Allan Okello mambo fresh Yanga SCOkello
  • Mohamed Damaro ameshaanza kazi Yanga SC ikiwa ni ingizo jipya kwenye timu hiyo.
  • Allan Okello mambo fresh Yanga SC, suala la muda kutambulishwa Jangwani.
  • Marouf Tchakei kuna jambo halijakaa sawa huko licha ya utambulisho wake.

Allan Okello mambo fresh Yanga SC tetesi zinaeleza hivyo baada ya kufikia makubaliano pande zote mbili. Yanga SC tayari wametambulisha wachezaji wapya watatu hivyo kuna wengine wanafuata. Taarifa zinaeleza kwamba kuna asilimia kubwa winga huyo kutoka Vipers akatambulishwa muda wowote.

SOMA HII: Usajili Yanga SC umeanza Emmanuel Samuel asaini miwili/ Okello mkataba mpya

Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Allan Okello mambo fresh Yanga SC, watatu watambulishwa

Allan Okello mambo fresh Yanga SC
Allan Okello

Ni Allan Okello mambo fresh Yanga SC baada ya mazungumzo kuelezwa kuwa yamefikia sehemu nzuri. Raia huyo wa Uganda anatajwa kufikia hatua nzuri kuwa njano na kijani. Okello ambaye ni mchezaji wa Vipers inaelezwa kuwa ni suala la muda kutambulishwa Jangwani. Tetesi zinaeleza kuwa ni miaka miwili ameandaliwa kwenye mkataba wake.

Mohamed Damaro

Mwanzi ilikuwa ni tetesi kwamba amemalizana na mabingwa watetezu Baada ya tetezi wa ligi ya NBC Yanga SC. Hatimaye  dili limekamilika na ameanza kazi Jangwani. Desemba 31 2025 nyota huyo alitambulishwa ikiwa ni saa chache kabla ya kuukaribisha mwaka mpya 2026.

Tayari ndani ya 2026 ameanza kazi katika kikosi hicho. Yupo na timu kambini Zanzibar kwenye NMB Mapinduzi Cup. Yanga SC imefika fainali na itamenyana na Azam FC, Januari 13 2025.

Emmanuel Samuel

usajili Yanga SC umeanza Emmanuel Samuel asaini miwili
Emmanuel Samuel nyota mpya Yanga SC. Source: Yanga SC.

Huyu alitambulishwa Jangwani rasmi Desemba 30 2025 akiwa ni mchezaji wa kwanza kuwekwa wazi kwa mashabiki. Alikuwa ndani ya TRA United tayari ameanza kazi visiwani Zanzibar kwenye NMB Mapinduzi Cup. Mchezaji huyu anapewa nafasi kucheza fainali dhidi ya Azam FC, Januari 13 2026.

Marouf Tchakei kuna jambo

Nyota Tchakei mwanzo wa msimu alikuwa ni mali ya Singida Black Stars. Kwa sasa tayari amesajiliwa na Yanga SC.Utambulisho wake ulikuwa ni kwenye NMB Mapinduzi Cup ambapo jina lake lilijumuishwa kwenye orodha ya wachezaji. Yupo na timu Zanzibar na ameanza kazi katika timu yake mpya.

Ni zawadi ya 2026 kwa mashabiki wa Yanga SC ambao wamekuwa wakiifuatilia timu hiyo. Ingizo hilo jipya linatarajiwa kuongeza ushindani wa namba kwenye eneo la kiungo. Licha ya kuwa sehemu ya kikosi Zanzibar inatajwa kwamba utaratibu wa kupata saini yake haujakamilika asilimia 100 kuna uwezekano akarejea Singida Black Stars.

SOMA HII: Mohamed Damaro Camara ametambulishwa Yanga SC/ Marouf Tchakei anafuata

image

Maneno ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalves

Yanga SC vs AS FAR CAF
Kocha Mkuu wa Yanga SC, Pedro Goncalves. Source: Yanga SC.

Kocha Mkuu wa Yanga SC amesema uwepo wa wachezaji wapya unaongeza ukubwa wa timu hiyo. Amebainisha kwamba anatambua watachuku muda kuitambua falsafa.

“Kuna wachezaji wapya ambao wapo kwenye timu yetu hilo ni jambo jema. Lakini nina amini watatumia muda kuitambua falsafa hivyo tunaanza nao kuwapa kile ambacho kinastahili. Kupitia mashindano ya NMB Mapinduzi itakuwa ni sehemu sahihi kuwatumia na mashindano mengine,” alisema.

Dennis Nkane ni TRA

Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Dennis Nkane ni mali ya TRA United. Mchezaji huyo ameshaanza kazi kwenye timu hiyo mpya akitokea Jangwani. Alikuwa sehemu ya mchezo wa NMB Mapinduzi dhidi ya waajiri wake wa zamani.

SOMA HII: Uganda imeishinda Niger 2-0 kwenye mchuano wa kundi C | Takwimu, magoli na rekodi | Chan 2024

image

Hawa wanatajwa kuondoka

Sure Boy

Kiungo mkabaji Sure Boy anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoondoka Yanga SC. TRA United wanatajwa kuwa kwenye hesabu kuinasa saini yake. Ndani ya kikosi cha Yanga SC kiungo huyo hana uhakika wan amba kikosi cha kwanza.

Conte

Nyota aliyekuwa anatajwa kuwa katika rada za Simba SC Mussa Balla Conte anatajwa kuwa kwenye mpango wa kutolewa kwa mkopo Singida Black Stars.

Farid Mussa

Kiungo Farid Mussa inatajwa kuwa huenda akaondoka Yanga SC. TRA United na Namungo zinatajwa kuhitaji saini yake.Ikiwa mchezaji atakuwa tayari kuna uwezekano akaondoka kwa mkopo.

Hitimisho

Allan Okello mambo fresh Yanga SC ikiwa watafikia makubaliano kwa asilimia 100. Nyota huyo atakuwa ni wanne kutambulishwa Jangwani kwenye dirisha dogo. Tayari wapya wengine wameanza kazi hivyo anasubiriwa Okello kujiunga na mabingwa watetezi wa ligi ya NBC ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.

Share this: