Dabi ya Kariakoo Yanga SC vs Simba SCBoyel vs KMC
  • Ushindi mkubwa kwa mabingwa watetezi Yanga SC wanaupata mbele ya wakusanya mapato ya Kindononi, KMC FC.
  • Yanga SC 4-1 KMC FC NBC Premier League 2025/25 nyasi ziliwaka moto kwa miamba 22 kusaka pointi tatu muhimu.
  • Pacome aliongoza jahazi Yanga SC ikipata ushindi wa 12 mbele ya KMC FC kwenye ligi tangu 2018.

Yanga SC 4-1 KMC FC NBC Premier League ni matokeo rasmi ya mchezo uliochezwa Jumapili, Novemba 9,2025. Ushindi huo unawapeleka kileleni mabingwa watetezi wakiwashusha watani zao wa jadi Simba SC. Hali inazidi kuwa ngumu kwa wakusanya mapato wakibaki kuburuza mkia na pointi 3 baada ya mechi 6.

SOMA HII: Yanga SC vs KMC NBC Premier League Novemba 9,2025

Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

image

Yanga SC 4-1 KMC FC NBC Premier League Pacome aliteka shoo

Yanga SC 4-1 KMC FC NBC Premier League
Pacome kiungo mshambuliaji wa Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Wakati ubao wa Uwanja wa KMC Complex ukisoma Yanga SC 4-1 KMC FC NBC Premier League kiungo Pacome Zouzoua aliteka shoo. Kazi kubwa alifanya kwa kushirikiana na wachezaji wenzake kusaka pointi tatu. Kutokana na kiwango alichoonyeshwa alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.

Pacome katika mchezo huo alifunga goli moja dakika ya 72 kwa pasi ya Prince Dube. Goli la ufunguzi lilifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 72. Magoli mawili yalifungwa na Andy Boyeli dakika ya 82 na 90+3.

Boyel alianzia benchi alichukua nafasi ya Dube. Kuingia kwake kuliongeza kasi ya kulishambulia lango la KMC FC ambao wao goli lao lilifungwa na Daruesh Saliboko dakika ya 42.

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26

  1. Yanga SC pointi 10, mechi 4.
  2. Simba SC pointi 9, mechi 3.
  3. Pamba Jiji pointi 9, mechi 6.
  4. Mbeya City pointi 8, mechi 6.
  5. Mashujaa FC pointi 8, mechi 6.

16. KMC FC pointi 3, mechi 6.

SOMA HII: Ratiba ya Yanga SC 2025/26 NBC Premier League, CAF

image

Yanga SC wababe kwa KMC FC

Rekodi zinaonyesha tangu 2018 timu hizi zimekutana mara 15. Yanga SC imepata ushindi mara 12, KMC FC ushindi mara moja, sare ni 2. Hivyo Yanga SC wamekuwa wababe mbele ya KMC FC wanapokutana.

Mechi 6 za KMC FC Tanzania Premier League ushindi mara moja

Prince Dube vs KMC FC
Prince Dube vs KMC FC NBC Premier League: Source: Yanga SC.

17/09/2025, KMC FC 1-0 Dodoma Jiji FC.
23/09/2025, KMC FC 0-1 Singida Black Stars.
27/09/2025, Tanzania Prisons 1-0 KMC FC.
18/10/2025, KMC FC 0-3 Mbeya City
25/10/2025, Fountain Gate FC 1-0 KMC FC.
09/11/2025, Yanga SC 4-1 KMC FC.

Kikosi cha Yanga SC kilichoanza dhidi ya KMC FC

Mlinda mlango

Djigui Diarra

Mabeki

Israel Mwenda

Zimbwe Jr

Dickson Job

Bakari Nondo

Viungo

Duke Abuya

Maxi Nzengeli

Mohamed Doumbia

Offen Chikola

Pacome Zouzoua

Mshambuliaji

Prince Dube

Wachezaji wa akiba wa Yanga SC

Boka vs KMC
Wachezaji wa Yanga SC mchezo dhidi ya KMC FC. Source: Yanga SC.

Balla Conte

Lassine Kouma

Khomeiny Abubakary

Ecua Celestine

Chadrack Boka

Aziz Andambwile

Shekhan Ibrahim

Andy Boyel

Abdulnassir Abdallah

Abubakar Othman

SOMA HII: Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar NBC Premier League,2025

image

Kikosi cha KMC kilichoanza dhidi ya Yanga SC

Hamisi Athuman
Kenny Ally
Redemtus Mussa
Salum Athuman
Rashid Chambo
Daruesh Saliboko
Juma Mwita
Samson Mwaituka
Nickson Mosha
Ibrahim Nindi
Kelvin Tondi

Wachezaji wa akiba wa KMC FC

Ibrahim Ajib

Ismail Gambo

Juma Shemvuni

Hance Masoud

Elly Kayombo

Goodluck Bosco

Oscar Paulo

Ahmed Pipino

Fabien Mutombora

Abdalla Said

Hitimisho

Yanga SC 4-1 KMC FC NBC Premier League matokeo haya yanamuweka kwenye wakati mgumu kocha Marcio Maximo. Kwa msimu wa 2025/26 wakusanya mapato hawajawa kwenye mwendo mzuri. Kutokana na kupoteza pointi tatu kwa mara nyingine kuna hatihati kocha huyo kufutwa kazi.

Share this: