MbossoMbosso
  • Ikiwa ni msimu wa 17 tangu kuanzishwa kwake, Tamasha kubwa la Simba Day 2025 linatarajiwa kufunika kwa upekee.
  • Uzinduzi wa jezi nao watikisa mkoani Iringa, rasmi uzi kutangazwa Jumapili hii Agosti 31, 2025.
  • Simba Day 2025 ni Simba SC vs Gor Mahia FC, moto utawaka kwa Mkapa.

Mambo yameiva ndani ya Simba SC, huku wakijiandaa kwa tukio kubwa la uzinduzi wa jezi zao mpya Jumapili hii. Uongozi wa Simba SC nao umeweka wazi rasmi klabu ya Gor Mahia kutoka Kenya ndio wamealikwa kwenye kilele cha Simba Day 2025. Tamasha mwaka huu litafanyika Uwanja wa Mkapa, huku msanii Mbosso akipewa jukumu kubwa la kutumbuiza.

SOMA HII PIA: Simba Day Septemba 10 2025 | Ali Kiba kutumbuiza | Ubaya Ubwela pasua kichwa

Cheza na ushinde mamilioni leo kwa kupaisha Kindege cha SportPesa (bonyeza picha hii chini)

image

Alichosema semaji Ahmed kuhusu tamasha la Simba Day 2025 ni Simba SC vs Gor Mahia FC

Simba Day 2025 ni Simba SC vs Gor Mahia FC
Ahmed Ally uzinduzi wa hamasa Iringa

Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo, Meneja Habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema: “Tulitangaza kwamba Septemba 10, 2025 itakuwa Simba Day. Ni wazi mara nyingi Simba Day inafanyika wiki ya kwanza ya mwezi wa nane. Lakini kutokana na kubanana kwa ratiba na hasa mashindano ya CHAN imefanya imesogea hadi mwezi wa tisa.

 “Hata mwezi Septemba pia haikuwa rahisi kupata tarehe sababu ya ratiba. Tukiwa tunaingia msimu huu wa 17 tumeanzisha utamaduni wa kufanya uzinduzi wa Wiki ya Simba nje ya Dar es Salaam. Mwaka jana ilikuwa Morogoro na mwaka huu tumezindua mkoani Iringa.

Kuhusu uzinduzi wa jezi mpya Jumapili hii

Utatu wa ushambuliaji Simba SC
Utatu wa ushambuliaji Simba SC

Kuhusu tukio kubwa la uzinduzi wa jezi za Simba SC kwa msimu huu wa 2025/26 Jumapili hii, Ahmed amesema: “Ndugu zangu tuna tukio kubwa sana, tukio la uzinduzi wa jezi. Tanzania itang’aa sana kwa jezi mpya ya Simba. Niwambie Wanasimba wa ukanda huu wenye baridi, ukivaa jezi mpya ya Simba usivae koti, iache wazi na utambe. Jezi inayozinduliwa kesho ukivaa husikii baridi hata kidogo, inakuchemsha, unasikia raha.”

SOMA HII ZAIDI: Mfungaji bora wa muda wote John Bocco na Jonas Mkude kupewa tuzo Simba Day 2025

Usajili wa Maema, mastaa wapya Simba SC wampagawisha Semaji

Kuhusu mastaa wapya waliosajiliwa Simba, Ahmed amesema: “Heshima ya Simba Sports Club inakwenda kurudi msimu wa 2025/26, tumechoka kushikwa sharubu na watoto wadogo, Mnyama anarudi kwenye ufalme wake. kwa usajili tulioufanya niwahakikishe Wanasimba msimu huu ni Ubaya Ubwela Part Two. Hii Simba tunayozungumzia hapa imesajili mchezaji kutoka Mamelodi Sundown, tumesajili mchezaji kutoka Wydad, tumesajili mchezaji kutoka Tunisia.

“Wachezaji ambao tumesajili msimu huu kwanza wana uwezo mkubwa sana na wana uzoefu. Ni wachezaji ambao tunaamini kwa njaa yao ya mafanikio itakwenda kutuvusha msimu huu. Timu yetu imekamilika. Mkiangalia golini kuna Moussa Camara na tumemuongezea kijana mwingine bora bado hatujamtambulisha. Upande wa kulia upo sawasawa na upande wa kushoto tumeleta watu bora zaidi, hawezi kupita binadamu wa kawaida.

“Mabeki wa kati ya uwanja hapo kuna hatari kwanza Chamou amebaki, Hamza bado yupo kufanya kazi zake za kistaarabu lakini tumemsajili mtu anaitwa The Rock. Acha nisimalize utamu, tukutane Simba Day.

“Katikati yupo Kagoma lakini tumemuongezea mtu anaitwa Kunta Kinte. Ila eneo la mbele ndio kuna balaa zaidi. Kuanzia kwa Ahoua, Neo Maema, Mpanzu, sijamtaja Sowah, mfalme Gomez, itoshe kusema mwaka huu timu tunayo. Majonzi tuliyopitia kwa miaka minne huu ndio mwisho wake.”

SOMA HII PIA: Kikosi cha Simba SC kurejea Tanzania leo Agosti 28, 2025 usiku

Mbosso kuiteka shoo ya wasanii kwa Mkapa

Mbosso
Mbosso

“Kwenye burudani, leo nipo hapa kumtangaza msanii mkubwa ambaye ataimba kwenye tamasha letu la Simba Day. Mwaka huu tumeleta msanii ambaye hajawahi kuimba Simba Day na kwa sasa ndio msanii anayefanya vizuri zaidi Afrika Mashariki, na pia ni Mwanasimba mwenzetu. Namtangaza msanii wa Simba Day 2025 ni Mbosso. Utamu wa Aviola, Powa, Selemani tutaimba wote na Mbosso. Usikose,” Ahmed Ally.

Hitimisho: Mgeni rasmi naye achimba mkwara

Mgeni rasmi uzinduzi
Mgeni rasmi uzinduzi

Naye Mjumbe wa Bodi na Mgeni rasmi wa uzinduzi wa Simba Week 2025 tukio la kuielekea Simba Day 2025 ni Simba SC vs Gor Mahia FC, Selemani Haroub amesema: “Uzinduzi mkubwa kama huu ni ishara kubwa kuelekea msimu mkubwa na usajili wenyewe si mmeona. Siku ya kuona zaidi ni Simba Day, wote tuliopo hapa tuhakikishe tunafika uwanja wa Mkapa. Kuna vitu hamjawahi kuona vikitokea mwaka huu mtaona.”

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.