Yanga SC vs Bandari FC Septemba 12Zuchu
  • Kutoka viunga vya Super Dome, Masaki Dar es Salaam, stori yamoto ni kuhusu Yanga.
  • Hii ni baada ya kufanyika mkutano mkuu wa Yanga SC 2025.
  • Mkutano huu ulibeba mambo mbalimbali ya kushtua ikiwemo ‘Surprise’ ya msanii Zuchu.
  • Makala hii inachambua mambo 10 yaliyotikisa kwenye mkutano huo.

Stori kubwa kwenye anga za michezo leo Septemba 7, 2025 ni kuhusu Mkutano mkuu wa Yanga SC 2025. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa kisasa wa Super Dome, uliopo Masaki, Dar es Salaam. Mkutano huu ni takwa muhimu la kikatiba na kikanuni, ambao kwa kawaida hufanyika kila mwaka. Makala hii inakuletea mambo 10 yaliyotikisa kwenye mkutano huo.

SOMA HII PIA: Yanga SC wiki ya wananchi ni Ijumaa Septemba 12

Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Bado hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

SEO Banner LV

Kuhusu Mkutano Mkuu wa Yanga SC 2025 na Agenda zake

Makombe
Makombe

Mkutano mkuu wa Yanga SC 2025, ni takwa muhimu la kikatiba na kikanuni. Mkutano huu kwa kawaida hufanyika kila mwaka, kama jukwaa rasmi la kutoa taarifa muhimu za uendeshaji wa klabu hiyo. Baadhi ya vipaumbele na Agenda muhimu za mkutano huo ni Pamoja na ufuatiliaji wa mafanikio, na kuweka msingi imara wa kiuchumi kwa msimu ujao. Yafuatayo ni mambo 10 yaliyotikisa kwenye Agenda za leo.

SOMA HII ZAIDI: Usajili wa Yanga SC orodha ya wapya 11 msimu wa 2025/26 | Rekodi, magoli na timu walizotoka

Utambulisho wa kocha Msauzi

Kama ambavyo imekuwa utaratibu wa miaka ya karibuni, uongozi wa Yanga SC umekuwa ukileta baadhi ya watu muhimu kama wageni katika mkutano huo. Mwaka huu pia maofisa wetu wa benchi la Ufundi wakiongozwa na Kocha Mkuu, Romain Folz walitambulishwa rasmi. Utambulisho huo ulifanyika mbele ya wanachama wa Yanga SC.

Ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa

Hii imebaki kuwa ahadi pekee ambayo uongozi wa Rais Hersi haujautimiza mpaka sasa. Kiongozi huyo mkuu wa Yanga SC ametoa taarifa juu ya maendeleo ya mchakato wa mradi wa kujenga uwanja wa kisasa Jangwani. Yanga SC kupitia kwa makamu mwenyekiti wao, Arafat Haji wameweka wazi kuwa kwa kuanza wameandaa Bilioni 1 kwa ajili za hatua za awali za ujenzi. Ikumbukwe mradi huo wa ujenzi wa Uwanja wa Yanga SC unafanywa kwa mashirikiano na Serikali, ambayo ina mradi mkubwa wa mto Msimbazi.

Bajeti ya Bilioni 33.4 msimu wa 2025/26

Makamu Rais- Arafat
Makamu Rais- Arafat

Hii ni miongoni mwa hoja iliyoshtua, kutoka kwenye Ajenda ya taarifa ya fedha ya Yanga SC. Ikumbukwe bajeti ya Yanga kwa nmsimu uliopita wa 2024/25 ilikuwa Bilion 25, ambapo baada ya matumizi walibakiwa na bakaa ya milion takribani 300m. Kuelekea msimu wa 2025/26, Yanga SC imepanga bajeti ya Tsh Bilioni 33.4 hii ikiwa ni ongezeko la kiasi cha shilingi Bilioni 8. Kama ilivyo kawaida Ripoti ya fedha ilitolewa na makamu Rais, Arafat Haji.

Usajili wa Bilioni 7 msimu mpya wa 2025/26

Kupitia taarifa hiyo ya kifedha, ambayo ilisomwa na kuidhinishwa na viongozi wa Wanachama wa Yanga. Uongozi wat imu hiyo umeweka wazi kuwa, wanatarajia kutumia kiasi cha Shilingi Bilioni 7 kwenye usajili ndani ya msimu huu mpya. Ikumbukwe tayari fedha hiyo imeanza kutumika kusajili mastaa wapya, na kuongeza mikataba wale waliokuwepo.

