Barcelona vs Real MadridBarcelona vs Real Madrid
  • Moto utawaka Jumapili hii huko Saudi Arabia. Ni katika mchezo wa Fainali ya Supercopa Clasico wa Barcelona vs Real Madrid.
  • Mchezo huu unaozikutanisha timu mahasimu wakubwa, unakuja baada ya timu zote kushinda mechi za Nusu Fainali.
  • Yamal na Mbappe wote wametajwa kuwa tayari kukinukisha wakitokea kwenye majeraha.

Kinawaka Jumapili hii huko Saudi Arabia. Ni katika mchezo wa Fainali ya Supercopa Clasico wa Barcelona vs Real Madrid. Mchezo huu unaozikutanisha timu mahasimu wakubwa unakuja baada ya timu zote kushinda mechi za Nusu Fainali. Barcelona wao walitinga fainali baada ya kuwaondosha Athletic Bilbao kwa kipigo cha mabao 5-0, huku Real wakiikanda Atletico mabao 2-1.

SOMA HII PIA: BARCELONA VS REAL MADRID 26/4/2025, USO KWA USO FAINALI COPA DEL REY

Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

H2H, Barcelona vs Real Madrid

Rekodi ya historia ya soka la ushindani kati ya Barcelona na Real Madrid inaonyesha timu hizi zimekutana mara 82. Barcelona imeshinda michezo 35, huku Real wakishinda mechi 28. Mechi 18 zilimalizika kwa matokeo ya sare, hivyo hii ni nafasi nyingine kwa timu hizi kuandika rekodi mpya.

Fomu ya Barcelona kwenye mechi 5 zilizopita

W W W W W

Fomu ya Real Madrid kwenye mechi 5 zilizopita

W W W W W

Mbappe, Yamal kuanza vikosi tarajiwa Barcelona vs Real Madrid

Barcelona vs Real Madrid
Vita ya makocha

Barcelona

Kipa: J Garcia

Walinzi: Kounde, Cubarsi, E Garcia, Balde

Viungo: Pedri, De Jong, Yamal, Raphinha, Fermin

Mshambuliaji: F Torres

Real Madrid

Kipa: Courtois

Walinzi: Valverde, Asencio, Huijsen, Carreras

Viungo: Camavinga, Tchouameni, Bellingham

Washambuliaji: Rodrygo, Mbappe, Vinicius

SOMA HII ZAIDI: Barcelona’s Epic Showdown: El Clásico 2023 vs Real Madrid

Habari za timu

The final push of the year- ❄️⚽️
The final push of the year

Barcelona wamepata muda mwingi zaidi wa kupumzika kulinganisha na Real Madrid, hii inatajwa kuwa faida kubwa kwao. Kikosi cha Hansi Flick kilionyesha soka la hali ya juu katika nusu fainali, Raphinha akifunga mabao mawili, huku Fermin Lopez, Ferran Torres na Roony Bardghji pia wakifunga mabao. Barcelona inawania kushinda Spanish Super Cup kwa mara ya 16.

Ikumbukwe Barcelona iliifunga Real Madrid 5-2, katika fainali ya mwaka jana. Mabingwa hao watetezi wa La Liga wataandikisha ushindi wa michezo tisa mfululizo kama wataibuka na ushindi kesho Jumapili.

Barcelona wameshinda mechi nne kati ya tano zilizopita dhidi ya Real Madrid, ingawa Real Madrid wameshinda mechi tano kati ya tisa zilizopita. Real Madrid waliiondosha Atletico Madrid katika Nusu Fainali. Federico Valverde alifunga kwa mkwaju wa faulo wa umbali mrefu, kabla ya Rodrygo kuongeza bao la pili mapema katika kipindi cha pili. Alexander Sorloth aliifungia Atletico bao pekee la kufutia machozi. Ikumbukwe Real Madrid wameshinda Kombe la Uhispania la Super Cup mara 13.

Taarifa ya majeruhi

Real Madrid vs Celta Vigo
Mbappe na Vinicius

Barcelona itawakosa tena Gavi (goti), Marc-Andre ter Stegen (haijatajwa) na Andreas Christensen (goti) kutokana na jeraha. Lakini kikosi hicho kiko katika hali nzuri ya majeraha kulinganisha na nyakati nyingine kabla El Clasico.

Lamine Yamal hakuanza nusu Fainali kutokana na utimamu wa kimwili, lakini kocha wake ameweka wazi ataanza kesho Jumapili. Ronald Araujo ana nafasi ya kurejea kikosini, lakini kuna uwezekano, Eric Garcia na Pau Cubarsi wakaanza dimba la kati.

Marcus Rashford, Robert Lewandowski na Bardghji wanatarajiwa kuipa uimara safu ya ushambuliaji ya Barca.

Kwa upande wa Real Madrid, Kylian Mbappe amejiunga na kikosi baada ya kupona jeraha la goti. Mfaransa huyo anaweza kurejea moja kwa moja, kwenye kikosi cha kwanza. Trent Alexander-Arnold (paja), Eder Militao (hamstring) na Brahim Diaz (AFCON) wataendelea kukosekana.

Rodrygo (gonga), Antonio Rudiger (goti) na Raul Asencio (paja) wanahatihati ya kukosekana. Dean Huijsen alikuwa kwenye benchi dhidi ya Atletico baada ya kupona jeraha, sasa anaweza kuanza kama mbadala wa Rudiger.

SOMA HII ZAIDI: MADRID VS BARCELONA MOTO UTAWAKA LEO WEKA MKEKA WAKO SPORTPESA

Hitimisho

Real Madrid vs Celta Vigo

Barcelona vs Real Madrid, mara zote huu huwa mchezo unaobeba ushindani mzito. Unatarajiwa kuwa mchezo wa kuvutia, mchezo huu unatarajiwa kuwa na matokeo ya kushangaza kwa kila upande. Licha ya hayo Barcelona wanapewa nafasi kubwa kuibuka na ushindi.  Tusubiri kuona je, Real watamvua ubingwa Barcelona?

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.