Uganda vs TanzaniaUganda vs Tanzania
  • Timu mbili majirani Uganda na Tanzania zitavaana kesho Jumamosi.
  • Uganda vs Tanzania ni mchezo ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Stade El Barid mjini Rabat.
  • Unatarajia kuwa mchezo mgumu kwani, kipigo kwa timu yoyote kati ya hizi, inamaanisha ataaga mashindano rasmi.
  • Makala hii inaangazia baadhi ya dondoo muhimu za mchezo huo.

Baada ya kukubali vipigo katika mechi za ufunguzi za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), timu mbili majirani Uganda na Tanzania zitavaana kesho Jumamosi. Uganda vs Tanzania mchezo huu utapigwa kwenye Uwanja wa Stade El Barid mjini Rabat. Kipigo kwa timu yoyote kati ya hizi, inamaanisha atakayepoteza anaaga mashindano rasmi. Makala hii inaangazia baadhi ya dondoo muhimu za mchezo huo.

SOMA HII PIA: AFCON 2025 Matchday 1: stats, Mechi 12, Magoli 29

Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.]

image

H2H, Uganda vs Tanzania

One of Africa’s biggest #TotalEnergiesAFCON---- nights are loading- &#x f ;
Mashabiki Uganda vs Tanzania

Rekodi inaonyesha timu hizi mbili katika siku za karibuni, Uganda na Tanzania zimekutana mara 19 katika mashindano mbalimbali. Uganda wamekuwa na rekodi nzuri zaidi wakishinda mechi 11. Tanzania imeshinda mechi 4 tu, huku michezo  minne iliyosalia ikiisha kwa matokeo ya sare.

Mechi 5 zilizopita za Tanzania

Kuwait 4-3 Tanzania

Iran 2-0 Tanzania

Tanzania 0-1 Zambia

Tanzania 0-1 Niger

Congo 1-1 Tanzania

Mechi 5 zilizopita za Uganda

Morocco 4-0 Uganda

Uganda 2-1 Chad

Algeria 2-1 Uganda

Botswana 0-1 Uganda

Uganda 2-0 Somalia

SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 Mahrez, Jackson, Achouri watikisa: Hawa hapa wafungaji bora wa Raundi ya 1

Vikosi vinavyotarajiwa kuanza

Uganda vs Tanzania
Kikosi cha Uganda

Uganda

Kipa: Magoola

Walinzi: Sibbick, Torach, Obita, Kayondo

Viungo: Ssemugabi, Semakula, Aucho, Mato

Washambuliaji: Lorenzen, Mukwala

Tanzania

Kipa: Foba

Walinzi: Kapombe, Mwamnyeto, Hamad, Hussein

Viungo: Mirishi, Msanga, Msuva, M’Mbobwa, Allarkhia

Mshambuliaji: Samatta

SOMA HII PIA: AFCON 2025 Match round 1: Hawa hapa washindi wa tuzo za mchezaji bora wa kila mechi

Habari za timu

Nigeria 2-1 Tanzania AFCON 2025
Kikosi cha Tanzania

Uganda walianza vibaya kwa kupoteza kwa mabao 3-1 mbele ya Tunisia, katika mchezo wa kwanza wa mashindano hayo. Vijana wa Paul Put watakuwa na hamu ya kuibuka na ushindi mbele ya Tanzania. Uganda wana kazi kubwa kufanikisha hilo kwani kupoteza kwao dhidi ya Tunisia, kunafanya wanakuwa wamepoteza mechi 3 kati ya 4 zilizopita za mashindano yote.

Katika hatua nyingine Uganda wamepoteza mechi sita kati ya tisa za mwisho za AFCON. The Cranes wataingia kwenye pambano hili, wakitafuta kuepuka vipigo vitatu mfululizo kwa mara ya kwanza tangu Novemba 2023. Ikumbukwe kupoteza kunaashiria kukosa nafasi yao ya kusonga mbele, ikizingatiwa kwamba Nigeria inawangoja katika mchezo wao wa mwisho.
Kwa Tanzania hali ni mbaya zaidi kwani katika siku za hivi karibuni, hawajapata ushindi wowote ndani ya michezo 8 mfululizo. Wamepoteza michezo 6 na kutoa sare mechi 2 na mechi za michuano yote (D2, L6), huku mechi zao tano mfululizo zilizopita wakipata vipigo.

Kupoteza kwao mele ya Nigeria siku ya Jumanne kumefanya waandikishe mechi 10 bila ushindi kwenye mashindano ya AFCON wamefungwa mara 7 na kutoa sare 3.

Taarifa za majeraha

Nigeria 2-1 Tanzania AFCON 2025
Mbwana Stars vs Nigeria

Kuhusu majeraha, Uganda hawajaripoti mchezaji yoyote kabla ya mechi yao ya Jumamosi. Kwa Tanzania, Yakoub Suleiman na Feisal Salum, ambao wote walikosa mechi ya kwanza, huenda wakarejea kikosini.

Mlinzi Novatus Miroshi, anayechezea Goztepe ya Ligi Kuu ya Uturuki, alianza kwenye kiungo na alikuwa na kiwango bora.

Hitimisho

Uganda vs Tanzania ni vita ya majirani itakayopigwa Jumamosi hii nchini Morocco. Unatarajia kuwa mchezo mgumu hasa kwa kuwa atakayeruhusu kupoteza ataaga mashindano. Hivyo kila timu itapambana kutopoteza mchezo. Kwa kuangalia fomu yao katika siku za karibuni utabiri wa mchezo huu huenda ukaisha kwa matokeo ya sare.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.