RyanRyan
  • Benni McCarthy Kocha Mkuu wa Harambee Stars alia na mbinu za wapinzani wao kutaka kuwavunja miguu wachezaji.
  • Burundi 0-1 Kenya FIFA World Cup Qualification, wenyeji wakishindwa kupata ushindi mbele ya wenyeji katika dakika 90 za kazi.
  • Kadi nyekundu yatolewa mapema, goli lafungwa na Ogam ambaye alianzia benchi kwenye mchezo huo.

Burundi 0-1 Kenya FIFA World Cup Qualification 2026 matokeo ya mchezo wa kundi F. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Prince Louis Rwagasore, Bunjumbura. Mbinu za Burundi zilikuwa katika kujilinda zaidi huku Kenya ilikuwa kwenye kushambulia zaidi licha ya ugumu waliokutana nao.

SOMA HII: Tanzania 0-1 Zambia FIFA World Cup Qualifier 2026 | Highlights, goals, lineup

Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa

Ni sasa hivi unavuna mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa. Ni rahisi sana hasa ukizingatia Marubani wapo makini. Cheza Aviator upate mgao wako.

image

Burundi 0-1 Kenya FIFA World Cup kocha Harambee Stars hajafurahishwa na wapinzani

Burundi 0-1 Kenya
Nyota wa Kenya akipambania mpira na nyota wa Burundi. Source: Harambee Stars.

Licha ya ubao kusoma Burundi 0-1 Kenya FIFA World Cup Qualification, Kocha Mkuu wa Kenya, Harambee Stars hajafurahishwa na mwendo wa wapinzani. Benni McCarthy amebainisha alikuwa anaona wapinzani Burundi wanakwenda kuwavunja wachezaji wao. Anaamini kiwango walichocheza kilikuwa cha chini kutokana na hofu.

Goli la ushindi lilifungwa kipindi cha pili baada ya dakika 45 milango ya pande zote mbili kuwa migumu. Ni Oktoba 9 2025 mchezo huo ulichezwa. Benni McCarthy amesema wapinzani wao walikuwa wanacheza mchezo wa kutumia nguvu nyingi.

Benny
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars.

Kocha aliongeza kuwa mazingira ya uwanja na mbinu ambazo walikuwa wakitumiza wapinzani zilikuwa zinampa mashaka. Hii ilitokana na mfumo ambao wapinzani walitumia. Jambo hilo lilimfanya awe na hofu huku akifikiria zaidi usalama wa wachezaji.

“Burundi walikuwa wakitumia nguvu nyigi sana. Walikuwa wanakuja kwa kasi sana nadhani kwao ilikuwa ni hali ya kawaida. Lakini nilikuwa nina wasiwasi kuhusu wachezaji wangu kwa kuwa hawakuwa tayari kwa aina ya mchezo ule.

“Mchezo wa mpira kwetu haukuwa na uhalisia namna vile. Kulikuwa na matumizi makubwa ya nguvu jambo ambalo lililikuwa linanipa hofu. Pengine ni aina ya mchezo ambao wao wameuzoea.

“Najua walikuwa wanahitaji ushindi lakini haikupaswa kuwa katika kiwango kile. Nahisi walikuwa wanataka kuwavunja wachezaji miguu. Sijaja Burundi kupata aina hii ya mpira. Wana timu nzuri, wachezaji wazuri lakini lazima wacheze kwa haki mchezo wa mpira,” alisema kocha baada ya mchezo.

Mchezo wa kwanza walipokutana wababe hawa walitoshana nguvu kwa kufungana 1-1. Mchezo wa pili wakiwa ugenini Harambee Stars walipambana na kupata matokeo. Pointi tatu muhimu wanazikusanya wakivuna pointi nne mbele ya Burundi.

SOMA HII: CHAN 2024: Kenya 1-0 Morocco, mpira na matokeo ya ajabu/ Robo fainali imetiki / Magoli, msimamo

image

Goli na kadi nyekundu

 Goli la ushindi lilifungwa na Ryan Ogam dakika ya 75. Mchezaji huyu wa Kenya alianzia benchi alipoingia akafunga.Kadi nyekundu ilitolewa mapema kwa mchezaji wa Burundi Bonfils Caleb Bimenyimana dakika ya 5.

Mfumo wa makocha

Patrick Swanga, Kocha Mkuu wa Burundi alikuwa anatumia mfumo wa 5-4-1. Kocha Mkuu wa Kenya alikuwa anatumia mfumo wa 4-2-3-1. Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.

Msimamo

Harambee
Wachezaji wa Harambee Stars wakishangilia baada ya kufunga mbele ya Burundi. Source: Harambee Stars.

Kutoka kundi F, vinara ni Ivory Coast pointi 23 mechi 9.

Gobon nafasi ya pili pointi 20 mechi 9.

Kenya nafasi ya tatu pointi 12 mechi 9

Burundi nafasi ya nne pointi 11 mechi 9.

Seychelles nafasi ya tano pointi 0 mechi 9

Kikosi cha Burundi vs Kenya

Mlinda mlango

Jonathan Nahimana

Walinzi

B. Kanakimana

Nduwarugira

A.Muderi

O.Moussa

M.Weymans

Viungo

Girumugisha

Bigirimana

H. Msanga

Bimenyimana

Mshambuliaji

V.Mabanza

Wachezaji wa akiba

Mokono Eldhino

Richard Bazombwa

Abedi Bigirimana

Matteo Nkurunzinza

Onesmo Rukundo

Keita Bukuru

Jordi Liongola

Franck Nduwimana

Olivier Dushime

Jospin

Karim Kamana

S. Nahimana

SOMA HII: Tanzania vs Burkina Faso na Kenya vs DR Congo: Wenyeji waanza kwa kishindo CHAN 2024.

image

Kikosi cha Kenya vs Burundi

Mlinda mlango

Brian Bwire

Walinzi                              

Sylvester Owino  

Vincent Harper

Collins Sichenje

 Rooney Onyango

Viungo

Manzur Okwaro

Duke Abuya

Austin Odhiambo 

Adam Wilson

lliam Lenkupae

Mshambuliaji

Michael Olunga

Wachezaji wa akiba

Faroukh Shikhalo

 Byrne

 Omija

Kibwage

Sakari

 T. Ouma

 Stanley

 Nabwire

 Ochieng

 Muchiri

Ogam

 Okoth

Hitimisho

Burundi 0-1 Kenya FIFA World Cup Qualification haukuwa mchezo wenye utulivu kutokana na matumizi ya nguvu. Kadi tatu za njano zilitolewa na mwamuzi kwa Kenya na kadi moja nyekundu kwa Burundi. Mapema wenyeji dakika ya 5 walianza kucheza wakiwa pungufu.

image
Share this: