- Septemba imekuwa na matokeo mazuri kwa timu zote mbili katika mechi ambazo walicheza Uwanja wa Mkapa.
- Kariakoo Dabi, Yanga SC vs Simba SC itafanyika Septemba 16 kwenye fainali ya Ngao ya Jamii.
- Katika mchuano wa mwisho Yanga SC waliibuka washindi kwa mabao 2-0 je Simba SC watasawazisha?
Yanga SC vs Simba SC hapa tunakuetea uchambuzi wa mechi hii kali ambayo itachezwa Uwanja wa Mkapa Septemba 16 2025. Miamba hawa wa Tanzania wamecheza mechi 21, Simba SC wakishinda mara 4, Yanga SC ikiibuka na ushindi mara 8 na sare 9 kwa mechi za hivi karibuni. Je nani ataibuka mshindi kwenye hii Kariakoo Derby inayokuja?
Mamilioni yanakusubiri ukipaisha Kindege cha SportPesa
Kuna mamilioni yakutosha ambayo yanakusubiri na ni uhakika. Rahisi kuyachukua ukipaisha Kindege cha SportPesa. Cheza sasa Aviator upate mgao wako!

Uchambuzi wa Yanga SC vs Simba SC Kariakoo Dabi matokeo 2017/24

Soma hii: Kariakoo Dabi mchezo wa watani wa jadi Yanga SC vs Simba mechi ipo Juni 15 2025
Katika mechi nne za fainali Ngao ya Jamii, Yanga SC ushindi mechi 2 na Simba SC ushindi mechi mbili. Ushindi kwa Simba SC mechi zote mbili ilikuwa ni kwa penati.
Matokeo ya mechi za fainali kwa Yanga SC vs Simba SC:- 2017- Simba SC 5-4 Yanga SC, mshindi alipatikana kwa penati baada ya kutofungana kwenye muda wa kawaida. 2021- Yanga SC 1-0 Simba SC. 2022- Yanga SC 2-1 Simba SC.
2023- Simba SC 3-1 Yanga SC, mshindi alipatikana kwa penati. Baada ya kutofungana. Wababe hawa wawili wanatarajiwa kukutana Septemba 16 Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.
Fainali kiujumla ilikuwa namna hii tangu 2017
2017- Simba SC 5-4 Yanga SC, mshindi alipatikana kwa penati. 2018- Simba SC 2-1 Mtibwa Sugar. 2019- Simba SC 4-2 Azam FC. 2020 -Simba SC 2-0 Namungo FC. 2021- Yanga SC 1-0 Simba SC. 2022- Yanga SC 2-1 Simba SC.
2023- Simba SC 3-1 Yanga SC, mshindi alipatikana kwa penati. 2024- Yanga SC 4-1 Azam FC. Katika fainali ya 2024 goli la Azam FC lilifungwa na kiungo mshambuliaji Feisal Salum ambaye aliwahi kucheza Yanga SC.
Matokeo ya hivi karibuni kati ya Simba SC na Yanga SC

Soma hii: Kariakoo Dabi kuna vita nyingine kwa wachezaji
Kariakoo Dabi joto lake limezungukwa na hali ya ushindi. Hii inatokana na dakika 90 za kimataifa kuwa zenye kicheko. Timu hizi mbili Yanga SC na Simba SC kabla ya kukutana zilitoka kucheza mechi za kimataifa zikapata ushindi.
Mechi hizo zilikuwa kilele cha matamasha yao makubwa. Ilikuwa Septemba 10 2025, Simba SC 2-0 Gor Mahia, Simba Day. Magoli ya Simba SC yalifungwa na Abdulrazack Hamza na Steven Mukwala.
Yanga SC 1-0 Bandari, Uwanja wa Mkapa, ilikuwa ni Septemba 12 2025, Yanga Day. Goli la Yanga SC lilifungwa na Celestin Ecua dakika ya pili ya mchezo. Goli la Ecua linaingia kwenye rekodi ya kufungwa mapema zaidi ndani ya Septemba kwa wababe hawa wawili.
Vikosi vya Yanga SC na Simba SC
Kuelekea Kariakoo Dabi Yanga SC na Simba SC huenda asilimia kubwa wakatumia vikosi vilivyopita kwenye mechi za kimataifa. Ukweli ni kwamba mabadiliko yatakuwepo lakini sio makubwa. Hapa tunakuletea vikosi vya timu zote mbili vilivyokuwa namna hii:-
Hiki hapa kikosi cha Yanga SC kinachotarajiwa kuanza dhidi ya Simba SC

Diarra kipa namba moja wa Yanga SC anavaa jezi 39. Israel Mwenda anavaa jezi namba 33. Farid Mussa anavaa jezi namba 17. Bakari Mwamnyeto 3. Assink ingizo jipya anavaa jezi 36. Aziz Andambwile anavaa jezi namba 2, Maxi Nzengeli kiungo mshambuliaji anavaa jezi namba 7.
Kouma huyu anavaa jezi namba 8, Prince Dube anavaa jezi namba 29, Shekhan anavaa jezi namba 20, Ecua anavaa 11 hawa wameanza kikosi cha kwanza.
Wachezaji wa akiba
Aboutwalib Mshery, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Ninju. Shomari Kibwana,Mohamed Hussein, Boka, Casemiro, Conte. Duke Abuya, Mudathir Yahya, Doumbia, Sure Boy, Dennis Nkane, Offen Chikola, Edmund John na Boyel.
Kikosi cha Simba SC kinachotarajiwa kucheza

Moussa Camara anayevaa jezi namba 26 alianza langoni, Ladack Chasambi anayevaa jezi namba 36 alipewa majukumu ya kuwa beki. Anthony Mligo ingizo jipya kutoka Namungo alikabidhiwa jezi namba 5.
De Reuck ambaye ni beki alikabidhiwa jezi namba 23 huyu ni beki ingizo jipya. Hamza jezi namba 14 alicheza namba 6. Kibu Dennis kiungo mshambuliaji jezi namba 38 alipewa kitambaa cha unahodha. Jonathan Sowah mshambuliaji mpya wa Simba SC alikabidhiwa jezi namba 3. Jean Ahoua kiungo mshambuliaji alipewa jezi namba 10. Neo ingizo jipya alikabidhiwa jezi namba 35.
Wachezaji wa akiba
Hussen Abel, Yakoub Suleman, Alexader, Masinde. David Kameta, Shomari Kapombe, Mbegu, Yusuph Kagoma. Kante, Morice Abraham, Salum, Joshua Mutale, Awesu Awesu, Steven Mukwala, Seleman Mwalimu.
Hitimisho
Kariakoo Dabi ya Ngao ya Jamii ni ufunguzi wa pazia la 2025/25. Mchezo huu huashiria mwanzo wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC. Taji la Ngao ya Jamii kwa sasa lipo mikononi mwa Yanga SC.


