- Assinki ambaye ni raia wa Ghana, amejiunga na Yanga kwa mkopo kutokea ndani ya kikosi cha Singida Black Stars.
- Hakuna kulaza damu kwani mara tu, baada ya kutambulishwa nyota huyo amejiunga kambini.
- Maajuzi Yanga SC yamsajili Frank Assinki baada ya majeruhi kwenye timu- ataipandashia kasi?
Uongozi wa Yanga SC muda mchache uliopita umetangaza kumtambulisha rasmi mlinzi, Frank Assinki. Nyota huyo ambaye pasi yake ya kusafiria inamtambua kuwa raia wa Ghana, amejiunga na Yanga kutokea Singida Black Stars. Assinki anamudu kucheza kwa usahihi katika maeneo mbalimbali uwanjani, japo anatumika zaidi kama mlinzi. Soma zaidi kuhusu jinsi Yanga SC yamsajili Frank Assinki kutoka Ghana kwa mkopo na maendeleo atakayo yaleta.
SOMA HII ZAIDI: Yanga SC wiki ya wananchi ni Ijumaa Septemba 12
Cheza sasa ‘Kindege’ SportPesa uvune mamilioni muda huu
Bado hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu.

Kuhusu usajili wa Assinki Yanga

Licha ya kumtambulisha rasmi leo, imethibitishwa kuwa Yanga tayari walimalizana na Assinki muda mrefu, ili kuboresha kikosi. Taarifa kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa, mlinzi huyo amesaini mkataba wa mkopo wa nusu msimu. Hii ni kutokana na Yanga kuwa na baadhi ya majeruhi katika eneo la ulinzi.
SOMA HII ZAIDI: Pacôme Zouzoua: Player profile, career, stats, market value, matches and latest news
Bado Yanga hawajamaliza usajili?
Licha ya kutangaza kumalizana na kutambulisha mastaa zaidi ya saba wapya mpaka sasa. Uongozi wa Yanga SC bado unaelezwa haujamaliza maboresho ya kikosi chao. Baadhi ya viongozi wao wanafuatilia kwa karibu mashindano ya Chan 2024, yanayoendelea Afrika Mashariki na chochote kinawezekana.
Ogopa matapeli Muda Pacome, Maxi, Abuya wapo Sana Yanga
Ukiachana na wapya wanaotambulishwa, Yanga pia imeendelea kuwapa mikataba mipya baadhi ya mastaa wao. Viungo wa kimataifa Pacome, Maxi na Abuya wote wameongeza mikataba ya miaka miwili kuendelea kusalia ndani ya Yanga. Hivyo mastaa hao wanatarajia kumaliza rasmi mikataba yao mwaka 2027.
Hawa hapa wazawa walioongezewa mikataba Yanga mpaka sasa
Mpaka sasa Yanga SC tayari imefanikiwa kuwaongezea mikataba baadhi ya mastaa wao kadhaa wazawa. Miongoni mwa mastaa hao ni Pamoja na nahodha wao msaidizi, Dickson Job, Kiungo Denis Nkane na Mudathir Yahya. Utaratibu huu unaendelea kwa nyota wote ambao kocha bado anawahitaji.
Kikosi kipya kunasukwa Avic Town chini ya kocha mpya Msauzi

Baada ya kucheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports nchini Rwanda, kikosi kipya cha Wananchi kimerejea kwenye kambi yao ya Avic Town, Kigamboni. Kikosi hiko kinaendelea kusukwa na aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Mamelodi Sundowns, Roman Folz. Kocha huyo ni miongoni mwa wakufunzi wenye wasifu mkubwa na uzoefu na sola la Afrika.
SOMA HII PIA: Yanga FC club profile, latest fixtures, results, news and match previews
Folz kuanza na Ngao ya Hisani Septemba 16, 2025

Mara baada ya kumaliza ratiba za Pre-season, kocha Folz anatarajiwa kuanza rasmi majukumu yake ya mechi za ushindani kupitia Ngao ya Hisani. Katika hatua hiyo Folz ataiongoza Yanga SC dhidi ya watani zao Simba SC, Mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu, ukitarajiwa kupigwa Uwanja wa Mkapa Septemba 16, mwaka huu.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC Septemba 16 Uwanja wa Mkapa | Takwimu, matokeo, H2H
Wiki ya Wananchi nayo kinawaka Septemba 12

Kuelekea msimu mpya, uongozi wa Yanga umeitangaza siku ya Ijumaa ya Ijumaa Septemba 12, mwaka huu kuwa siku rasmi ya kilele cha wiki ya Wananchi. Hii ni siku maalum ambayo, hutumiwa kwa ajili ya kutambulisha wachezaji na kikosi kipya mbele ya mashabiki. Pamoja na utambulisho huo matukio kama burudani za muziki na mechi kali ya soka hunogesha. Hili ni miongoni mwa matamasha makubwa ya michezo Afrika.
Tamasha hili awali lilitumika kwa lengo ya kuwa chanzo cha mapato, Baada ya timu kuwa na misuli ya uongozi, lengo kuu likabadilika kutoka kukusanya fedha mpaka kuwa burudani rasmi. Burudani hii huhusisha utambulisho wa wachezaji na benchi la ufundi. Hii pia inahusisha viongozi kuweka wazi shabaha ya timu kwa msimu husika.
Ili kusherehesha tukio hilo, katika miaka ya karibuni mara nyingi tamasha hilo huhusisha burudani mbalimbali za wasanii. Wasanii hao hutoka katika viwanda mbalimbali ikiwemo muziki, sarakasi na kadhalika.
SOMA HII PIA: Ali Kamwe: Kuna wachezaji wapya watatu kutambulishwa Yanga SC/ Zimbwe Jr usajili wa mkubwa
Hitimisho
Kuendana na usajili ambao Wananchi wameufanya, ikiwemo huu wa Yanga SC yashusha chuma kingine kutoka Ghana, inaonyesha dhamira yao ya kuendelea pale ilipoishia msimu uliopita. Hii ikiwa ni pamoja na kuendelea kukusanya makombe msimu ujao. Hii inaweza kuonekana pia katika namna ambavyo wamefanikiwa kuzuia mastaa wao muhimu kuondoka.

