Tottenham vs LiverpoolTottenham vs Liverpool
  • EPL inaendelea wikiendi hii, macho ya wengi yatakuwa kwenye mchezo wa Tottenham vs Liverpool.
  • Mchezo huu utapigwa kesho Jumamosi Uwanja wa Tottenham Hotspur.
  • H2H, Liverpool wamekuwa na historia ya ubabe wa ushindi wa mechi 31 dhidi ya 14. Nani atakalishwa kesho cheki uchambuzi huu.

Ligi Kuu England inaendelea tena wikiendi hii, michezo kadhaa itachezwa ila macho ya wengi yatakuwa kwenye mchezo wa Tottenham vs Liverpool. Mchezo huu utapigwa kesho Jumamosi Uwanja wa Tottenham Hotspur. Mabingwa watetezi watakuwa ugenini wakiendelea kujitafuta. Hii ni baada ya kuwa na msururu wa kupoteza mechi katika siku za karibuni.

SOMA HII PIA: Tottenham: Habari Mpya, Ratiba, Vidokezo vya Kubashiri & Uchanganuzi wa Kikosi 2025

Bado hujashinda? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Tottenham vs Liverpool, h2h

Timu hizi mbili zimekutana mara 51 katika historia ya michezo ya ushindani. Liverpool wameshinda mechi 31, huku Spurs wakiibuka na ushindi kwenye mechi 14. Mechi 14 zilizosalia zilimalizika kwa matokeo ya sare.

Mechi 5 zilizopita za Tottenham

Mastaa Spurs
Mastaa Spurs

14 Dec Nottingham Forest 3-0 Tottenham

9 Dec Tottenham 3-0 Slavia Prague

6 Dec Tottenham 2-0 Brentford

2 Dec Newcastle United 2-2 Tottenham

29 Nov Tottenham 1-2 Fulham

Mechi 5 zilizopita za Liverpool

13 Dec Liverpool 2-0 Brighton

9 Dec Inter 0-1 Liverpool

6 Dec Leeds 3-3 Liverpool

3 Dec Liverpool 1-1 Sunderland

30 Nov West Ham 0-2 Liverpool

Fomu za timu katika mashindano yote

Tottenham Hotspur – LLDWWL

Liverpool – LWDDWW

SOMA HII ZAIDI: Premier League Games: A Season of Drama, Decisions, and Destiny

Vikosi tarajiwa Tottenham vs Liverpool

Kikosi cha Spurs (-)
Kikosi cha Spurs

Tottenham Hotspur

Kipa: Vicario

Walinzi: Porro, Romero, Van de Ven, Spence.

Viungo: Palhinha, Bergvall, Kudus, Simons.

Washambuliaji: Kolo Muani Richarlison

Liverpool

Kipa: Alisson

Walinzi: Bradley, Konate, Van Dijk, Kerkez

Viungo: Mac Allister, Gravenberch, Chiesa, Jones,

Washambuliaji: Wirtz, Ekitike

Habari za timu

Tottenham vs Liverpool
Salah

Spurs kwa kiasi wameboresha ushindani wao wakicheza nyumbani, Uwanja wa Tottenham Hotspur katika siku za hivi karibuni. Wameshinda michezo mitatu na kupoteza mmoja tu kati ya mitano yao ya mwisho nyumbani. lakini hilo haliwafariji mashabiki baada ya kipigo Kizito wikiendi iliyopita.

Huko Liverpool nao walikuwa na mambo mengi ya nje ya uwanja. Ugomvi wa staa wa kimataifa wa Misri, Mo Salah na kocha wake uliibua hisia tofauti miongoni mwa wadau wa soka. Lakini yote yalifunikwa wikendi iliyopita, pale Mohamed Salah aliyerejeshwa alipoandika ukurasa mwingine wa historia kwa kutoa asisti ya bao la Ekitike.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 bado huenda hana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza. Lakini alipoingia kutoka benchi alitoa pasi ya bao la Ekitike katika ushindi wa 2-0. Salah aliweka rekodi mpya ya Nyota wenye asisti nyingi zaidi kwa klabu moja akifikisha asisti 277.

Kwa sasa Nyota huyo yupo kuiongoza Misri kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Liverpool huenda wakafaidika na ugomvi huo kwa kuzoea kucheza bila Salah.  Tangu staa huyo aondolewe kwenye kikosi cha kwanza, Liverpool imecheza mechi 5 na haijapoteza mchezo wowote.

SOMA HII PIA: Unveiling the Reds’ Journey: Liverpool Standings & Key Matches in 2024

Mastaa muhimu watakaokosa mchezo huu

Safu ya kiungo ya Tottenham itapungua kutokana na wito wa AFCON, wa staa Pape Sarr na Yves Bissouma wanaoiwakilisha Senegal na Mali mtawalia. Ingawa Bissouma tayari alikuwa nje kwa sababu ya majeraha, na masuala ya nidhamu. Kuhusu hali ya majeruhi spurs ina orodha hii; Dominic Solanke (kifundo cha mguu), Dejan Kulusevski (goti), Destiny Udogie (paja) na James Maddison (ACL).

Wengine ni Radu Dragusin (utayari wa mwili) na Kota Takai (paja). Hawa tayari wameanza mazoezi na huenda wakapata nafasi kuendana na ripoti za matabibu. Inatarajiwa Joao Palhinha na Lucas Bergvall huenda wakaanza dhidi ya Liverpool.

Kwa upande wa mabingwa watetezi, Salah ameondoka kwa majukumu ya AFCON, jambo ambalo linaonekana halitakuwa tatizo kwa Slot. Dominik Szoboszlai alitoka uwanjani na jeraha la kifundo cha mguu dhidi ya Brighton. Mchezaji huyo wa Hungary ambaye hakuonekana vizuri baada ya mchezo, kulingana na Slot ni miongoni mwa majeruhi wawili.

Joe Gomez anasumbuliwa na misuli, wakati huohuo Conor Bradley amerudi. Jeremie Frimpong pia anaweza kuwa karibu kurejea kutoka kuuguza jeraha la paja. Wataru Endo (kifundo cha mguu), Cody Gakpo (misuli) na Giovanni Leoni (ACL) watakosekana.

Hitimisho

Kikosi cha Liverpool (-)
Kikosi cha Liverpool

Tottenham vs Liverpool unatarajiwa kuwa mchezo wa ushindani, hasa kwa kuzingatia nafasi na matokeo yao ya karibuni. Kwa kawaida timu hizi zikikutana mechi zao huzaa mabao mengi, japo hilo halitarajiwi wikiendi hii. Kila timu imefaidi mapumziko mafupi hivyo mvua inyeshe tuone panapovuja.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.