Simba SC 3-0 Fountain Gate FCAhoua vs Fountain Gate (-)
  • Feisal Salum wa Azam FC na Rushine De Reuck wa Simba SC ni vinara chati ya ufungaji 2025/26.
  • Mfungaji bora 2024/25 Jean Ahoua ataivunja rekodi yake msimu mpya wa 2025/26?
  • Vigezo vya ufungaji NBC hakuna vipengele vingi kwa mchezaji nafasi yoyote ile.

Furaha ya mechi ni magoli na yule anayefunga kuliko wengine hutwaa tuzo yake msimu unapofika tamati. Mfungaji bora 2024/25 Jean Ahoua kwenye Ligi Kuu Bara ya NBC alimaliza akiwa na magoli 16, anatarajiwa kupokea tuzo yake Desemba. Tayari msimu mpya wa 2025/26 umeanza je, Jean Ahoua ataivunja rekodi ya kufunga magoli mengi na kutengeneza pasi nyingi za magoli?

SOMA HII: Jean Ahoua kubeba tuzo kiatu cha ufungaji bora 2024/25/ Orodha ya wafungaji

Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

Mfungaji bora 2024/25 Jean Ahoua kuivunja rekodi yake?

Mfungaji bora 2024/25
Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Jean Ahoua 2024/25 alifunga magoli 16 ni mfungaji bora. Ahoua alitengeneza pasi 9 za magoli akihusika kwenye magoli 25 kati ya 69 yaliyofungwa na Simba SC. Ni mkali kwenye kufunga magoli ya kutengwa ambapo alifunga kwa mapigo huru magoli mawili na alifunga kwa penati magoli 6.

Ahoua ndani ya Stella Club d’Adjame msimu wa 2023/24 rekodi zinaonyesha kuwa alifunga mabao 12. Mbali na kufunga mabao hayo 12 alitoa pasi 9 za mabao. Hivyo msimu mmoja alihusika kwenye jumla ya magoli 21. Kutokana na mchango wake huo alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora 2023/24, (MVP).

Magoli yake 16 ndani ya ligi

Katika magoli 16 ambayo kafunga, magoli 15 kafunga kwa mguu wa kulia. Goli moja alifunga kwa pigo la kichwa mchezo dhidi ya Pamba Jiji akitumia pasi ya Ellie Mpanzu. Magoli 6 alifunga kwa mikwaju ya penati.

Tayari msimu mpya wa 2025/26 umeanza huku vinara wakiwa ni Feisal Salum wa Azam na De Reuck wa Simba SC. Hakuna vigezo vingi kuwa mfungaji bora zaidi ni kufunga magoli mengi kuliko wengine. Kila mchezaji hesabu kubwa ni kuona timu inapata matokeo ndani ya uwanja. Mashabiki wanajiuliza kasi ya Ahoua itaongezeka ama atakwama kuvunja rekodi yake?

SOMA HII: Mfungaji bora wa muda wote John Bocco na Jonas Mkude kupewa tuzo Simba Day 2025

image

Wafungaji wengine waliofunga magoli mengi

Clement Mzize wa Yanga SC-14

Mzizeeeeeee⚽️
Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Clement Mzize alifunga jumla ya magoli 14. Mshambuliaji huyu kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate alichaguliwa kuwa mchezaji bora. Atakumbukwa kwenye Kariakoo Dabi mzunguko wa pili alikuwa kwenye ubora alipoingia dakika ya 45 akichukua nafasi ya Prince Dube. Alipachika goli dakika ya 87 akitumia pasi ya Pacome na kufikisha magoli 14 kwenye ligi.

Yanga SC ikiwa imefunga magoli 83, alifunga magoli 14 na kutoa pasi tano za mabao. Mechi tatu mfululizo alikuwa kwenye ubora dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji alitoa pasi za magoli kwa Clatous Chama na kwenye mchezo Kariakoo Dabi alifunga.

Prince Dube wa Yanga SC magoli -13

Nyota wa Yanga SC Prince Dube Juni 25 2025 alitumia dakika 45 kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi. Alifunga jumla ya magoli 13 na pasi 8 za magoli ambazo zinamfanya ahusike kwenye magoli 21 kati ya 83 ambayo yaliyofungwa na Yanga SC.

Ikumbukwe kwamba hakuwa fiti asilimia 100 alipoanza kikosi cha kwanza katika mchezo wa Kariakoo Dabi. Kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alipata maumivu. Alimaliza msimu akiwa amefunga magoli 13 ndani ya ligi ya NBC.

SOMA HII: Orodha ya mastaa kwenye vita ya ufungaji bora 2024/25

image

Steven Mukwala wa Simba SC magoli – 13

Steven Mukwala mshambuliaji wa Simba SC alifunga jumla ya magoli 13. Nyota huyo alianza kikosi cha kwanza mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC na kukutwa mara tatu kwenye mtego wa kuotea. Goli lake la 13 alifunga kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa KMC Complex.

Pacome Zouzoua wa Yanga SC magoli -12

Rekodi zinaibeba Yanga SC mbele ya Pamba Jiji FC
Pacome kiungo mshambuliaji wa Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Pacome kagotea kwenye mabao 12. Alipachika bao la 12 kwenye Kariakoo Dabi dakika ya 66 kwa mkwaju wa penati. Alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo huo.

Ni pasi 10 za mabao anazo ndani ya msimu wa 2024/24. Kwenye mchezo dhidi ya Simba SC alitoa pasi ya bao kwa Clement Mzize. Kahusika kwenye mabao 22 kati ya 83 yaliyofungwa na Yanga SC.

Jonathan Sowah wa Simba SC magoli 13

Huyu 2024/25 alikuwa katika kikosi cha Singida Black Stars alipofunga magoli 13. Msimu mpya 2025/26 ameanza changamoto mpya Simba SC, Je atafikia rekodi yake?

Hitimisho

Mfungaji bora 2024/25 tayari ameshajulikana baada ya msimu kufika mwisho. Ni mwanzo mwingine katika kumtafuta mchezaji ambaye atakuwa kinara wa ufungaji. Endelea kupata habari kutoka SportPesa ambapo kutakuwa na mwendelezo wa wafungaji na matokeo kila siku.

Bonyeza hapa chini na ujishindie mamilioni kwa kucheza SportPesa Supa Jackpot 17

image

Share this: