- Mara baada ya kupewa jukumu la kuiongoza Simba SC, Hatimaye meneja mkuu Pantev anaanza kazi rasmi.
- Nsingizini Hotspurs vs Simba SC, hu ndio mtihani wa kwanza kwa Pantev ambao mashabiki wanasubiri majibu.
- Wasifu (CV), ya meneja mkuu Pantev imesheheni mafanikio makubwa, sasa ni wakati wa kuandika historia mpya hapa Tanzania.
Simba SC vs Nsingizini Hotspurs mechi kali inayotarajiwa kupigwa Jumapili Oktoba 19, 2025 ndio mtihani wa kwanza kwa meneja mkuu mpya wa kikosi hiko, Dimitar Pantev. Hii ni baada ya mkufunzi huyo, kutangazwa kuchukua mikoba ya kuinoa Simba SC Oktoba 3, mwaka huu. Swali kubwa sasa ni Je, kocha huyo atafaulu mtihani huo?
SOMA HII PIA: Kuelekea Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champion League 2025
Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Kuhusu mechi ya Nsingizini Hotspurs vs Simba SC

Huu ni mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya pili ya awali, ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mchezo huu na ule wa marudiano unaotarajiwa kupigwa Oktoba 26, mwaka huu ndio utatoa tiketi ya timu gani inaenda hatua ya makundi. Mshindi wa jumla wa mechi hizo mbili atajiweka kwenye nafasi ya kufuzu hatua ya makundi.
SOMA HII ZAIDI: Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League | H2H, kikosi kilichosafiri, utabiri
Mchezo huu una maana gani kwa Meneja Pantev?
Ikumbukwe Meneja mkuu Pantev ambaye ni raia wa Bulgaria anakuja kuchukua majukumu yaliyoachwa na kocha, Fadlu Davis aliyetimkia Raja Casablanca. Pantev amejiunga na Simba SC akitokea ndani ya kikosi cha Gaborone United. Simba ilipata mafanikio makubwa na ya haraka chini ya kocha Fadlu, huu unabaki kuwa mtihani mwingine kwa Pantev.
Ikumbukwe chini ya Fadlu Simba SC msimu uliopita waliibuka washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika. Hii ni baada ya matokeo ya jumla ya kipigo cha mabao 3-1, katika michezo miwili ya fainali. Hivyo mchezo huu unarasimisha safari ya Pantev rasmi ndani ya Simba SC.
Makubaliano ya Simba SC na Pantev
Simba SC ililazimika kuilipa fidia Gaborone United, ili kumpata meneja huyo. Hii ilikuwa ni sehemu ya makubaliano ya kufanikisha uhamisho kwa kuwa bado alikuwa na mkataba. Ndani ya Simba inaelezwa Pantev amesaini kandarasi ya miaka 2.
Wasifu (CV), ya meneja mkuu Pantev

Pantev mwenye umri wa miaka 49, ni mzaliwa wa Varna, Bulgaria. Mkufunzi huyo ana urefu wa mita 1.79 ambaye aikuwa akihudumu kama kiungo wa ulinzi, na ulinzi wa kati wakati akiwa mchezaji. Amecheza soka kwenye klabu mbalimbali za kwao Bulgaria ikiwemo Spartak Varna.
Katika taaluma yake ya kufundisha soka ana rekodi nzuri ya mafanikio, katika klabu tofauti barani Afrika. Akiwa kocha wa Gaborone United, aliongoza timu hiyo kushinda Ubingwa wa Ligi nchini Botswana msimu uliopita 2024/25. Pia amefanya vyema akiwa kocha wa Victoria United nchini Cameroon.
Pantev anasifika zaidi kwa falsafa ya soka la kushambulia na umiliki wa mchezo. Falsafa hii ilishuhudiwa katika michezo yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba SC. Katika michezo hiyo miwili licha ya Simba kupata ushindi wa jumla wa mabao 2-1 na kufuzu, lakini walikumbana na ushindani mkubwa.
SOMA HII PIA: Kocha mpya Simba SC CV yake hii hapa | Ratiba ya mechi zijazo CAF Champion League
Malengo ya Simba SC na mtihani kwa Pantev

Kazi kubwa ambayo uongozi wa Simba umempa mkufunzi huyo, ni kurejesha utawala wao ndani ya ligi ya Tanzania. Hii ni baada ya utawala huo kuchukuliwa na watani zao wa Jadi Yanga SC kwa misimu 4 mfululizo. Mtihani mwingine mkubwa wa kocha huyo mpya ni kuhakikisha Simba SC inaleta ushindani mkubwa kwenye mashindano ya kimataifa, hasa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ni wazi kuwa kocha huyo atakabiliwa na changamoto ya kuunganisha kikosi kipya. Kuweka mfumo wa ufundishaji unaolingana na matarajio ya mashabiki. Mwisho atapaswa pia kushindana na timu kadhaa zilizo na nguvu ndani na nje ya Tanzania.
Hitimisho
Nsingizini Hotspurs vs Simba SCni nafasi nyingine kwa Pantev kuthibitisha ubora wake wa kimbinu. Mchezo huu unasubiriwa kwa hamu na Wanasimba wote na wadau wa michezo, ili kuanza kumfanyia tathimini kocha huyo. Ni wazi mkufunzi huyo atatamani kuanza na rekodi nzuri ya ushindi. Faida kubwa kwake ni mchezo huo, kupigwa eneo la kijiografia analolifahamu.


