- Kocha mwenye CV kubwa aliangusha pointi mbele ya mzawa Malale Hamsini kwenye mchezo wa Ligi ya NBC.
- Romain Folz bado yupoyupo Yanga SC akiwa na majukumu kubadilisha mfumo wa uchezaji kwa mechi zijazo.
- Ratiba ya mechi zijazo za Yanga SC ni vigongo vizito, Kariakoo Dabi kufunga ukurasa 2025.
Romain Folz bado yupoyupo Yanga SC akiendelea kufundisha kikosi kwa mechi zijazo. Tetesi zinaeleza kutokana na timu kucheza katika kiwango kisichofurahisha tathimini inafanyika. Kocha huyo mwenye CV kubwa aliangusha pointi mchezo dhidi ya Mbeya City inayofundishwa na mzawa Malale Hamsini.
Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Muda wa kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Romain Folz bado yupoyupo Yanga SC kipi kinafuata?

Wahenga walisema kuwa lisemwalo lipo kama halipo laja. Romain Folz bado yupoyupo Yanga SC kipi ambacho kitamfanya asalie hapo? Limekuwa swali ambalo linagonga vichwa vya wengi. Taarifa zinaeleza kuwa kocha huyo amekaa kikao na uongozi wa Yanga SC na kuzungumza nao kuhusu mwendo wa timu.
Mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Mbeya City, waliangusha pointi mbili kwa suluhu ya 0-0. Baada ya mchezo huo Folz alibainisha kuwa mbinu zote za kusaka ushindi zilikwama.Licha ya ijtihada za wachezaji, uwanja haukuwa rafiki.
“Tulifanya kila jitihada kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mbeya City. Hakuna ambacho tulikuwa tunahitaji zaidi ya matokeo mazuri. Bahati mbaya eneo ambalo tulichezea halikuwa rafiki kwetu,” alisema Folz.
SOMA HII: Wiki ya Mwananchi Septemba 12 2025 tunapiga kichwani tu | Matukio muhimu, burudani, wachezaji wapya

Kazi imeanza kwa Folz Yanga SC

Mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City, wachezaji wa Yanga SC walipewa mapumziko mafupi. Wakati wengine wakiwa kwenye mapumziko wapo walioitwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Wachezaji ambao hawajaitwa katika majukumu ya taifa, Oktoba 6 2025 wameripoti kambini.
Tayari kazi imeanza kwa Kocha Mkuu, Romain Folz kuwafundisha wachezaji hao. Miongoni mwa wachezaji waliopo kambini ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr, Maxi Nzengeli, Dennis Nkane. Ikumbukwe kwamba ndani ya Septemba Yanga SC ilicheza mechi mbili, ilishinda mchezo mmoja na kuambulia sare mchezo mmoja.
Ratiba ya mechi za Yanga SC Oktoba
Yanga SC ina mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika. Ni dhidi ya Silver Strikers ya Malawi. Mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa Malawi Okotba 18 na ule wa marudiano utapigwa nyumbani kati ya tarehe 24-26. Mshindi wa jumla kwenye mechi hizi mbili atatinga hatua ya makundi.
Mchezo mmoja ni wa ligi ya NBC itakuwa dhidi ya Mtibwa Sugar. Ni Oktoba 29 2025 Uwanja wa Mkapa mchezo huo unatarajiwa kuchezwa. Mechi hizi tatu itakuwa ndani ya Oktoba 2025.
Mechi za Yanga SC Novemba 2025
Yanga SC vs KMC mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Novemba 4 2025. Kwenye ligi ndani ya Novemba Yanga SC inatarajiwa kucheza mchezo mmoja. Itawakaribisha watonza ushuru watoto wa Kinondoni.
Ratiba ya Yanga SC Desemba 2025 kuna Kariakoo Dabi

Coastal Union vs Yanga SC unatarajiwa kuchezwa Desemba 10 2025 na Yanga SC vs Simba SC unatarajiwa kuchezwa Desemba 13 2025. Kariakoo Dabi inatarajiwa kuwa funga kazi kwa NBC ndani ya 2025.
SOMA HII: Orodha ya wachezaji waliosajiliwa Yanga SC 2025/26 | Vita yao na Simba SC balaa zito

Matokeo ya mechi za Yanga SC chini ya Romain Folz
Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki)
Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii).
Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).
Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).
Hitimisho
Romain Folz bado yupoyupo Yanga SC akiendelea kuwapa mbinu wachezaji. Ikiwa hakutakuwa na mabadiliko kwenye eneo la uchezaji kuna asilimia ndogo kubaki Jangwani. Kocha ambaye anatajwa kurejea hap oni Sead Ramovic.


