- Fedha za zawadi za Fifa World Cup 2026 zimeongezwa kwa 50%.
- Kwa mara ya kwanza itashuhudiwa Fifa ikitoa dola milioni 50 sawa na zaidi ya Bilioni 123 kwa bingwa.
- Mataifa yote 48 yatakayoshiriki yatapata angalau dola milioni 10.5
Uongozi wa shirikisho la soka la kimataifa (FIFA), umetangaza ongezeko la asilimia 50 la fedha za zawadi itakazotoa kwa timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia la mwaka 2026. Bingwa wa FIFA World Cup 2026 anatarajiwa kujivunia kiasi cha dola 50m sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 123 za Tanzania. Mashindano hayo makubwa zaidi ya soka, yanatarajiwa kuandaliwa kwa Pamoja nan chi tatu za Marekani, Canada na Mexico.
Je, bado hujashinda? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Kuhusu maandalizi ya Fifa World Cup 2026

Zikisalia siku chache kuelekea mashindano hayo makubwa ya soka, tangazo hilo la thamani mpya ya zawadi limezua maoni mesto. Hili linakuja wakati kukiwa na ukosoaji mkubwa kuhusu bei ya tiketi za mashindano hayo. Wakati huu Fifa World Cup 2026, yanatarajiwa kugharimu mgawo wa kifedha wa rekodi wa dola milioni 727.
Washindi wa Kombe la Dunia watapokea dola milioni 50, huku washindi wa pili wakipewa dola milioni 33. Timu zitakazoshindwa kuvuka hatua ya makundi, zitapokea dola milioni 9. Kila timu itakayofuzu itapokea dola milioni 1.5 kwa ajili ya kugharamia maandalizi. Hii inamaanisha kuwa, kila chama mwanachama kinachoshiriki kitahakikishiwa angalau dola milioni 10.5
SOMA HII PIA: Tanzania 0-1 Zambia FIFA World Cup Qualifier 2026 | Highlights, goals, lineup
Kauli ya Rais wa Fifa

Gianni Infantino, Rais wa Fifa amesema malipo hayo yanaonesha kuwa Kombe la Dunia litakuwa la kihistoria. Hii ni kutokana na kwa mchango wake wa kifedha kwa jamii ya soka duniani. Tayari shirikisho hilo limetabiri mapato ya kihistoria ya zaidi ya dola bilioni 13, kwa kipindi cha 2023 hadi 2026.
Tangazo hilo limekuja siku moja baada ya Fifa kutambulisha idadi ndogo ya tiketi za pauni 45 kwa mechi zote 104 za Kombe la Dunia. Hili linafuatia malalamiko makubwa kuhusu mfumo wa bei za tiketi za mashindano hayo. Mwenyekiti wa Chama cha Mashabiki wa Soka, Tom Greatrex, alisema hii inaonesha wazi kuwa, hakuna upungufu wa fedha zinazohusishwa na Kombe la Dunia.
SOMA HII ZAIDI: Chelsea FC 3-0 PSG FIFA Club World Cup 2025 | Cole Palmer, Joao Pedro magoli ya ushindi
Usajili wa manunuzi ya tiketi za Fifa World Cup 2026 uko tayari
Usajili sasa umefunguliwa kwa ajili ya kushiriki mchakato wa kunua tiketi za Kombe la Dunia la Fifa 2026. Ikumbukwe mechi ya ufunguzi ikipangwa kuchezwa katika Uwanja wa Azteca jijini Mexico City tarehe 11 Juni 2026. Baada ya mkutano wa Baraza la Fifa uliofanyika Doha, Fifa ilisema kuwa dola milioni 727 zitasambazwa kwa mataifa wanachama kwa ajili ya Kombe la Dunia la Fifa 2026.
Faida kubwa yakadiriwa kombe la Dunia

Katika marekebisho ya awali ya makadirio yake, Fifa ilisema inatarajia mapato ya kiwango cha rekodi katika kipindi cha miaka minne kinachoishia na Kombe la Dunia la mwaka 2026. Chombo hicho cha utawala wa soka kinatarajia kupata dola bilioni 13 kati ya 2022 na 2026. Kiasi hiki kinalinganishwa na dola bilioni 7.5 katika kipindi cha miaka minne kilichoishia 2022 (ambacho nacho kilikuwa ongezeko kutoka dola bilioni 6.4 katika mzunguko uliotangulia).
Sehemu kubwa ya ukuaji huo ilielezwa na Fifa kuwa umetokana na kupanuliwa kwa Kombe la Dunia na Kombe la Dunia la Klabu za Wanaume, lililofanyika Marekani msimu uliopita wa kiangazi. Hata hivyo, ni asilimia 10 tu ya tiketi ndani ya mgao huo zitakazopatikana kwa bei hiyo. Kwa mfano, katika mechi ya England dhidi ya Croatia, takribani mashabiki 400 tu kati ya zaidi ya 4,000 ndio watanufaika.
SOMA HII PIA: Mbappe World Cup goals 2023/24
Hitimisho
Hamasa ya mashindano ya Fifa World Cup 2026 inazidi kukua, ikiwa imesalia miezi michache mashindano hayo kuanza. mashindano ya mwaka huu yanatajwa kuwa ya kihistoria kutokana na hamasa kubwa ya nchi waandaaji. Licha ya kuwepo vikwazo kadhaa ikiwemo bei za tiketi za kushuhudia mechi hizo, lakini tayari imetabiriwa pato kubwa kupatikana kupitia mashindano hayo.

