nyingine. Jean Ahoua ambaye ni tegemeo eneo la ushambuliaji msimu wa 2025/26 hajarejea katika ubora wake.

Kuondoka kwa Awesu Awesu

Awesu Awesu
Awesu Awesu kiungo mshambuliaji wa Simba SC. Source: Simba SC.

Kwenye eneo la kiungo mshambuliaji Awesu Awesu alikuwa anapewa nafasi kufanya vizuri. Kwa sasa kiungo huyo hayupo. Ametambulishwa Police FC ya Kenya kwa mkopo wa miezi 6 hivyo kuna uhitaji mkubwa eneo la kiungo. Jina ambalo linatajwa ni Chama.

Licha ya kwamba Awesu hakuwa chaguo la kwanza Msimbazi bado kuna kazi alikuwa anafanya. Katika NMB Mapinduzi Cup 2026 alikuwa anaaminiwa na kocha mpya. Kuondoka kwake kunawafanya mabosi wat imu hiyo kufikiria mbadala wake.

Uzoefu wa ligi ya ndani

Clatous C
Clatous Chama Mwamba wa Lusaka. Source: Singida Black Stars.

Clatous sio mgeni na ligi ya ndani kutokana na kucheza kwa muda mrefu. Timu ya kwanza kumtambulisha Bongo ilikuwa ni Simba SC. Hivyo inatajwa kwamba uelewa wake wa ligi utampa nafasi kikosi cha kwanza.

Benchi la Simba SC kumfundisha

Kufundishwa na benchi la ufundi la Msimbazi kunampa nafasi kurejea kwa mara nyingine. Ikumbukwe kwamba Chama aliwahi kuondoka Simba SC kuelekea RS Berkane. Huko alicheza msimu mmoja akarejea unyamani. Kwa sasa yupo Selemen Matola ambaye ni kocha msaidizi anatambua uwezo wa Chama.

SOMA HII: Clatous Chama kiungo wa Yanga SC kuongezewa mkataba, Fei Toto, Ahoua, Job

image

Uwezo wakufunga kitaifa na kimataifa mabao muhimu

Chama anakumbukwa kwa magoli yake ya jioni katika anga la kimataifa ikiwemo dhidi ya AS Vita. Pasi zake na utulivu vinatajwa kujadiliwa. Ikumbukwe kwamba ni mkali wa mapigo huru aliwahi kuwafunga Azam FC dakika za lala salama mchezo wa ligi wakigawana pointi mojamoja.

Licha ya kucheza Yanga SC msimu mmoja bado anatajwa kuwa na mawasiliano mazuri na baadhi ya viongozi wa Simba SC. Taarifa zinaeleza kuna mgawanyiko wa pande mbili. Wapo viongozi wanaohitaji Chama arejee wengine wanaona asirudi kwa sasa.

Msikie Hussen Masanza wa Singida Black Stars

Hussen Masanza, Ofisa Habari wa Singida Black Stars hivi karibuni wakati timu hiyo ikitokea nje ya Tanzania katika mchezo wa kimataifa alibainisha kuna timu nyingi zinahitaji saini ya Chama. Masanza aliongeza kuwa Chama ni kiungo bora kutokana na kazi ambayo anaifanya.

“Kuna timu nyingi zinahitaji saini ya Chama hilo lipo wazi. Zipo za ndani na nyingine kutoka nje ya nchi. Ukweli ni kwamba Clatous Chama ni kiungo mwenye uwezo mkubwa.

“Chama amefunga magoli mengi kwenye anga la kimataifa. Uzoefu wake ni hazina ndani ya Singida Black Stars. Kwa sasa bado yupo na ataendelea kuwapa burudani wana Singida Black Stars,”.

SOMA HII: Clatous Chama kiungo wa Yanga SC kusaini Zesco United | Mkataba umeisha | Simba SC yatajwa

image

Hitimisho

Clatous Chama kumalizana na Simba SC itafahamika kwani bado usajili unaendelea. Chini ya Steve Barker timu hiyo haijatambulisha mchezaji mpya. Ni suala la kusubiri nani atakuwa ingizo jipya unyamani.

Share this: