NBC Tanzania Premier League table 2025-26.Pacome na kocha
  • Yanga SC vs Mtibwa Sigar NBC Premier League Oktoba 28,2025 kutimua vumbi kwa wababe wawili uwanjani.
  • Patrick Mabedi kocha msaidizi wa Yanga SC amebainisha kuwa watakabiliana na upinzani mkubwa uwanjani.
  • Uwanja wa KMC Complex saa 10:00 jioni mchezo huo utapigwa katika msako wa pointi tatu muhimu.

Yanga SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier League leo ni mchezo mkali kwa wababe wawili. Timu hizi zitashuka Uwanja wa KMC Complex saa 10:00 jioni kusaka pointi tatu Oktoba 28,2025. Mabingwa watetezi Yanga SC kwenye msimamo ni nafasi ya 13 wakiwa na pointi 4 baada ya mechi mbili. Mtibwa Sugar ya Morogoro ni pointi 5 wamekusanya baada ya mechi 4 nafasi ya 8 kwenye msimamo.

SOMA HII: Matokeo ya Yanga SC 2025/26 | Wafungaji, magoli, ratiba ya mechi zijazo

Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

Yanga SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier League nani atakosekana?

Yanga SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier League
Ibrahim Bacca beki wa Yanga SC atakosekana mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar. Source: Yanga SC.

Kuelekea Yanga SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier League kuna wachezaji ambao watakosekana. Kwa upande wa wenyeji, mshambuliaji Clement Mzize atakosekana. Nyota huyu anasumbuliwa na maumivu ya goti. Ibrahim Bacca beki wa Yanga SC atakosekana kwenye mchezo kutokana na adhabu anayoitumikia.

Tarehe ya mchezo yabadilishwa

Awali mchezo huu ulipangwa kuchezwa Oktoba 29,2025 siku ya kesho. Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe alibainisha kuwa ratiba ilibadilishwa. Hivyo ni leo Oktoba 28,2025 mchezo utachezwa.

“Awali mchezo ulikuwa umepangwa kuchezwa Oktoba 29,2025. Lakini kutokana na sababu mbalimbali ratiba imebadilishwa. Hivyo Wanayanga mjitokeze kwa wingi Oktoba 28,2025 kwenye mchezo wetu,” alisema Kamwe.

Maoni ya Patrick Mabedi kocha msaidizi wa Yanga SC

Mabedi
Mabedi, kocha msaidizi wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Patrick Mabedi, kocha msaidizi wa Yanga SC amebainisha kuwa wanatambua mchezo utajuwa mgumu wapo tayari kwa ushindani. Kocha huyo ameongeza kwamba wanachohitaji ni matokeo mazuri.

“Tunatambua kwamba mpinzani wetu ni mgumu. Licha ya hayo tumefanya maandalizi mazuri hivyo tupo tayari.Tutawakabili wapinzani wetu kwa nidhamu mpango mkubwa ikiwa ni kutafuta matokeo uwanjani,”.

H2H

13/05/2024 FT: Mtibwa Sugar 1-3 Yanga SC
16/12/2023 FT: Yanga SC 4-1 Mtibwa Sugar
31/12/2022 FT: Mtibwa Sugar 0-1 Yanga SC
13/09/2022 FT: Yanga SC 3-0 Mtibwa Sugar
29/06/2022 FT: Yanga SC 1-0 Mtibwa Sugar
23/02/2022 FT: Mtibwa Sugar 0-2 Yanga SC
20/02/2021 FT: Yanga SC 1-0 Mtibwa Sugar

SOMA HII: Romain Folz amefukuzwa Yanga SC mrithi mikoba yake huyu hapa

image

Ushindi mkubwa

16/12/2023, Yanga SC 4-1 Mtibwa Sugar
13/05/2024, Mtibwa Sugar 1-3 Yanga SC

Mechi 5 zilizopita za Yanga SC

Duke vs Silver
Duke vs Silver Strikers mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Source: Yanga SC.

Septemba 24,2025 – Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).

Oktoba 27,2025 -Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).

Septemba 30,2025, Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).

Oktoba 18,2025, Silvers Strikers 1-0 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika)

Oktoba 25,2025, Yanga SC 2-0 Silver Strikers, (Ligi ya Mabingwa Afrika)

Mechi 5 zilizopita za Mtibwa Sugar

22/10/2025, Dodoma Jiji 0-0 Mtibwa Sugar
19/10/2025, Mtibwa Sugar 0-0 Coastal Union
28/09/2025, Mtibwa Sugar 2-0 Singida Fountain Gate
21/09/2025, Mashujaa FC 1-0 Mtibwa Sugar
11/10/2024, Mtibwa Sugar 1-0 Songea United

Mechi zijazo kwa Mtibwa Sugar

02/12/2025, JKT Tanzania vs Mtibwa Sugar
29/11/2025, Mtibwa Sugar vs TRA United
25/11/2025, KMC vs Mtibwa Sugar

Kikosi cha Yanga SC vs Mtibwa Sugar kinachotarajiwa kuanza

Kipa

Djigui Diarra

Mabeki

Israel Mwenda

Zimbwe Jr

Dickson Job

Nondo

Viungo

Duke Abuya

Maxi Nzengeli

Aziz Andambwile

Pacome

Doumbia

Mshambuliaji

Dube

SOMA HII: Beki Ibrahim Bacca wa Yanga SC amefungiwa mechi 5 na TPLB

image

Kikosi cha Mtibwa Sugar kinachotarajiwa kuanza dhidi ya Yanga SC

Toba Kutisha, Oscar Masai, Haroun Evod, Omar Selemani, Ibrahim Imoro, Kassim Msafiri, Twalibu Muhenga, Andrea Simchimba, Abdul Hilary, Magata Charles na Omary Manga.

Hitimisho

Yanga SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier League utawakutanisha miamba wawili Uwanja wa KMC Complex. Ni vita ya kusaka pointi tatu uwanjani. Wananchi wanapewa nafasi kubwa kushinda mchezo huo ambao Mtibwa Sugar nao wanahitaji ushindi. Je Mtibwa Sugar watakubali kupoteza ugenini? Matokeo utayapata hapahapa.

Share this: