- Marouf Tchakei nyota wa Singida Black Stars anatajwa kukamilisha dili la kusaini Yanga SC.
- Mohamed Damaro Camara ametambulishwa Yanga SC akitokea Singida Black Stars.
- Aziz Andambwile na Balla Conte kuna jambo linakuja Jangwani.
Mohamed Damaro Camara ametambulishwa Yanga SC kuwa mchezaji mpya 2025/26. Nyota huyo alikuwa ndani ya kikosi cha Singida Black Stars. Kiungo huyu mshambuliaji anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa Jangwani. Ni Emmanuel Samuel alikuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa.
SOMA HII: Usajili Yanga SC umeanza Emmanuel Samuel asaini miwili/ Okello mkataba mpya
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Mohamed Damaro Camara ametambulishwa Yanga SC 2025/26

Rasmi Mohamed Damaro Camara ametambulishwa Yanga SC kwa changamoto mpya 2025/26. Huyu ni kiungo mshambuliaji mwenye uwezo wakufunga na kutoa pasi za mwisho. Anatarajiwa kuanza kazi kwenye Mapinduzi Cup.
Baada ya tetesi kueleza kwamba atasaini Yanga SC dili limekamilika. Ni Desemba 31 2025 nyota huyo ametambulishwa ikiwa ni saa chache zimesalia kuukaribisha mwaka mpya 2026. Yanga SC wanaendelea na maboresho katika timu hiyo.
Baada ya Camara nani anafuata Yanga SC?

Bado Yanga SC hawajamaliza kufanya utambulisho kwa wachezaji wapya. Wapo wengine ambao wanatarajiwa kutambulishwa.Yote haya ni kuwa na kikosi cha ushindani ndani ya uwanja.
Mpaka dili lake linakamilika inaelezwa kulikuwa na ofa zaidi ya mbili. Ushawishi wa mabosi wa Yanga SC unatajwa kuwa sababu ya nyota huyo kuchagua kuwa hapo. Matajiri wa Azam FC walikuwa wanatajwa kuwania saini ya kiungo huyo.
SOMA HII: Usajili wa Yanga SC orodha ya wapya 11 msimu wa 2025/26 | Rekodi, magoli na timu walizotoka

Hawa hapa bado kidogo
Allan Okello
Winga Allan Okello raia wa Uganda anatajwa kufikia hatua nzuri kuwa njano na kijani. Okello anaicheza Vipers kwa majukumu yake kwa sasa. Mshahara mnono ametengewa ikiwa atasaini dili jipya ndani ya Yanga SC.
Tetesi zinaeleza kuwa ni miaka miwili ameandaliwa kwenye mkataba wake. Okello ni miezi sita amebakisha kwenye mkataba wake na Vipers. Yanga SC inatarajiwa kufanya mazungumzo na uongozi wa Vipers kupata saini yake.
Marouf Tchakei
Nyota Tchakei ambaye yupo ndani ya Singida Black Stars huenda akasajiliwa na Yanga SC. Nyota huyo inaelezwa yupo tayari kuwa njano na kijani. Hatua ambayo wamefikia kwa sasa tetesi zinaeleza kuwa kuna uwezekano akatambulishwa hivi karibuni.
Huyu anatajwa kuwa ni asilimia kubwa amefikia makubaliano kusaini Yanga SC. Ikiwa dili litajibu hueda ikawa ni zawadi ya mwaka mpya 2026. Hivyo kuwa mchezaji wa tatu kutambulishwa Jangwani.
Hawa hapa wanatajwa kuondoka
Sure Boy
Kiungo mkabaji Sure Boy anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoondoka Yanga SC. TRA United wanatajwa kuwa kwenye hesabu kuinasa saini yake. Ndani ya kikosi cha Yanga SC kiungo huyo hana uhakika wan amba kikosi cha kwanza.
Conte
Nyota aliyekuwa anatajwa kuwa katika rada za Simba SC Mussa Balla Conte anatajwa kuwa kwenye mpango wa kutolewa kwa mkopo Singida Black Stars.
Dennis Nkane
Wonder Kid Dennis Nkane anatajwa kuwa ataondoka dirisha dogo. Kiungo huyu anatajwa kuwa kwenye rada za Namungo FC.

Aziz

Kiungo Aziz Andambwile mara baada ya Romain Folz kuondoka utawala wake umepotea kikosi cha kwanza. Huyu anatajwa kuwa katika rada za Mbeya City na Singida Black Stars. Bado uongozi wa Yanga SC haujatoa taarifa kuhusu Aziz.
Hitimisho
Mohamed Damaro Camara ametambulishwa Yanga SC akitokea Singida Black Stars.Huu ni usajili wa pili Jangwani katika dirisha dogo. Baada ya tetesi za muda mpango kazi umejibu. Endelea kutufuatilia kwa ajili ya taarifa zaidi kuhusu usajili dirisha dogo.

