MC Alger ya Mokwena yaanza kwa kipigo 2-1 Al Hilal Omdurman CAF Champions LeagueUshindi Al
  • Al Hilal Omdurman ya Sudan vs MC Alger mchezo wa ufunguzi hatua za makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
  • MC Alger ya Mokwena yaanza kwa kipigo 2-1 Al Hilal Omdurman CAF Champions League, Novemba 21,2025.
  • Wanaume 10 wawapiga MC Alger katika mchezo uliokuwa ukifuatiliwa kwa umakini kwenye ardhi ya Kigali, Rwanda, Uwanja wa Amahoro.

MC Alger ya Mokwena yaanza kwa kipigo 2-1 Al Hilal Omdurman CAF Champions League. Ni kwenye mchezo wa hatua ya makundi uliochezwa Uwanja wa Amahoro, Kigali nchini Rwanda. Kocha Mkuu wa MC Alger, Rulan Mokwena alishuhudia rekodi ya kutofungwa mechi 7 zilizopita ikivunjwa na vijana wa Sudan.

SOMA HII: Al Hilal Omdurman vs MC Alger CAF Champions League Novemba 21,2025/ H2H, Live score, lineups, stats, fixture

Paisha ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Sasa ni zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

MC Alger ya Mokwena yaanza kwa kipigo 2-1 Al Hilal Omdurman CAF Champions League ngome zilivunjwa

MC Alger ya Mokwena yaanza kwa kipigo 2-1 Al Hilal Omdurman CAF Champions League
Mokwena Kocha Mkuu wa MC Alger. Source: MC Alger.

Mchezo wa Novemba 21,2025, MC Alger ya Mokwena yaanza kwa kipigo 2-1 Al Hilal Omdurman CAF Champions League. Wenyeji Al Hilal Omdurman walivunja ukuta wa wapinzani dakika ya 45 sekunde chache kabla ya mapumziko. Abdelrazing Omer alifungua ukurasa wa magoli huku upande wa Mokwena ukipata zawadi ya kusawazishiwa na beki Mustafa Karshoum aliyejifunga dakika ya 53. Goli la ushindi lilifungwa na Mohamed Abdel Raman dakika ya 75.

 Wenyeji Al Hilal Omdurman walicheza dakika 3 wakiwa 10 baada ya mchezaji Salaheldin Adil kuonyeshwa kadi mbili za njano na alitoka dakika ya 87. Licha ya kadi hiyo bado walipambana na kulinda ushindi wao. Ni rasmi kampeni zimeanza hatua ya makundi na wenyeji wamepata ushindi nyumbani.

Msimamo kundi C

1.Al Hilal Omdurman pointi 3 mchezo 1
2.Mamelodi Sundowns pointi 0 mchezo 0
3.St Eloi Lupopo pointi 0 mchezo 0
4.MC Alger pointi 0 mchezo 1

SOMA HII: Makundi Klabu Bingwa Afrika CAF 2025/26 haya hapa | Simba SC na Yanga SC zapewa waarabu

image

Kikosi cha Al Hilal Omdurman kilichoanza

Al
Al Hilal Omdurman vs MC Alger. Source: Al Hilal Omdurman

Mlinda mlango
Ouedraogo
Mabeki
Luzolo
Karshoum
Mohamed Ering
Ebuela
Viungo
Salah Adel
Walieldin Khedr
Girumugisha
Abdel Raouf
Coulibaly
Mshambuliaji
Adetunji

MC Alger kikosi kilichoanza

Mlinda mlango
Guendouz
Mabeki
A.Bouguerra
Abdellaoui
Ghazala
Halaimia

Viungo
O.Benhaoua
L.Tabti
K.Zunon

Washambuliaji
Ferhat
S.Bayazid
Z.Naidji

Rekodi za mchezo dakika 90

Al Ahl shangwe

Al Hilal Omdurman wachezaji kwenye mchezo dhidi ya MC Alger. Source: Al Hilal Omdurman

Rekodi zinaonyesha kuwa wababe hawa wawili walitoshana nguvu katika umiliki wa mpira ilikuwa ni asilimia 50 kila timu. Mashuti ambayo Al Hilal Omdurman langoni mwa MC Alger yalikuwa 8 huku MC Alger wakipiga mashuti 6.

Katika mashuti 8 ni mawili yalilenga lango na kuwa magoli huku MC Alger wakiwa hawajapiga shuti ambalo lililenga lango.

SOMA HII: Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League funga kazi hatua ya makundi/ Jezi mpya

image

Mabadiliko ya mchezo

Mabadiliko ya lazima yalifanywa na MC Alger dakika ya 13 baada ya Ayoub Ghezala kupata maumivu nafasi yake ulichukuliwa na Marwane Khelif. Wengine ambao walifanyiwa mabadiliko ni Zakaria Naidji nafasi yake ilichukuliwa na Alhassane Bangoura na Amine Messousa alichukua nafasi ya Soufiane Bayazid dakika ya 62 kwa MC Alger.

Pia Yacine Hamadouche alichukua nafasi ya Kipre Zunon na Aimen Bouguerra alitoka nafasi yake ilichukuliwa na Daniel Illyes Mahdid ilikuwa dakika ya 90 nyota wote wawili.

Al Hilal Omdurman walifanya mabadiliko dakika ya 74 alitoka Abdelrazing Abderraouf Omer nafasi yake ilichukuliwa na Mohamed Abdel Raman, Adam Coulibaly alitoka dakika ya 74 nafasi yake ilichukuliwa na Ahmed M’Bracek. Madicke Kane aliingia dakika ya 81 akichukua nafasi ya Jean Claude Girumugisha.

Hitimisho

MC Alger ya Mokwena yaanza kwa kipigo 2-1 Al Hilal Omdurman CAF Champions League. Hakuna aliyedhania kuona mchezo mkali ukichezwa Kigali. Kwenye kampeni za pointi tisa za nyumbani wenyeji wamevuna tatu bado mechi mbili nyumbani 2025/26.

Share this: