- The best Fifa Men’s 11 – 2025 imetangazwa rasmi, huku mastaa wa kikosi cha PSG wakiibuka na ushindi mkubwa.
- Ousmane Dembele amenyakua tuzo la kuwa mchezaji bora wa Fifa kwa wanaume, huku Aitana Bonmati akiendeleza ubabe wake kwa upande wa Wanawake.
- Kiungo wa Barcelona, Raphinha na staa wa Liverpool Mo Salah waibua gumzo kwa mashabiki kwa kukosekana kwenye kikosi cha Best Fifa Men’s 11.
Kikosi cha Best Fifa Men’s 11 – 2025 kimetajwa rasmi huku mastaa ikiwemo Ousmane Dembele, Yamal, Donnarumma, Jude Bellingham na wengineo kujumuishwa kwenye kikosi hiki. Raphinha, Salah na Mc Tomminay ni wachezaji waliokadiriwa kutokosa kwenye kikosi hiki, lakini hawapo kwenye top 11 ya wachezajji bora wa Fifa 2025. Kwenye tuzo za Wanawake, kiungo mshambuliaji wa Spain, Aitana Bonmatti aliibuka mshindi kwa mara ya pili mtawalia. Kocha mkuu wa PSG, Luis Enrique naye aliyeibuka na tuzo ya Fifa best Men’s coach of the year 2025.
SOMA HII PIA: Fifa World Cup 2026: Bingwa kuzoa Bilioni 123
Bado hujashinda? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.
Kikosi Bora cha Wanaume cha FIFA (The Best FIFA Men’s 11)

Kipa:
Gianluigi Donnarumma
Mabeki:
Achraf Hakimi, Willian Pacho, Virgil van Dijk, Nuno Mendes
Viungo:
Cole Palmer, Vitinha, Pedri, Jude Bellingham
Washambuliaji:
Ousmane Dembélé, Lamine Yamal
PSG yatoa mastaa mastaa 6

PSG imeandika rekodi kwa mastaa wake 6 kuingia ndani ya kikosi hiko. Hii ni baada ya kuisaidia timu hiyo kutwaa taji lao la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) na kufika fainali ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA. Mastaa hao ni kipa Gianluigi Donnarumma, Achraf Hakimi, Willian Pacho, Nuno Mendes, Vitinha na Ousmane Dembélé.
SOMA HII PIA: Burundi 0-1 Kenya FIFA World Cup Qualification | Highlights, goals
Lamine Yamal, Cole Palmer achomoza

Mshindi wa Mpira wa Dhahabu wa Kombe la Dunia la Klabu, Cole Palmer, naye pia yumo katika kikosi hicho. Pamoja na nyota chipukizi wa Hispania na Barcelona, Lamine Yamal. Nyota hao wawili walikuwa na msimu bora wakizisaidia timu zao kushinda mataji muhimu.
Washindi wa tuzo hizo wamepatikanaje?
Mastaa hao wamepatikana kufuatia mchakato wa kupiga kura wa kikosi Bora cha Wanaume cha FIFA 2025. Ni vipi kikosi bora cha Wanaume cha FIFA (The Best FIFA Men’s 11) kilivyopatikana?
- Kwa kawaida Tuzo hizi zinawatambua wachezaji bora wa soka katika kipindi cha msimu mpya (kuanzia tarehe 11 Agosti 2024 hadi 2 Agosti 2025).
- Orodha ya waliopendekezwa iliandaliwa na FIFA kwa kushirikiana na wadau wa soka.
- Washindi walichaguliwa na jopo la wataalamu wa soka pamoja na mashabiki, kutoka kote duniani waliojiandikisha kwenye FIFA.com.
- Chaguo kutoka kwa makundi yote mawili mashabiki na jopo la wataalamu yalikuwa na uzito sawa, bila kujali idadi ya wapiga kura katika kila Kundi.
- Wachezaji walipewa pointi kulingana na idadi ya kura walizopata kwa kila nafasi ndani ya kila kundi la upigaji kura.
- Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Wanaume wa FIFA aliingizwa moja kwa moja.
- Mshindi wa Tuzo ya Kipa Bora wa Wanaume wa FIFA alianza akiwa na pointi tisa za alama.
- Nafasi tisa za kwanza zilitolewa kwa wachezaji waliopata pointi nyingi zaidi kulingana na mgawanyo wa nafasi ufuatao: kipa mmoja, mabeki watatu, viungo watatu, washambuliaji wawili.
- Baada ya hatua hizo, wachezaji wawili wa uwanjani waliopata pointi nyingi zaidi ambao hawakuwa tayari wamechaguliwa waliingizwa katika kikosi cha mwaka, kwa kuzingatia idadi ya juu ya wawakilishi kwa kila nafasi kama ifuatavyo: mabeki wanne, viungo wanne, washambuliaji watatu
Raphinha ageuka Gumzo

Staa wa Barcelona na timu ya Taifa ya Brazil, Raphinha ameendelea kuteka vichwa vya Habari na kuwa gumzo. Hii ni baada ya kukosekana kwenye kikosi hiko, na kuacha wengi wakiuliza maswali. Hii ni kutokana na msimu bora ambao alikuwa nao, akiiongoza Barcelona kushinda ubingwa wa La Liga na Copa Del Rey.
SOMA HII ZAIDI: Iran 2-0 Tanzania International FIFA Friendly Match |Highlights, goals, lineups
Hitimisho
Best Fifa Men’s 11 au maarufu kikosi bora cha wanaume cha mwaka kinaendelea kujadiliwa vikali na wadau wa soka. Wapo ambao wanaamini baadhi ya watu walistahili zaidi. Je, wewe msomaji wa SportPesa blog una maoni gani?

