- Clement Mzize mashine ya magoli Tanzania inatajwa kuwa kwenye rada za Waarabu wa Tunisia ambao wanahitaji kuinasa saini yake.
- CHAN 2024 Mzize amekuwa katika ubora wake akifunga magoli mawili kwenye mchezo mmoja ndani ya dakika 6.
- CAF wanatambua ubora wake na wamekuwa wakimuita Goal Machine Mtanzania mwenye magoli 14 katika Ligi Kuu Bara ya NBC 2024/25.
Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga SC inaelezwa kuwa Waarabu wa Tunisia wameikomalia saini yake kwa kuweka dau nono. Klabu ya Esperance ya Tunisia inatajwa kuwa kwenye hatua nzuri kupata saini yake. Mshambuliaji huyo amekuwa gumzo kutokana na uwezo wake kuzidi kupanda chati kila wakati.
Paisha kindege cha SportPesa uvune mamilioni
Ni muda wako sasa hivi rubani shujaa kubwa bingwa. Kuna mamilioni yanakusubiri ukiwa hewani na ukitua wewe ni milionea. Chakufanya cheza Aviator upate mgao wako leo.

Timu ambazo zinatajwa kuwania saini ya Mzize
Klabu ya Esperance ya Tunisia inapewa chapuo kubwa kuipata saini yake. Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini tetesi zilikuwa zinaizungumzia. Zamalek ya Misri ilikuwa inatajwa kuwa miongoni mwa timu ambazo zinahitaji saini yake.

Soma hii: Baada ya Aziz Ki: Mzize na Aucho wanaondoka Yanga? Tetesi usajili bongo
Mzize ndani ya ligi namba nne kwa ubora
Clement Mzize kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2024/25 alikuwa chaguo la kwanza. Alicheza mechi 30 na timu hiyo ilitwaa ubingwa ikiwa na pointi 82. Kwa sasa nyota huyo yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwenye CHAN 2024.
Mzize alicheza jumla ya mechi 30 za ligi. Ni dakika 1,877 alizitumia uwanjani kwenye mechi za ushindi. Alifunga jumla ya magoli 14 kati ya 83 yaliyofungwa na Yanga SC.
Yanga SC kuhusu kuondoka kwa Mzize
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amebainisha kuwa kuna ofa ambazo zinamuhitaji Mzize. Kamwe aliweka wazi kuwa hayo yote yanatokana na kile ambacho kinaonekana uwanjani. Kuhusu alisema kwamba ni makubaliano ya kimkataba yakikamilika kila kitu kitakuwa wazi.

Soma hii: Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga SC anaondoka
“Kuhusu Clement Mzize bado ni mchezaji wa Yanga SC. Ana mkataba wa miaka miwili ambayo alisaini. Mengi yanasemwa kuhusu yeye lakini bado tupo naye kwenye timu.
“Tumepokea ofa nyingi sana ambazo zinamuhusu Clement Mzize. Wakati Mzize anaboresha mkataba wake aliambiwa anapaswa kupambana ndani ya msimu mpya. Hilo amelifanya na kazi yake imeonekana.
“Kuna taratibu linapofikia suala la mchezaji kwenda kwenye timu nyingine. Ofa za mchezaji zikifika mezani inakuwa mazungumzo ya mchezaji na klabu. Tunamwabia kuna ofa kadhaa zimekuja mchezaji anaamua wapi ambapo atakwenda kucheza.
“Ninachoweza kuwaambia mashabiki wa Yanga SC ni kwamba mchezaji wetu ana mkataba wa miaka miwili. Ambacho kitaamua aondoke ama abaki ni suala la mkataba. Kila kitu kipo sawa na utaratibu ukikamilika tutatoa taarifa kuhusu mchezaji wetu Clement Mzize,” alisema Kamwe.
Mzize kwenye timu ya taifa ya Tanzania

Soma hii: Tanzania 2-1 Madagascar Mzize afunga magoli mawili
Clement Mzize amekuwa katika mwendo mzuri jambo ambalo linakuza thamani yake.Tanzania katika CHAN 2024 imekata tiketi kutinga hatua ya robo fainali. Alikuwa na mchango mkubwa kwenye kufunga na kutengeneza nafasi za magoli.
Katika mchezo wa ufunguzi wa Tanzania dhidi ya Burkina Faso Agosti 2 alianza kikosi cha kwanza.Mzize alikuwa sababu ya penati katika mchezo huo. Bao la ufunguzi lilifungwa na Sopu na Tanzania ilishinda mabao 2-0 kwenye mchezo huo.
Agosti 6 2025 aliwaka kwa kuwa katika ubora wake. Katika mchezo wa kundi B alifunga mabao mawili peke yake. Anaingia kwenye orodha ya washambuliaji waliofunga mabao mengi kwenye mchezo mmoja.
Baada ya dakika 90 mchezo huo ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Tanzania 2-1 Madagascar. Ndani ya dakika 7 katika mashindano makubwa Afrika alifunga magoli mawili. Nyota huyo alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.
Ikumbukwe kwamba Mzize alifungua ukurasa wa magoli dakika ya 13 na 20. Goli la Madagascar lilifungwa na Nantenaina Razafimahatana dakika ya 34. Magoli yote matatu yalifungwa kipindi cha kwanza.
Mzize kamili kwa hatua ya robo fainali CHAN 2024

Soma hii: CHAN 2024: Central African 0-0 Tanzania, Uwanja wa Mkapa
Clement Mzize hakuwa kwenye orodha ya wachezaji waliocheza dhidi ya Central Afrikan. Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa timu zote zilitoshana nguvu bila kufungana. Taarifa zinaeleza kuwa alipumzishwa kuwa tayari kwa ngwe nzito inayofuata.
Mchezo ujao wa robo fainali CHAN 2024 unatarajiwa kuchezwa Agosti 2 2025. Ni Uwanja wa Mkapa kazi kubwa itakuwa kwa wababe hao kusaka ushindi ndani ya uwanja. Tanzania itacheza na Morocco ambayo ilikuwa kundi A.
Katika kundi ambalo Morocco ilikuwa ipo ni Kenya waliongoza wakiwa na pointi 10. Morocco nafasi ya pili ikiwa na pointi 9. Inakutana na vinara Tanzania ambao wanaongoza kundi B wakiwa na pointi 10.
Hitimisho
Clement Mzize ni mshambuliaji tegemeo ndani ya kikosi cha Yanga SC na timu ya taifa ya Tanzania. Kwa wachezaji wa ndani anatajwa kuwa na thamani kubwa sokoni. Ikiwa atauzwa Yanga SC itavuna mkwanja mrefu kutokana na makubaliano ambayo watafikia.