Mahitaji na miradi ya baadaye

Mkutano mkuu wa Yanga SC 2025
MC wa Mkutano Mkuu- Ali Kamwe

Ukiachana na mradi wa ujenzi wa uwanja, uongozi wa Yanga SC umetangaza mipango yao mizito ya baadae. Kati ya miradi hiyo ni suala la kukuza soka la vijana na Wanawake. Kwa sasa uongozi unatazama hilo kama fursa ya kibiashara kuuza wachezaji nje ya nchi. Pamoja na hayo uongozi wat imu hiyo pia umeweka wazi mipango ya kuimarisha timu hiyo kiuchumi, hususani mkakati wa kuongeza mapato kupitia usajili wa wanachama na wateja wapya, pamoja na wadhamini wapya.

Thamani ya Yanga SC kuwa Bilioni 100

Kufuatia mchakato wa mabadiliko wa timu hiyo kuwa na mfumo wa kisasa. Uongozi wa Yanga SC kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya mabadiliko, Wakili Alex Mgongolwa ameweka wazi kuwa Thamani ya Klabu ya Yanga SC ni Tsh Bilioni 100. Klabu ya Yanga sasa inaweza kuendelea na mchakato wa mabadiliko kwa kuzingatia matakwa ya Katiba na Sheria za Soko la Hisa.

Zuchu kuuwasha moto kwa Mkapa siku ya Wananchi

Zuchu
Zuchu

Kuelekea tukio la kilele cha siku ya Wananchi, Yanga SC wamemtangaza msanii Zuchu kuwa mtumbuizaji wao mkuu. Zuchu pia alitambulishwa ukumbini hapo. Zuchu kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii alithibitisha hilo na kuandika: “Wananchiiiiiiiii. Tukutane katika Sikukuu ya Taifa 12 Septemba 2025. Mkapa Stadium, I will be your HEADLINER.”

Rekodi ya kucheza misimu 4 bila kufungwa Shirikisho

Miongoni mwa rekodi kubwa ambayo Yanga SC wanaishikilia na wameikumbushia leo, ni kucheza misimu minne bila kupoteza kwenye kombe la FA. Rais wa Yanga SC, Hersi Said amesema: “Ni heshima kubwa na ya kipekee na pengine inaweza kuwa rekodi bora kwa sasa AFRIKA. Niwapongeze sana wachezaji na benchi la ufundi.”

Ushiriki wa matawi kutoka nje ya Tanzania

Wawakilishi kutoka kanda tofauti tofauti
Wawakilishi kutoka kanda tofauti tofauti

Mbali na uwepo wa wawakilishi wa wanachama kutoka maeneo mbalimbali Tanzania. Jambo la kuvutia ni ushiriki wa baadhi ya matawi kutoka nje ya nchi kama vile matawi yaliyopo nje ya nchi kama vile, China, Afrika Kusini, DR Congo, Uganda na Kenya, na wanachama wetu kwa njia ya mtandao.

Alichosema Rais, Hersi Said

    “Msimu uliopita Makamu wetu alitoa ahadi ya kuhakikisha timu yetu ya wanawake inabeba ubingwa. Tulianza na SAMIA cup sasa tunataka ubingwa ligi kuu. Niwaambie jambo muhimu, ile kauli haikuwa kauli ya Arafat Haji pekee yake bali ni kauli yetu sote. Hata mimi niliwahi kutoa kauli kama hii watu wakanibeza. Niwaombe wananchi tuwe na subira tunaenda kufanya makubwa na timu ya wanawake” Hersi Ally Said

    Hitimisho

    Mkutano leo unadhihirisha kujitoa kwa Yanga katika kuwa klabu thabiti na endelevu. Pia hii ilielezea utashi wa kuhakikisha wanachama wanashirikishwa, usawa wa kifedha unatiwa mkazo. Kuwa mstari wa mbele kwa miundo bora na ubunifu katika soka la Tanzania.

    SOMA HII ZAIDI: Yanga SC yamsajili Frank Assinki kutoka Ghana kwa mkopo | Usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26

    Share this:

    By Joel Thomas

    Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.