- Joto linazidi kupanda kwa watani wa jadi kutoka mitaa ya Kariakoo zikiwa zimesalia siku tatu mchezo mkubwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
- Yanga SC vs Simba SC kuna wachezaji ambao itakuwa ni Kariakoo Dabi yao ya kwanza ndani ya uwanja.
- Simba SC hawana matokeo mazuri mbele ya Yanga SC kwenye mechi za ushindani.
Yanga SC vs Simba SC Septemba 16 2026 wanatarajiwa kukutana uwanjani zimebaki siku tatu. Huu ni mchezo wa Ngao ya Jamii. Timu zote mbili zimekamilisha matamasha yao makubwa ni Simba Day Septemba 10 2025, Yanga Day Septemba 12 2025.
Muda wa kuvuna mamilioni na Kindege cha SportPesa
Kwa marubani hii isikupite kwa kuwa ni rahisi kweli. Unachotakiwa kufanya ni kupaisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi. Cheza Aviator upate mgao wako.

Yanga SC vs Simba SC wachezaji ambao ni Kariakoo Dabi ya kwanza kwao
Yanga SC vs Simba SC baada ya kukamilisha matamasha yao makubwa wanakwenda kukutana uwanjani. Kuna wachezaji ambao walitambulishwa katika kilele cha Simba Day na Yanga Day waliokuwa wapya hawakuwahi kucheza Kariakoo Dabi. Makala hii inakuletea orodha ya wachezaji kutoka timu hizi mbili namna hii:
Andy Boyeli

Soma hii: Yanga SC imetambulisha wachezaji wapya 11
Alikuwa anacheza Klabu ya Sekhukhune United ya Afrika Kusini yupo kwa mkopo wa mwaka mmoja. Julai 31 alitambulishwa kuwa Mwanajangwani. Kariakoo Dabi hii Yanga SC vs Simba SC inakwenda kuwa ya kwanza kwake.
Lassine Kouma
Lassine Kouma yeye ni kiungo mkabaji. Ametambulishwa Yanga SC iliyonasa saini yake akitokea Stade Malien. Anavaa jezi namba 8 iliyokuwa ikimtambulisha Khalid Aucho 2024/25.
Balla Conte
Huyu ni nyota aliyekuwa akicheza CS Sfaxien ya Tunisia ni raia wa Guinea. Nyota huyu alisaini mkataba wa miaka mitatu. Septemba 16 2025 itakuwa ni Kariakoo Dabi yake ya kwanza.
Ecua Elastin

Amefungua akaunti ya magoli, alifunga katika mchezo wa Wiki ya Mwananchi. Septemba 12 2025 mbele ya Bandari. Agosti Mosi 2025 alitambulishwa Yanga SC kwa dili la miaka miwili. Yeye ni mshambuliaji ni Kariakoo Dabi yake ya kwanza itakuwa.
Doumbia
Mohamed Doumbia ni kiungo mpya Yanga SC. Ana umri wa miaka 26 amejiunga na Yanga SC kutokea FC Slovan Liberec ya Jamuhuri ya Czech. Katika Yanga Day alianzia benchi.
Edmund John
Agosti 15 2025 Yanga SC ilimtambulisha winga Edmund John kutoka Singida Black Stars. Nyota huyo alitambulishwa kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Rayon Sports 1-3 Yanga SC. Kwenye mchezo huo Edmund aliazia benchi.
Assinki
Agosti 21 2025 Yanga SC ilimtambulisha nyota mpya kuelekea msimu wa 2025/26 ambaye ni beki wa kati. Anaitwa Frank Assinki ni raia wa Ghana na msimu wa 2024/25 alikuwa ndani ya kikosi cha Singida Black Stars. Septemba 12 2025 alianza kikosi cha kwanza dhidi ya Bandari.
Wachezaji wengine ambao itakuwa ni Kariakoo Dabi yao ya Kwanza ndani ya Yanga SC ni Offen Chikola kiungo mshambuliaji. Abubakar Nizar Othuman, maarufu kwa jina la Ninju kutoka Azam FC alitambulishwa rasmi Julai 27 2025. Casemiro.
Yanga SC vs Simba SC wachezaji wa Simba SC ambao itakuwa Kariakoo Dabi ya kwanza
Mwalimu

