- ‘Dar is white and blue’ ndivyo unavyoweza kusema mara baada ya kumalizika kwa Mzizima dabi
- Simba FC 0-2 Azam FC ndivyo ubao ulivyosoma katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Bara NBC.
- Huku Simba SC wakila kichapo, watani zao Yanga SC hawakamatiki, hii ni baada ya kuicharaza Coastal Union 1-0.
Azam FC imeandika historia nyingine katika Ligi Kuu Bara NBC, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2–0 dhidi ya Simba SC kwenye Mzizima ‘Derby’. Mchezo huo umepigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. wakati Simba SC wakichezea kipigo, watani zao Yanga SC wameibuka na ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union.
SOMA HII PIA: Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2025/26 hii hapa | Mechi za Dabi, kanuni kwa timu ambayo haitafika uwanjani
Bado hujashinda? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Kuhusu mechi za leo za Ligi Kuu Bara NBC

Mzizima dabi ni mchezo uliokuwa na hamasa kubwa, ukikutanisha timu mbili zenye rekodi na historia nzito ndani ya soka la Tanzania. Simba SC walikuwa wakihitaji ushindi kurejesha morali baada ya matokeo yasiyoridhisha katika michezo ya karibuni. Licha ya majaribio kadhaa walijikuta wakipata wakati mgumu kutoka kwa Azam ambayo ilicheza kwa nidhamu, kasi na umakini mkubwa.
SOMA HII ZAIDI: Feisal Salum ‘Feitoto’ ashtua! tetesi za usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26
Simba SC 0-2 Azam FC: Mchezo ulikuaje?

Dakika za mwanzo zilishuhudia Azam wakianza mchezo kwa presha ya juu, wakipiga pasi kwa utulivu na kutengeneza nafasi kupitia upande wa kulia. Licha ya Simba kujaribu kujibu mashambulizi kwa kuingia katikati ya uwanja, walikosa ubunifu wa kutosha kuvunja safu imara ya ulinzi ya Azam. Mpaka dakika 45 za kwanza zinakamilika hakukuwa na mbabe.
Kipindi cha pili kilianza na kasi, huku Simba SC wakitengeneza nafasi nzuri za kupata mabao na kushindwa kuzitumia. Baada ya majaribio kadhaa, Azam FC walipata bao lao la kwanza dakika ya 81 kupitia kwa straika wao Jephte Kitambala. Kitambala alifunga bao hilo kwa kuunganisha krosi kutokea upande wa kushoto.
Dakika 8 mara baada ya bao la kwanza, kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Idd Nado aliifungia timu hiyo bao la 2. Nado alifunga bao hilo kwa kuunganisha krosi iliyopigwa kutokea upande wa kushoto.
Simba walijaribu kusaka mabao ya kusawazisha, lakini mpaka dakika 90 zinakamilika ubao ulisalia kuwa 2-0. Simba walionekana kukosa mwelekeo katika kukamilisha mashambulizi. Baada ya bao la pili, Azam waliongeza umiliki wa mpira na kutuliza mchezo ili kudhibiti kasi ya Simba.
SOMA HII PIA: Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26: Straika mpya Yanga huyu hapa, Chama ‘Out’
Yanga SC hawakamatiki waichapa Coastala Union 1-0

Wakicheza jijini Dodoma, Yanga SC wamefanikiwa kuibuka na ushindi muhimu wa bao 1-0. Ilibidi Wananchi wasubiri mpaka dakika ya 88 kushangilia bao la straika wao Mzimbabwe, Prince Dube. Ushindi huu umewafanya Yanga wazidi kuelekea kileleni mwa msimamo ambako JKT Tanzania wameng’ang’ania kwa muda mrefu.
Sura ya msimamo baada ya mechi za leo

Kwa Azam FC ushindi huu ni wa muhimu, ambapo sio tu kwamba wameongeza pointi 3, bali pia wameongeza morali ya timu na kuthibitisha kuwa wanapambana vikali kwenye mbio za ubingwa. Aam wamefikisha pointi 9 baada ya kucheza mechi 5. Hii inawafanya kukamatia nafasi ya 9 kwenye msimamo.
Baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union, Yanga SC sasa wamepanda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo. Yanga SC wamefanikiwa kufikia pointi 16 baada ya kucheza mechi 6. Yanga SC wamepanda nafasi moja zaidi ya ile waliyokuwepo.
Kipigo kwa Simba na Coasta kinawafanya wasalie na pointi zao zilezile. Simba SC wanasalia nafasi ya 5 na pointi zao 12. Coastal wao wanashuka mpaka nafasi ya 11 na pointi zao 9.
Hitimisho
Azam FC leo wameonyesha kuwa wao ni moja ya timu zinazopigania nafasi ya kuwa bingwa kwa uhalisia, si kwa maneno. Kwa ushindi huu, wanajidhihirisha kuwa ni tishio kubwa kwa timu yoyote ndani ya ligi. Simba SC, kwa upande wao, watalazimika kujipanga upya na kurejea na mbinu bora zaidi.

