Allan Okello mambo fresh Yanga SCJude na Okello
  • Kundi D CHAN 2024 limemaliza likiwa moto kwa timu mbili kutinga hatua ya robo fainali zote zikiwa na pointi 5 kwenye msimamo.
  • Uganda wameonyesha ubabe wao wakiwa nyumbani kwa kuvuna pointi moja katika dakika mbili za mwisho wa mchezo.
  • Tanzania kwenye kibarua kizito kuwakabili Waarabu wa Morocco hatua ya robo fainali CHAN 2024.

CHAN 2024 imekuwa na ushindani mkubwa kutokana na matokeo ya mshangao. Miongoni mwa mchezo uliokamata mashabiki macho ni Sudan 0-0 Senegal katika Kundi D. Mechi hii ilichezwa Agosti 19 kwenye Uwanja wa Amaan New Complex, Zanzibar.

Paisha kindege cha SportPesa uvune mamilioni

Ni muda wakupaisha kindege cha SportPesa. Ukiwa hewani rubani nafasi ni yako kuvuna mamilioni. Cheza sasa Aviator upate mgao wako.

SEO Banner LV

Dakika 90 za maamuzi

Timu hizi mbili zilikuwa zinawania nafasi ya kuongoza kundi. Ilikuwa ni zaidi ya fainali kwa kuwa mshindi alikuwa na nafasi kuongoza kundi moja kwa moja. Pointi moja ambayo walivuna ilikuwa faida kwa Sudan ambayo imemaliza hatua ya makundi ikiongoza.

Okelo
Okelo nyota wa timu ya taifa ya Uganda.

Soma hii: Uganda imeishinda Niger 2-0 mchuano wa Kundi C

Sudan na Senegal zimekutana mara nne

Timu hizi mbili zimekutana mara nne hivi karibuni kwenye mechi tofauti. Katika mechi hizo nne ni Senegal matokeo yao yalikuwa bora. Ushindi ni kwenye mechi mbili na sare mechi mbili huku Sudan ikiwa haijapata ushindi mbele ya Senegal.

Agosti 18 2025 Afrika Kusini 3-3 Uganda. Mabao ya Afrika Kusini yalifungwa na Ramahlwe Mphahlele dakika ya 56, Thabiso Kutumela dakika ya 59 na Ndabayithethwa Ndlondlo dakika ya 84. Uganda ni Jude Ssemugabi dakika ya 32, Allan Okello dakika ya 88 kwa mkwaju wa penalti na Rogers Ochaki Torach dakika ya 90 kwa penalti. Ndani ya dakika mbili Uganda wanafunga mabao mawili kwa penalti wakivuna pointi moja katika mchezo muhimu.

Robo fainali itakuwa namna hii

Uganda vs Senegal mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Agosti 23 Uwanja wa Nelson Mandela. Sudan vs Algeria, Uwanja wa Nelson Mandela. Kenya vs Madagascar itakuwa ni Agosti 22 Uwanja wa Moi. Tanzania vs Morocco. Agosti 22 2025 itakuwa Tanzania vs Morocco, Uwanja wa Mkapa.

Feisal Tuzo CHAN
Feisal kiungo wa Tanzania mwenye tuzo mbili ndani ya CHAN 2024.

Soma hii: CHAN 2024: Central African 0-0 Tanzania, Uwanja wa Mkapa

Msimamo wa Kundi A

Kutoka Kundi A ni Kenya inaongoza Kundi baada ya mechi 4 imekusanya jumla ya alama 10. Morocco ikiwa nafasi ya pili na pointi 9.DR Congo nafasi ya tatu pointi 6 Angola ni nafasi ya nne ikiwa na pointi 4. Zambia nafasi ya 5 haijavuna pointi kwenye mechi zakezote.

Msimamo wa Kundi B

Timu ya taifa ya Tanzania inaongoza Kundi B na pointi 10 baada ya kucheza mechi 4. Madagascar nafasi ya pili ikiwa na pointi 7 baada ya kucheza mechi nne.Mauritania nafasi ya tatu ina pointi 7 baada ya mechi nne. Burkina Faso nafasi ya tatu ina pointi 3 baada ya kucheza mechi nne.

