- Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), yanazidi kuchanja nchini Morocco.
- Mashindano hayo yanaingia raundi ya pili (Match day 2), leo Ijumaa baada ya kukamilika kwa Matchday 1.
- Matukio mengi yamevuta hisia kwenye fainali hizi, waswahili husema ‘raha ya mechi bao’. Hivyo matukio ya kufungwa kwa mabao kumewavutia zaidi.
- Makala hii inaangazia mastaa wanaoongoza listi ya ufungaji bora AFCON 2025 Mahrez, Jackson na Ashouri wakitikisa.
Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), yanaendelea nchini Morocco. Mashindano hayo yanaingia raundi ya pili baada ya kukamilika kwa Matchday 1. Matukio mengi yamevuta hisia lakini waswahili husema ‘raha ya mechi bao’. Hivyo matukio ya kufungwa kwa mabao kumewavutia wengi, Makala hii inaangazia mastaa wanaoongoza listi ya ufungaji bora.
SOMA HII PIA: Afcon 2025: Hawa hapa wachezaji 10 wanaolipwa pesa nyingi
hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

AFCON 2025 Mahrez, Jackson, Achouri vinara mabao

Nahodha wa Algeria, Riyad Mahrez ni miongoni mwa wafungaji bora wa raundi ya kwanza. Hii ni baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0. Ushindi huo wa timu yake ilikuwa dhidi ya Sudan. Katika listi hiyo, Mahrez anaunganishwa na mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson na Mtunisia Elias Achouri.
Jackson alifunga mabao hayo katika ushindi wa Senegal dhidi ya Botswana na Achouri alifunga mabao mawili wakati Tunisia ilipoiangamiza Uganda.
SOMA HII ZAIDI: Nigeria vs Tanzania AFCON 2025 – Live Score, H2H, lineups, utabiri, habari za timu
AFCON 2025: Mastaa hawa wamefunga bao 1 kila mmoja

Wachezaji wengine kadhaa pia wamefanikiwa kufunga bao moja baada ya raundi ya kwanza. Mastaa hao ni Pamoja na Mohamed Salah wa Misri, Semi Ajayi na Ademola Lookman wa Nigeria, Amad Diallo wa Ivory Coast, Lyle Foster wa Afrika Kusini, na Marvin Anieboh wa Equatorial Guinea
SOMA HII PIA: Hawa hapa wachezaji 5 wa kuchungwa AFCON 2025 Morocco
Hitimisho:

AFCON 2025 inapoendelea kwenye Match day 2 kuanzia leo Ijumaa. Mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona ni nani ataendeleza moto wa kufunga mabao na hatimaye kuibuka mshindi wa Kiatu cha Dhahabu mwishoni mwa shindano hilo. Ikumbukwe kwenye AFCON 2023 kule Ivory Coast straika na nahodha wa Equqtorial Guinea, Emilio Nsue aliibuka mfungaji bora na mabao yake 5

