- Morocco yatwaa ubingwa mbele ya wapinzani wao Madagascar katika mchezo wa fainali uliochezwa Kenya, Uwanja wa Moi.
- Madagascar walianza kufungua ukurasa wa mabao mapema kipindi cha kwanza dakika ya 9.
- Mabao matano yamefungwa katika mchezo wa fainali huku mfungaji bora akipatikana katika mchezo wa leo ambaye ni Oussama Lamlioui mwenye mabao 6.
CHAN 2024 Morocco yaifunga 3-2 Madagascar fainali Agosti 30 2025. Safari ndefu ya kumsaka bingwa mpya imefika tamati huku Morocco akiwa ni bingwa mpya anafikisha jumla ya mataji matatu ya CHAN. Kwenye mchezo wa leo Uwanja wa Moi yamefungwa mabao matano ndani ya dakika 90.
Shinda mkwanja ukipaisha Kindege cha SportPesa
Nafasi ni yako sasa kushinda mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa. Rahisi mno kwako rubani, cheza Aviator sasa hivi uvune mahela. Mgao upo kila siku unakusubiri.

Soma hii: SportPesa Goal Rush washindi Agosti 24-30, 2025 hawa hapa
CHAN 2024 Morocco yaifunga 3-2 Madagascar fainali, Nairobi, Kenya.

Soma hii: CHAN 2024: Tanzania 0-1 Morocco
Katika mashindano ya Pamoja CHAN 2024 Morocco yaifunga 3-2 Madagascar fainali na kutwaa taji la ubingwa. Ikumbukwe kwamba timu ya taifa ya Morocco kwenye hatua ya makundi ilikuwa kundi A ikimaliza nafasi ya pili na pointi 9. Vinara walikuwa ni Kenya walikusanya pointi 10.
Kwenye mchezo wa leo, Morocco walianza kufungwa bao la mapema na wapinzani wao Madagascar. Mabao ya Madagascar mawili yamefungwa na Felly dakika ya 9 na bao la pili limefungwa na Toky Rakotondraibe dakika ya 69.
Iliwachukua dakika 18 Morocco kupata bao la kuweka usawa kwenye mchezo huo. Ni Youssef Mehri alipachika bao dakika ya 27. Nyota Oussama Lamlioui dakika moja kabla ya kwenda mapumziko alifunga bao la pili ilikuwa ni dakika ya 44. Ni yeye alifunga bao la ushindi dakika ya 80.
Nyota Oussama wa Morocco yeye ana tuzo ya ufungaji bora wa Pamoja CHAN 2024. Amefunga jumla ya mabao 6. Kwa upande wa Mohamed Hrimant wa Morocco yeye ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mashindano.
Taji la tatu kwa timu ya taifa ya Morocco

Soma hii: CHAN 2024: Kenya 1-0 Morocco
Timu ya taifa ya Morocco hili linakuwa ni taji lake la tatu la African Nations Championship, (CHAN). Yote hii ni baada ya ushindi katika mchezo wa fainali dhidi ya Madagascar. Ikumbukwe kwamba Madagascar kwenye hatua ya makundi ilikuwa kundi B.
Ushindi wa Agosti 30 2025 katika fainali unaifanya Morocco kutwaa jumla ya mataji matatu ya CHAN. Ilianza 2018, 2020. Hili la Pamoja CHAN 2024 linakuwa ni taji la tatu kwao.
Nafasi ya tatu ni Senegal iliyopata ushindi wa penati 4-2 dhidi ya Sudan. Wababe hawa wawili kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa tatu baada walifungana bao 1-1. Mchezo huo ulichezwa Agosti 29 2025.
Vikosi vilivyoanza kwenye fainali CHAN 2024
Kikosi cha Morocco

Soma hii: Tanzania vs Morocco robo fainali dume Uwanja wa Mkapa
Mehd Harrar mwenye miaka 24 ambaye anacheza Klabu ya Raja Casablanca huyu ni mlinda mlango. Youssef Belammari, Marwane Louadni mwenye miaka 30, Anas Bach mwenye miaka 30, Ayoub Khairi miaka 25, Mehri, M.Boulascout, Mohamed Rabie Hrimant ambaye ni nahodha. K. Baba, O. Lamlioui na S. Bougrine anayecheza Raja Casablanca.
Wachezaji wa akiba ni M. Mchakhchech, B. Arrasi, M. Moufid aliingia dakika ya 86 na alionyeshwa kadi ya njano, S. Errahouli, A. Souane, K.Ait Ouarkhane, Y. Ek Kaabi, H. Essadak, I. Riahi, Anas, S. Bouhra.
Kikosi cha Madagascar
Kwa upande wa Madagascar kikosi cha kwanza ilikuwa ni Michael Ramandimbisoa mwenye miaka 39 huyu ni mlinda mlango. Nantenaina Randriamanampisoa, Hajatiana Claude Ratsimbazafy, T. Randrianirina, B. Rabearivelo, J. Ranaivoson, H. Randrianantenaina, T. Randrianirina. Harrison Patrick, Nomena Lalaina, na Felicite Mantasoa.
Wachezaji wa akiba ni B. Randrianaivo, Manda Ratsimbazafy, P. Tolojanahary, P. Randrianjatovo, F. Rakotonandrasana, T. Ramahandrison, O. Ramamonjisoa, M.Rakotoson, R. Rajaonarivelo, A. Andrianarimana na T. Rakotondraibe.
Pamoja CHAN 2024 ilikuwa na kasi
Pamoja CHAN 2024 ilikuwa yenye kasi kwelikweli kutokana na kila timu kusaka matokeo chanya. Wenyeji walikuwa ni Kenya, Uganda na Tanzania. Hawa wote waliishia katika hatua ya robo fainali.
Kenya ilipata ushindi kwenye hatua ya makundi dhidi ya mabingwa Morocco. Tanzania ilipoteza mbele ya mabingwa Morocco kwa kufungwa bao 1-0 katika hatua ya robo fainali.
H2H
Januari 19 2023 walikutana kwenye mchezo wa CHAN ilikuwa Morocco 0-3 Madagascar. Agosti 30 2025 wamekutana kwenye fainali ya Pamoja CHAN 2024. Ubao wa Uwanja wa Moi umesoma Madagascar 2-3 Morocco. Baada ya Morocco kuifunga 3-2 Madagascar imetwaa taji hilo kubwa Afrika.
Hitimisho
Morocco hawakuanza na kasi yakutisha kwenye mashindano ya CHAN 2024 mpaka kutwaa taji hilo kwa kuifunga Madagascar 3-2. Mwendo wao wakinyonga umewapa taji la tatu la CHAN. Historia imeandikwa wanakuwa mabingwa mara tatu wa mashindano haya makubwa Afrika ambayo yanawahusisha wachezaji wa ndani.