Soma hii: Seleman Mwalimu ametambulishwa Simba SC Agosti 28 2025
Selemani Mwalimu alitambulishwa Simba SC, Agosti 28 kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja. Alikuwa Wydad Casablanca ya Morocco. Yeye ni mshambuliaji.
Kante
Nyota Alassane Kante ni kiungo alikuwa anacheza CA Bizertin ya Tunisia. Yupo ndani ya Simba SC msimu wa 2025/26. Alitambulishwa Julai 30 2025.
Morice
Morice Abraham alitambulishwa ndani ya Simba SC Julai 31 2025. Alianzia benchi kwenye mchezo dhidi ya Gor Mahia. Septemba 16 2025 itakuwa ni Kariakoo Dabi yake ya kwanza.
Semfuko
Hussein Daudi Semfuko alitambulishwa Simba SC, Julai 31 2025 kuwa ni mali ya Simba SC. 2024/25 alikuwa akicheza Coastal Union ya Tanga. Septemba 16 2025 itakuwa ni Kariakoo Dabi yake ya kwanza.
Bajaber
Agosti 2 2025 Simba SC ilimtambulisha Mohamed Bajaber. Kiungo mshambuliaji alikuwa anacheza Polisi ya Kenya. Huyu hakuwepo katika kikosi kilichocheza na Gor Mahia ya Kenya.
Nangu
Huyu ni beki ambaye mchezo wa Septemba 16 2025 itakuwa ni Karikoo Dabi yake ya kwanza. Msimu wa 2024/25 alikuwa ndani ya JKT Tanzania. 2025/26 yupo kikosi cha Simba SC kwa changamoto mpya.
Mligo
Anthon Mligo ni beki wa kushoto. Amesaini Simba SC akitokea kikosi cha Namungo FC 2024/25. Itakuwa ni Kariakoo Dabi ya kwanza Septemba 16 2025 kwake.
Wachezaji wengine wa Simba SC ambao itakuwa ni Kariakoo Dabi yao ya kwanza ni Yakoub Suleiman huyu ni kipa. Wawili hawa msimu wa 2024/25 walikuwa JKT Tanzania. Vedastus Masinde yeye ni beki alikuwa TMA Stars inayoshiriki Championship, Naby Camara.
H2H
Wababe hawa msimu wa 2024/25 walikutana mara tatu kwenye mashindano tofauti. Mara mbili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC na mara moja Ngao ya Jamii. Mechi zote tatu Yanga SC ilipata ushindi.

Ilikuwa katika nusu fainali Ngao ya Jamii. Ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 1-0 Simba SC Agosti 8 2024. Bao la ushindi lilifungwa na Maxi Nzengeli.
Katika Ligi Kuu Bara 2024/25 mechi zote mbili, nje ndani Simba SC ilipoteza Kariakoo Dabi. Dakika 180 pointi sita zilikuwa mali ya Yanga SC. Simba SC 0-1 Yanga SC mchezo ulichezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 19 2025, goli lakujifunga Kelvin Kijili dakika ya 88.
Mzunguko wa pili ilikuwa Yanga SC 2-0 Simba SC Juni 25 2025, Uwanja wa Mkapa. Magoli ya Pacome Zouzoua ambaye alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo na Clement Mzize.
Hitimisho
Yanga SC vs Simba SC ni mchezo unaosubiriwa kwa shauku kubwa. Timu zote mbili zimekamilisha usajili zinakwenda kukutana kwa mara ya kwanza. Hii inamaanisha pazia la ligi linakwenda kufunguliwa rasmi.


