- Clement Mzize ataingia kwenye orodha ya wachezaji wazawa wanaolipwa mshahara mrefu ndani ya Ligi Kuu Bara ya NBC ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.
- Waarabu wa Tunisia walikuwa wanahitaji huduma ya mshambuliaji huyo ambaye mguu wake wenye nguvu uwanjani ni ule wa kulia.
- Yanga SC imeonesha ukubwa wake Afrika kwa kutunishiana misuli na timu kubwa hivyo Clement Mzize haendi popote atabaki Jangwani.
Clement Mzize haendi popote kwa changamoto mpya atabaki katika kikosi cha Yanga SC. Inatajwa atalipwa mshahara mkubwa wa milioni 40 pesa ya Tanzania ili asiondoke. Tetesi zilikuwa zinaeleza kuwa Esperance ya Tunisia na Kaizer Chiefs zinahitaji saini yake. Kwa sasa uwezekano ni mkubwa mshambuliaji huyu atabakia Yanga SC.
Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni
Ukiwa hewani rubani hakuna unyonge kwa kuwa kuna faida kubwa. Ukipaisha Kindege ushindi njenje. Unachotakuwa kufanya ni kucheza Aviator upate mgao wako sasa hivi.

Sababu za Mzize kutoenda popote

Soma hii: Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga SC anaondoka
Kutokana na ofa kuwa nyingi na mabosi wa Yanga SC wakitajwa kuhitaji huduma mshahara umeongezwa. Inaelezwa kuwa Mzize kuna nafasi kubwa kusalia Jangwani na atavuta mshahara mrefu. Hiyo ni mbali na posho kila mchezo ambao atakuwa akicheza.
Ikiwa mpango huo utatimia anatajwa kuingia kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa pesa nyingi kwenye ligi kuu ya Tanzania. Kwa sasa inaelezwa kuwa mchezaji anayeoongoza kwa kulipwa pesa nyingi ni Feisal Salum wa Azam FC akiwa na mshahara wa shilingi milioni 50.
Takwimu muhimu za Mzize 2024/25

Soma hii: Baada ya Aziz Ki: Mzize na Aucho wanaondoka Yanga? Tetesi usajili bongo
Mzize kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2024/25 alicheza mechi 30. Alitwaa ubingwa na kikosi cha Yanga SC ambacho kilikusanya pointi 82. Jina lake lipo kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania iliyoishia robo fainali CHAN 2024.
Rekodi zinaonyesha kuwa alitumia dakika 1,877 kwenye mechi za ligi. Alifunga jumla ya magoli 14 kati ya 83 yaliyofungwa na Yanga SC. Ni mzawa namba moja kufunga mabao mengi ndani ya ligi.
Katika CHAN 2024 alifunga magoli mawili akicheza dhidi ya Madagascar. Ilikuwa kwenye mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Madagascar. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa na Taifa Stars iliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-1.
Mzize na Simba SC
Mzize amekuwa na rekodi yake kwenye mechi ambazo wanakutana na Simba SC. Kwenye Kariakoo Dabi amekuwa katika ubora wake huku kwenye mzunguko wa pili akiweza kufunga walipokutana. Mchezo huo Mzize alianzia benchi. Alipoingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Prince Dube alifunga. Ilikuwa ni goli la pili na Yanga SC ilishinda kwa mabao 2-0.
Watani hawa wanatarajiwa kukutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii mnamo Septemba 16 2025. Mchezo huu utafanyika Uwanja wa Benjamini Mkapa na huenda Mzize akachezea Yanga SC.
Ali Kamwe kuhusu Clement Mzize
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC ameweka wazi kuwa mchezaji huyo bado ana mkataba. Kamwe aliongeza kuwa mkataba wake ni miaka miwili na iwapo ataweza kuhamia timu nyingine ni lazima maafikiano yatimie.
“Tumepokea ofa nyingi ambazo zinamuhusu Clement Mzize. Wakati Mzize anaboresha mkataba wake aliambiwa anapaswa kupambana ndani ya msimu mpya. Hilo amelifanya na kazi yake imeonekana.
“Kuna taratibu linapofikia suala la mchezaji kwenda kwenye timu nyingine. Ofa za mchezaji zikifika mezani inakuwa mazungumzo ya mchezaji na klabu. Tunamwabia kuna ofa kadhaa zimekuja mchezaji anaamua wapi ambapo atakwenda kucheza.
“Ninachoweza kuwaambia mashabiki wa Yanga SC ni kwamba mchezaji wetu ana mkataba wa miaka miwili. Ambacho kitaamua aondoke ama abaki ni suala la mkataba. Kila kitu kipo sawa na utaratibu ukikamilika tutatoa taarifa,” alisema Kamwe.
Timu ambazo zilikuwa zinatajwa kuwania saini ya Mzize

Soma hii: Tanzania 2-1 Madagascar Mzize afunga magoli mawili
Klabu ya Esperance ya Tunisia ilikuwa inatajwa kuwania saini yake. Ilikuwa inaelezwa kuwa timu hii ilikuwa tayari kulipa dau nono kupata saini yake. Mpaka sasa hakuna taarifa zozote kuhusu kukamilika kwa usajili wa Mzize.
Mbali na timu hiyo kutoka Tunisia, kuna ofa kutoka Afrika Kusini. Kaizer Chiefs ilikuwa inatajwa kuiwinda saini ya mzawa huyo. Zamalek ya Misri ilikuwa inatajwa kuwa miongoni mwa timu ambazo zinahitaji saini yake.
Hitimisho
Clement Mzize haendi popote ila atabakia kuwa mchezaji wa Yanga SC. Baada ya tetesi nyingi kuibukia mshambuliaji huyu ameongeza mkataba wa mwaka mmoja na Wanajangwani. Mzize ni tegemeo sio kwa Yanga SC peke yake ila katika timu ya taifa ya Tanzania pia.


