Kagoma StarsKagoma Stars
  • CHAN 2024 imefika hatua nzuri kwa sasa ikiwa ni robo fainali, moja ya mchezo dume utawakutanisha Tanzania vs Morocco, Uwanja wa Mkapa.
  • Wachezaji muhimu wa Morocco huenda wakaikosa Tanzania kwenye mchezo kutokana na kutokuwa fiti na adhabu ya kadi za njano.
  • Hemed Suleiman, Kocha Mkuu wa Tanzania na Tarik Kocha Mkuu wa Morocco wametambiana kuhusu mchezo huo muhimu.

Tanzania vs Morocco Agosti 22 2025 mchezo dume kwa wababe wawili kusaka tiketi kutinga nusu fainali. Robo fainali ya CHAN 2024 inatarajiwa kuzikutanisha timu hizi mbili Uwanja wa Mkapa, saa 2:00 usiku. Makocha wa timu zote mbili wametamba kuja na mbinu tofauti.

Wikiendi ni kwa marubani kuna mamilioni

Marubani makini wakiwa hewani na Kindege cha SportPesa hawatui kinyonge. Kuna mamilioni yakushindasasa hivi ukicheza Aviator. Unachotakiwa kufanya ni kucheza upate mgao wako.

SEO Banner LV

H2H Tanzania vs Morocco

Feisal kwenye majukumu Stars
Feisal Salum, kiungo wa Tanzania.

Soma hii: CHAN 2024: Central African 0-0 Tanzania, Uwanja wa Mkapa

Rekodi zinaonyesha kuwa katika mechi tano zilizopita walipokutana Tanzania vs Morocco, ushindi kwa Tanzania ilikuwa ni mechi moja. Morocco ilipata ushindi katika mechi nne. Katika dakika 450, Morocco ilipata ushindi dakika 360 inapewa nafasi kupata upinzani mkubwa kutoka Tanzania.
Morocco 2-0 Tanzania, mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia, Machi 26 2025, Morocco 3-0 Tanzania, Januari 17 2024, mchezo wa Afcon.

Tanzania 0-2 Morocco, Novemba 21 2023, mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia. Morocco 2-1 Tanzania, Juni 8 2013, mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia. Tanzania 3-1 Morocco, Machi 24 2013, mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Huyu hapa Kocha wa Tanzania, Hemed Suleiman

Hemed Morocco
Hemed Kocha Mkuu wa Tanzania.

Soma hii: Tanzania 2-1 Madagascar Mzize afunga magoli mawili

“Tuna mchezo mgumu dhidi ya wapinzani wetu Morocco. Hakika tumefanya maandalizi mazuri ili kupata matokeo. Makosa yaliyopita kwenye mechi zetu tumeyafanyia kazi.

“Tumeona katika mechi zetu ambazo zimepita tulikuwa tunatengeneza nafasi. Hilo ni jambo zuri hivyo ni muhimu kuzitumia. Hatua ambayo tupo kwa sasa inahitaji matokeo na wachezaji wapo tayari.”

Tarik Sektoui Kocha Morocco awataja wachezaji watakaokosekana

Tarik
Tarik Kocha Mkuu wa Morocco.

Soma hii: CHAN 2024: Kenya 1-0 Morocco

Kocha Mkuu wa Morocco, Tarik Sektoui amebainisha kuwa wachezaji wapo tayari kuwakabili Tanzania. Amesema licha yakuwakosa wachezaji muhimu bado watapambana. Aliongeza kuwa wanawaheshimu wapinzani wao.

 “Abdelhakh Assal na Morouane wataukosa mchezo wa kutokana na kutokuwa fiti. Bouchouaib Arrasi huyu ana adhabu ya kadi za njano. Tutafanya chaguo sahihi kuwakabili Tanzania.”

Mechi za robo fainali CHAN 2024

Uganda vs Senegal mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Agosti 23 Uwanja wa Nelson Mandela. Sudan vs Algeria. Kenya vs Madagascar itakuwa ni Agosti 22 Uwanja wa Moi. Tanzania vs Morocco. Agosti 22 2025 itakuwa Tanzania vs Morocco, Uwanja wa Mkapa.

Msimamo wa Kundi A lilikuwa na Morocco

Kutoka Kundi A ni Kenya inaongoza Kundi baada ya mechi 4 imekusanya jumla ya alama 10. Morocco ikiwa nafasi ya pili na pointi 9.DR Congo nafasi ya tatu pointi 6 Angola ni nafasi ya nne ikiwa na pointi 4. Zambia nafasi ya 5 haijavuna pointi kwenye mechi zakezote.

Huu hapa msimamo wa Kundi B la Tanzania

Timu ya taifa ya Tanzania inaongoza Kundi B na pointi 10 baada ya kucheza mechi 4. Madagascar nafasi ya pili ikiwa na pointi 7 baada ya kucheza mechi nne.Mauritania nafasi ya tatu ina pointi 7 baada ya mechi nne. Burkina Faso nafasi ya tatu ina pointi 3 baada ya kucheza mechi nne.

Cental African Republic nafasi ya tano. Ina pointi moja kibindoni. Inaburuza kundi ikiwa imevuna pointi moja kwa Tanzania.

Rekodi ya mechi 7 za Tanzania

 Eswatini 1-2 Tanzania, mchezo huu ulichezwa Juni 11 2025. Tanzania 1-0 Uganda ulichezwa Julai 22 2025. Tanzania 2-1 Senegal ulichezwa Julai 27 2025.

Tanzania 2-0 Burkina Faso ulichezwa Agosti 2 2025. Huu ulikuwa ni mchezo wa ufunguzi wa CHAN 2024 Uwanja wa Mkapa. Mauritania 0-1 Tanzania, Agosti 6 2025. Tanzania 2-1 Madagascar. Agosti 16 2025, Central African 0-0 Tanzania.

Matokeo ya Tanzania CHAN 2024

Tanzania v Madagascar
Tanzania v Madagascar mchezo wa CHAN 2024.

Soma hii: Tanzania 2-1 Madagascar Mzize afunga magoli mawili

Agosti 2 2025, Tanzania 2-0 Burkina Faso. Mauritania 0-1 Tanzania. Tanzania 2-1 Madagascar, Agosti 9 2025. Agosti 16 Central African 0-0 Tanzania.

Hitimisho

Tanzania imeandika rekodi kufuzu robo fainali CHAN ikiwa haijapoteza. Inakutana na mabingwa mara mbili amba oni Morocco. 2018 na 2020 Morocco ilitwaa CHAN.

image
Share this: