Ellie Mpanzu, Jean Ahoua, Mzamiru Yassin kuondoka Simba SC?Mzamiru
  • Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC anatajwa kuwa katika rada za Raja Casablanca ya Morocco.
  • Ellie Mpanzu winga wa Simba SC huyu inatajwa kwamba kuna timu zinahitaji saini yake huku Yanga SC wakitajwa.
  • Matokeo ya Simba SC katika CAF Champions League na NBC Premier League yatajwa kuwasababu baadhi ya nyota kuhitaji kuondoka.

Ellie Mpanzu, Jean Ahoua, Mzamiru Yassin kuondoka Simba SC? Ni swali ambalo limeanza kuzunguka kwenye vichwa vya mashabiki wa timu hiyo kwa sasa. Ikumbukwe kwamba tunaelekea kwenye dirisha dogo la usajili huku nyota hao wakitajwa kuwa kwenye rada kutoka timu nyingine. Mbali na wachezaji hao matokeo ya hivi karibuni kwa mnyama katika mechi za CAF Champions League, NBC Premier League yanachochea moto kwa wachezaji kubwaga manyanga.

SOMA HII: Simba SC yasajili mashine hizi mbili kwa mpigo, kuelekea Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa

Nafasi yakushinda mamilioni inakusubiri muda huu hivyo amua kucheza Aviator. Ni rahisi sana kupata mgao wako wa mamilioni. Bofya picha hii chini na upaishe Kindege cha SportPesa.

image

Ellie Mpanzu, Jean Ahoua, Mzamiru Yassin kuondoka Simba SC? Hizi hapa timu zinazotajwa

Ellie Mpanzu, Jean Ahoua, Mzamiru Yassin kuondoka Simba SC?
Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC. Source: Simba SC.

Viungo wenye uwezo mkubwa uwanjani Ellie Mpanzu, Jean Ahoua, Mzamiru Yassin kuondoka Simba SC? Kila mmoja kazi yake ni bora uwanjani huku mkongwe Mzamiru Yassin akiwa amepoteza kabisa nafasi kikosi cha kwanza. Kuna timu ambazo zinatajwa kuhitaji saini za nyota hao namna hii:-

Jean Ahoua

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC chaguo la kwanza ndani ya kikosi.Huyu anatajwa kuwa kwenye hesabu za Raja Casablanca ya Morocco. Ikiwa mpango huo utajibu kuna uwezekano akaondoka kikosini.

Ahoua kwa msimu wa 2024/25 alikuwa ni kinara kwenye ufungaji magoli. Alifunga 16 na kutoa pasi 9 za mabao. Alihusika kwenye magoli 25 kwenye kikosi hicho kilichomaliza kikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo.

Ndani ya msimu mpya wa 2025/26 ni miongoni mwa wachezaji waliofanikisha timu kutinga hatua ya makundi. Kwenye CAF Champions League Simba SC ipo kundi D. Alifunga goli moja dhidi ya Gaborone United hatua ya awali.

Steven Mukwala

Mukwala
Mukwala Steven mshambulaji wa Simba SC. Source: Simba SC.

Mshambuliaji wa Simba SC raia wa Uganda anatajwa kuwa katika hesabu za Kaizer Chiefs. Kwa msimu wa 2025/26 bado hajawa kwenye mwendo mzuri kwenye mechi za ushindani. Tetesi zinaeleza kuwa mabosi wa Kaizer Chiefs wameulizia namna ya kuipata saini yake mitaa ya Msimbazi.

Joshua Mutale

Kiungo huyu mshambuliaji ubora wake umeshuka ghafla uwanjani. Kwenye mechi ambazo amecheza msimu wa 2025/26 hajawa imara licha yakupewa nafasi kikosi cha kwanza. Zama za Dimitar Pantev, Mutale alikuwa ni chaguo la kwanza kwenye mechi za ushindani. Tetesi zinaeleza kuwa kwa sasa kuna uwezekano kiungo huyo akaachwa.  

Ellie Mpanzu

Winga tegemeo katika kikosi cha Simba SC anatajwa kuwa kwenye hesabu za kuondoka kwenye kikosi hicho. Sababu ya kuondoka kwake ni kupata changamoto mpya. Miongoni mwa timu ambazo zinatajwa kuhitaji huduma yake ni watani zao wa jadi Yanga SC.

SOMA HII: Ellie Mpanzu kusaini RS Berkane ama Yanga SC | Simba SC yatoa masharti mazito | Magoli na rekodi zake CAF

image

Jonathan Sowah

Mshambuliaji Jonathan Sowah ni ingizo jipya ndani ya Simba SC. Aliibuka hapo akitokea Singida Black Stars.Inatajwa kuwa alikuwa anapigiwa hesabu na Yanga SC. Kuwa kwake ndani ya Simba SC maisha 2025/26 yamekuwa tofauti kwake.

Sio chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Simba SC jambo ambalo linafanya atajwe kuwa kwenye hesabu za kuondoka. Kwenye eneo la ufungaji amekuwa bora ambapo katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania alifunga goli la ushindi akitokea benchi.

SOMA HII: Seleman Mwalimu ametambulishwa Simba SC kwa mkopo akitokea Wydad | Takwimu zake, magoli

image

Mzamiru Yassin

Kiungo mkongwe mwenye uwezo wa kupanda na kushuka anatajwa kuwa ataondoka Simba SC. Kutokuwa na nafasi kikosi cha kwanza ni sababu inayotajwa kumfanya aodoke. Miongoni mwa timu ambazo zinatajwa kuhitaji saini yake ni TRA United na Mbeya City.

Awesu Awesu

Awesu Awesu
Awesu Awesu

Rasta ambaye ni kiungo mshambuliaji ndani ya kikosi cha Simba SC hana nafasi kikosi cha kwanza. Inatajwa kuwa ameomba kuondoka akapate changamoto mpya. Kuna uwezekano akaondoka kwa mkopo. Timu ambayo inatajwa kuhitaji saini yake ni Mbeya City inayotumia Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Katika mechi za ushindani msimu wa 2025/26 nafasi ya Awesu ni Mutale amekuwa akianza.Hata alipokuwa akifanyiwa mabadiliko ni Jean Ahoua alikuwa anapata nafasi ya kuingia. Hivyo tetesi zinaeleza kuwa anaweza kuondoka.

Ahmed Ally, Semaji la Simba SC

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC hivi karibuni aliweka wazi kuwa suala la usajili wakati ukifika kila kitu kitawekwa wazi. Wanatambua umuhimu wa kila mchezaji na kazi ambayo anafanya inaheshimiwa.

“Kila mchezaji ndani ya Simba SC ni bora kutokana na kazi ambayo wanaifanya. Bado kazi inaendelea na wachezaji wanajukumu la kutimiza uwanjani. Ikifika muda wake tutaweka wazi kila kitu nani ataondoka nani atabaki,”.

Hitimisho

Ellie Mpanzu, Jean Ahoua, Mzamiru Yassin kuondoka Simba SC? Ni tetesi zinataja hivyo huku majibu yakitarajiwa kujulikana hivi karibuni. Jina la Mpanzu muda mrefu lilikuwa likitajwa kwa watani wa jadi Yanga SC. Mbali na wachezaji hao kuna orodha ya nyota wengine kutoka unyamani ambao kuna uwezekao wakaondoka.

Share this: