Romain Coach
  • CAF Champion League Oktoba itakuwa moto kwa mechi kupigwa uwanjani mzunguko wa pili.
  • Yanga SC vs Silver Strikers inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Bingu-Malawi, Oktoba 18, 2025.
  • Silver Strikers ilitinga hatua ya pili kwa faida ya goli la ugenini huku Yanga SC ikipata ushindi wa jumla ya magoli 5-0 Wiliete SC ya Angola.

Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champion League ni ngazi kwa mabingwa hao kutinga hatua ya makundi. Clement Mzize na Dickson Job warejea kwenye kikosi cha Yanga SC na kuwapa motisha kwenye mechi ijayo. Wawakilishi wa Tanzania Yanga SC wataanzia ugenini na kumalizia nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa.

SOMA HII: Wiliete SC 0-3 Yanga SC CAF Champions League 2025 | Magoli yote, takwimu muhimu, super sub

Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

Yanga SC vs Silver Strikers utachezwa lini?

Yanga SC vs vs Silver Strikers
Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC Maxi Nzengeli akiwa mazoezini. Source: Yanga SC.

Kwenye anga la kimataifa kuna mchezo mkali unaosubiriwa kwa shauku kubwa. Ni Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League. Huu ni mchezo wa hatua ya pili unatarajiwa kuchezwa Oktoba 18, 2025 nchini Malawi saa 10:00 jioni.

Mchezo wa pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Oktoba 25, 2025. Huu ni mchezo ambao utaamua timu ipi kati ya hizi mbili kutinga hatua ya makundi. Yanga SC ina kibarua kigumu ugenini na nyumbani katika kufikia malengo kama ilivyo kwa wapinzani.

Yanga SC wamefikaje hapo kimataifa?

Aziz Andambwile (-)
Aziz Andambwile kiungo wa Yanga SC na Prince Dube kwenye moja ya mchezo wa ushindani.Source: Yanga SC.

Yanga SC imetinga hatua ya pili kwa kuipiga Wiliette SC kwa jumla ya magoli 5-0. Ugenini ilipata ushindi wa magoli 3-0. Huku mchezo wa pili ikiibukia Yanga SC 2-0 Wiliette SC.

Kwenye mchezo uliopita kiungo mkabaji alitisha kwa kupiga magoli nyumbani na ugenini. Je kwenye mchezo huu ujao, Aziz ataendeleza rekodi yake ya kufunga magoli kwenye CAF Champions League?

SOMA HII: Yanga SC watachuana na vijana wa Angola Wiliete SC kwenye CAF Champions League 2025

image

Wapinzani wa Yanga SC Silver Strikers walifikaje?

 Silver Strikers ya Malawi iliwafungashia virago Elgeco Plus ya Madagascar kwa faida ya goli la ugenini.
Katika mchezo wa kwanza walipokutana Septemba 21, 2025 Elgeco Plus waiibuka sare na Silver Strikers ya 1-1. Mchezo wa kuamua mshindi ulichezwa Septemba 27 2025, ambapo bado hawakufungana magoli Silver Strikers 0-0 Elgeco Plus.

Mechi 6 zilizopita kwa Yanga SC inayoshiriki NBC Premier League

Mudathir
Mudathir Yahya kiungo mkabaji wa Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki)

Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii).
Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).
Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).

Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).

SOMA HII: Yanga SC vs Pamba Jiji FC Septemba 24 | Vikosi, H2H, utabiri, milioni 15 zakunjwa

image

Mechi 6 Silver Strikers ambayo inashiriki Malawi Super League

Silver Strikers 1-0 Chitipa United, mchezo wa League Agosti 27 2025.

Shire FC 1-4 Silver Strikers, Septemba 11 2025 Malawi Cup

Elgeco Plus 1-1 Silver Strikers, Septemba 21 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Silver Strikers 0-0 Elgeco Plus Septemba 27 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Blue Eagles 0-3 Silver Strikers Oktoba 2 2025, Malawi Cup.

Bullets 2-1 Silver Strikers Oktoba 5 2025, Malawi Cup.

Makocha kwenye vita ya ushindi kimataifa

Romain Folz kuondoka Yanga SC
Romain Folz,Kocha Mkuu wa Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Makocha wawili watakuwa kwenye vita ya kusaka ushindi uwanjani katika mchezo wa kimataifa. Yanga SC ipo chini ya Romain Folz na Silver Strikers ipo chini ya kocha Pieter de Jongh.

Hitimisho

Yanga SC vs Silver Strikers utakuwa mchezo wa kukata na shoka. Wananchi wanapewa upato wa kushinda mechi hii. Je, Silvers Strikers wakali wa Malawi watawapiga wababe wa Tanzania? Fuata habari za hivi sasa kuhusu huu mchezo kupitia SportPesa Blog.

Bonyeza hapa chini na ujishindie mamilioni kwa kucheza SportPesa Supa Jackpot 17

image

Share this: