Clement MzizeClement Mzize
  • Taarifa za kushtusha zimetolewa na uongozi wa Yanga SC kumhusu straika wao, Clement Mzize.
  • Nyota huyo aliyechaguliwa kuwania tuzo ya bao bora la mwaka CAF Champions League yupo hatarini.
  • Msimu uliopita Mzize alihusika katika mabao 19 ya Yanga SC ambapo, alifunga mabao 14 na kutoa pasi 5 za mabao.

Hivi karibuni uongozi wa Klabu ya Yanga SC ulitangaza kuwa mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Clement Mzize anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili hadi na nusu. Hii ni baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa goti. Upasuaji huo umekuja kutokana na majeraha ambayo Mzize aliyapata Septemba 19, 2025 katika mechi dhidi ya Wiliete ya Angola.

Ushindi mzito wa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Sasa ni zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

Nini kimemtokea Clement Mzize Yanga?

Huu ulitarajiwa kuwa msimu bora zaidi kwa Mzize ndani ya Yanga SC, hasa baada ya Nyota huyo kufanya makubwa msimu uliopita lakini imekuwa kinyume na matarajio. Swali ni je, nini kimemkuta Clement Mzize? Ukweli ni kwamba msimu huu Mzize hajaanza vizuri kulinganisha na msimu jana.

Hizi hapa takwimu za Mzize za msimu uliopita

Mzize namba
Mzize namba

Msimu uliopita Mzize alihusika katika mabao 19 ya Yanga SC ambapo, alifunga mabao 14 na kutoa pasi 5 za mabao. Hii ilimfanya Mzize kuwa mchezaji mzawa aliyefunga mabao mengi akifuatiwa na Nassor Saadun wa Azam FC. Saadun yeye ameifungia Azam FC mabao nane, sawa na Paul Peter wa Dodoma Jiji.

SOMA HII PIA: Clement Mzize Waarabu waikomalia saini yake | Mkataba wake upo hivi | Takwimu, magoli

Aipeleka Taifa Stars Robo Fainali ya CHAN 2024 kwa mara ya kwanza.

Clement Mzize
Mzize Stars

Ukiachana na Klabu, Mzize pia amekuwa na wakati mzuri akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ndani ya msimu uliopita. Mzize alikuwa karata maalum ya kuibeba Stars katika safari ya kwanza ya kihistoria, ya kufuzu Robo Fainali ya mashindano ya CHAN 2024. Mabao yake mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Madagascar yaliipeleka Stars Robo Fainali.

Mabao ya Tanzania yalifungwa na Clement Mzize dakika ya 13 na 20. Goli la Madagascar lilifungwa na Nantenaina Razafimahatana dakika ya 34. Ikumbukwe magoli yote matatu yalifungwa kipindi cha kwanza. Katika mchezo wa mapema wa kundi B, Afrika ya Kati walipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Goli la Mauritania lilifungwa na Ahmed Ahmed dakika ya 9. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa. Goli hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Katika mashindano hayo Tanzania walikuwa wenyeji na kuandika rekodi nzuri ya ushindi wa asilimia 100, katika michezo ya hatua ya makundi. Kiwango chake katika mashindano haya kilizivutia timu kubwa ndani na nje ya Tanzania.

SOMA HII ZAIDI: Baada ya Aziz Ki: Mzize na Aucho wanaondoka Yanga? Tetesi usajili bongo

Ofa zamiminika kusaka Saini ya Mzize

Mzize VS Wiliete
Mzize VS Wiliete

Kiwango bora ambacho staa huyo alikionyesha kwenye Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024), kilifanya thamani ya mzize kuzidi kupaa. Baadhi ya timu kubwa kutoka ndani na nje ya Tanzania ziliingia vitani kusaka Saini yake.

Awali mchezaji huyo alihusishwa na klabu kutoka Ubelgiji, Misri, Afrika Kusini na Morocco kabla ya kuibuka taarifa ya ofa nyingine kutoka Qatar. Timu nyingine ambazo zimetajwa kusaka Saini ya Mzize ni pamoja na: Zamalek FC ya Misri, Esperance ya na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Mzize msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania ya NBC 2024/25 alikuwa chaguo la kwanza. Alicheza mechi 30 na timu hiyo ilitwaa ubingwa ikiwa na pointi 82. Katika mechi hizo 30 Mzize alitumia dakika 1,877.

SOMA HII PIA: Usajili Yanga SC: Clement Mzize haendi popote | Takwimu muhimu, magoli, mechi | Kariakoo Dabi

Walichosema Yanga SC kuhusu kuondoka kwa Mzize

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC alibainisha kuwa kuna ofa za kumhitaji Mzize. Kamwe alisema: “Kuhusu Clement Mzize bado ni mchezaji wa Yanga SC. Ana mkataba wa miaka miwili ambayo alisaini. Mengi yanasemwa kuhusu yeye lakini bado tupo naye kwenye timu.

“Tulipokea ofa nyingi sana ambazo zinamuhusu, wakati Mzize anaboresha mkataba wake aliambiwa anapaswa kupambana ndani ya msimu mpya. Hilo amelifanya na kazi yake imeonekana.”

Hitimisho

Mzize Hospitali
Mzize Hospitali

Ikiwa ni takribani mwaka mmoja na siku kadhaa zimepita tangu ‘saga’ za usajili wa Clement Mzize zishike kasi, na kushuhudia mshambuliaji huyo akisaini kandarasi ya miaka miwili hadi 2027. Mzize amepigwa pigo kubwa la jeraha ambalo linamuweka nje kwa muda mrefu kiasi. Hofiu imekuwa kubwa ikiwa thamani ya staa huyo itaendelea kusalia kuwa sio chini ya Sh. Bilioni 2.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.