- Mrithi wa mikoba ya Dimitar Pantev aliyesitishiwa mkataba wake unyamani anatarajiwa kutambulishwa hivi karibuni.
- Kocha mpya Simba SC jina lipo mezani mwa mabosi wa timu hiyo.
- Romain Folz kocha aliyeifunga Simba SC Ngao ya Jamii akiwa Jangwani anatajwa kuwa kwenye orodha.
Kocha mpya Simba SC jina mezani mwa mabosi anasubiriwa kutangazwa kurithi mikoba ya Dimitar Pantev. Hiyo ni muda mchache baada ya kusitisha mkataba na Pantev kutokana na mwendo mbovu wa timu. Ikiwa chini ya Meneja Mkuu Pantev ilipoteza mechi mbili mfululizo CAF Champions League hatua ya makundi.
SOMA HII: Kocha mpya Simba SC CV yake hii hapa | Ratiba ya mechi zijazo CAF Champion League
Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Zamu yako kushinda na SportPesa unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Kocha mpya Simba SC jina mezani mwa mabosi orodha hii hapa

Wakati kocha mpya Simba SC jina likiwa mezani mwa mabosi kuna orodha ya majina yanayotajwa kuomba kazi. Makao makuu ya unyamani inatajwa kuwa zinachambuliwa CV za mrithi mikoba ya Dimitar Pantev. Kwenye orodha hiyo inaelezwa kuwa majina ya makocha Yanga SC yapo pia. Ushindani uliopo katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC unatajwa kuwa sababu makocha wengi kupenda kuja Bongo. Ipo wazi kwamba NBC Premier League ni namba nne kwa ubora Afrika.
Taarifa zinaeleza kuwa muda sio mrefu kocha mpya atatangazwa. Ikumbukwe kwamba baada ya Dimitar Pantev kusitishiwa mkataba wake mikoba yake alikabidhiwa Seleman Matola kwa muda. Taarifa zinaeleza mchakato wa kumpata kocha mpya unaendelea.
Kuna orodha ndefu ya CV ambazo zimetumwa Msimbazi kwa ajili ya kupata kazi hapo.
Miongoni mwa majina ambayo yanatajwa kuomba kazi ni Romain Folz aliyekuwa kocha wa Yanga SC, Mohamed Sahli raia wa Tunisia ambaye aliwahi kuinoa US Monastri.
Mbali na hao pia Lucy Eymael aliyewahi kuinoa Yanga SC. Makocha walionia Yanga SC wanauzoefu na soka la Tanzania ikiwa watapata kazi itarahisisha utendaji. Ni suala la muda mabosi wa timu hiyo kutangaza jina la kocha mpya.
Sifa za kocha mpya
Mabosi wa Simba SC kupitia kwa Mtendaji Mkuu wakati huu wanatajwa kuzingatia zaidi vyeti na uwezo. Pantev hakuwa na sifa za kuwa kocha mkuu hivyo alikuwa anatambulika kuwa ni meneja mkuu. Kocha mpya ajaye anapaswa kuwa na leseni inayokidhi kufundisha ligi kuu ya NBC pamoja na CAF.
SOMA HII: Kocha mpya Simba SC Hemed Morocco hana presha | Ameanza kazi tayari

Mchezo wa mwisho kwa Pantev

Stade de Malien 2-1 Simba SC, CAF Champions League, Novemba 30,2025. Baada ya mchezo huo Simba SC ilitangaza kuachana na kocha huyo aliyekuwa akinoa Gaborone United. Matole mbeba mikoba yake alikaa benchi kwenye mechi mbili mfululizo.
Mechi za Simba SC chini ya Matola
Simba SC 3-0 Mbeya City, Ligi Kuu Bara, Desemba 4,2025.
Simba SC 0-2 Azam FC, Desemba 7,2025.
Katika mechi mbili za ligi, Matola alipata ushindi mchezo mmoja na alipoteza mchezo mmoja. Inaelezwa kuwa huenda Matola akaondoka katika kikosi cha Simba SC kupisha benchi jipya lijalo.
Utambulisho wa kocha mpya Simba SC
Simba SC wanatarajiwa kumtambulisha kocha mpya kabla ya Desemba 28. Hiyo ni maandalizi ya mechi zijazo kwa timu hiyo. Ni Ligi ya Mabingwa Afrika, NBC Premier League, CRDB Federation Cup na Mapinduzi Cup timu hiyo inatarajiwa kushiriki.
SOMA HII: Dimitar Pantev kibarua kimeota nyasi Simba SC/ CAF Champions League matokeo, mrithi wake

Mechi zijazo kwa Simba SC

Es Tunis vs Simba SC, CAF Champions League, Januari 23,2026.
Simba SC vs Mtibwa Sugar, Januari 29,2025.
Simba SC vs ES Tunis, Januari 30,2025, CAF Champions League.
Simba SC vs Singida Black Stars, Februari Mosi,2025.
KMC vs Simba SC, Februari 6,2025 unatarajiwa kuchezwa.
Hitimisho
Kocha mpya Simba SC atakuwa na kazi kurejesha morali ndani ya kikosi na kupambania kuunda safu kali ya ushambuliaji. Kwenye mechi zilizopita timu hiyo imekuwa kwenye mwendelezo wakushindwa kufunga. Licha ya kutengeneza nafasi nyingi katika mechi za kimataifa bado kulikuwa na ugumu kuzibadili ziwe magoli.