Cental African Republic nafasi ya tano. Ina pointi moja kibindoni. Inaburuza kundi ikiwa imevuna pointi moja kwa Tanzania.

Msimamo wa Kundi C ulivyo kwa sasa

Uganda wanaongoza kundi C wakiwa na pointi 7 baada ya mechi nne. Algeria nafasi ya pili wana pointi 6. Afrika ya Kusini nafasi ya tatu wana pointi 6. Guinea nafasi ya nne pointi nne huku Niger wakiwa nafasi ya tano hawajavuna pointi mbili.

Msimamo wa kundi D

Sudan vinara wakiwa na pointi 5. Nafasi ya pili ni Senegal ina pointi 5 pia kibindoni. Nigeria nafasi ya tatu ina pointi tatu huku DR Congo ikiwa nafasi ya nne na pointi mbili zote zikiwa zimecheza mechi tatu.

Mechi tano za Senegal zilizopita

Agosti 12 2025, Senegal 1-1 Republic Of Congo, (CHAN). Agosti 5 2025, Senegal 1-0 Nigeria, (CHAN).Julai 24 2025 Uganda 2-1 Senegal, mchezo wa kirafiki. Julai 22 2025, Tanzania 2-1 Senegal mechi ya kirafiki. Julai 7 2025 Senegal 1-0 Guinea, mechi ya kirafiki.

Mechi tano zilizopita za Sudan

Sudan vs Senegal
Sudan vs Senegal CHAN 2024. Source: CAF.

Soma hii: Tanzania vs Burkina Faso na Kenya vs DR Congo: Wenyeji waanza kwa kishindo CHAN 2024.

Agosti 12 2025, : Sudan 4-0 Nigeria, (CHAN). Agosti 5 2025 Republic of Congo 1-1 Sudan, (CHAN). Machi 25, Sudan 1-1 Sudan ya Kusini kuwania kufuzu Kombe la Dunia. Machi 22 2025 Sudan 0-0 Senegal, mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia. Machi 13 2025 Oman 0-0 Sudan mchezo wa kirafiki.

Kikosi cha Sudan ambacho kilianza

Mohamed Abooja, Yaser Awad, Altayeb Abaker. Mazen Simbo, Ahmed Yousif, Abdel Raouf, Salah Adel. Walieldin Khedr, Mazin Fadul Al-Bahli, Ali Abdalla, Musa Hussien.

Wachezaji wa akiba wa Sudan

16 – Ahmed Al Fatih (mlinda mlango) 21 – Mohamed Madani (mlinda mlango) 3 – Mohamed Saeed Ahmed (beki wa kati) 2 – Musab Makeen (beki wa kulia) 22 – Faris Abdallah (beki wa kushoto). 7 – Khater Gumaa (kiungo). 10 – Maaz Kandani (kiungo). 13 – Al Misbah Faisal (kiungo) 17 – Mohamed El-Rasheed (kiungo) 14 – Mubark Abdalla (winga). 24 – Mohamed Tia Asad (winga) .12 – Awad Zayed (mshambuliaji wa kati)

Kikosi cha Senegal ambacho kilianza

M. Diof, J. Samb, (13), M. Sembene, (14), S.Ndiay (2). D. Ba, (22), O.Ba, (11), M. Yaya Ly, (17). Moussa Cisse, (6), L.Gueye, (7), C.Gomis, (9), P.Badji, (24).

Wachezaji wa akiba wa Senegal

Cheikh Ndoye (mlinda mlango), Mbaye Ndiaye (beki wa kati) Baye Ciss (beki wa kati). Amadou Coly (beki wa kulia), Ousseynou Seck (kiungo), Bonaventure Fonseca (kiungo), Moctar Koite (kiungo). Insa Boye (kiungo), Issa Kane (kiungo), Ameth Niang (kiungo). Vieux Cisse (kiungo) Ababacar Sarr (winga).

Hitimisho

Kwenye makundi timu kutoka ukanda wa CECAFA zimeongoza. Wenyeji wote ni uhakika hatua ya robo fainali CHAN 2024. Kifuatacho ni hatua ya robo fainali Agosti 22 2025.

image
Share this: