Wadi Degla SC 0-2 Simba SCCamara Simba SC
  • Naby Camara beki wa kushoto ametambulishwa ndani ya kikosi cha Simba SC kuelekea msimu mpya wa 2025/26.
  • Zimbwe Jr alikuwa chaguo la kwanza Simba SC miaka 11 kwa sasa atakuwa ndani ya Yanga SC kwa mkataba wa miaka miwili.
  • Rushine beki wa kwanza kutambulishwa Simba SC iliyoweka kambi nchini Misri chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Simba SC hawajamaliza usajili baada ya kumtambulisha nyota mwingine mpya. Ni Naby Camara ametambulishwa rasmi kuwa nyekundu na nyeupe Agosti 14 2025. Nyota huyo aliwahi kucheza Klabu ya Al Waab ya Qatar na CS Sfaxien anatajwa kubeba mikoba ya beki Mohamed Hussen Zimbwe Jr.

Rubani ni bingwa, nafasi ni sasa paisha kindege uvune mamilioni

Nafasi ni yako rubani bingwa kuvuna mamilioni. Cheza sasa ushinde mgao wako. Rahisi sana mchezo wa Aviator sio utani unapata unachostahili.

SEO Banner LV

Camara anacheza nafasi zaidi ya moja uwanjani

Camara New
Camara mchezaji mpya Simba SC.

Soma hii: Simba SC inasukwa upya kuelekea 2025/26

Camara mwenye miaka 23 ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja akiwa uwanjani. Anamudu kucheza kiungo wa kati na beki wa kushoto. Kwenye upande wa kushoto wa ulinzi hiyo ni nafasi iliyoachwa wazi na Mohammed Hussein Zimbwe Jr ambaye alitambulishwa Yanga SC akiwa mchezaji huru.

Nyota huyo mpya wa Simba SC aliwahi kuichezea Klabu ya CS Sfaxien ya Tunisia. Msimu uliopita wa 2024/25 alikuwa akiitumikia Al-Waab Sporting Club ya nchini Qatar. Msimu wa 2025/26 atakuwa ndani ya kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Hawa hapa wapya wengine Simba SC

Rushine

Rushine Kambini
Rushine nyota mpya Simba SC akiwa kambini Misri. Source: Simba SC.

Soma hii: Baada ya Rushine Simba yamshusha Allasane Kante huyu hapa: Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Rushine De Reuck ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya Simba SC. Haya ni maandalizi kuelekea Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/26. Huyu ni beki alitambulishwa Julai 29 2025. Beki huyu yupo nchini Misri ambapo timu hiyo imeweka kambi.

Kante

Nyota Alassane Kante ambaye ni kiungo alikuwa anacheza CA Bizertin ya Tunisia. Atakuwa ndani ya Simba SC msimu wa 2025/26. Alitambulishwa Julai 30 2025.

Morice

 Morice Abraham alitambulishwa ndani ya Simba SC Julai 31 2025. Nyota huyo amesema kuwa kuna kazi kubwa yakufanya katika changamoto mpya. Yupo kambini Misri kwa maandalizi ya msimu mpya.

Semfuko

 Hussein Daudi Semfuko alitambulishwa Simba SC, Julai 31 2025 kuwa ni mali ya Simba SC. 2024/25 alikuwa akicheza Coastal Union ya Tanga. Atakuwa kwenye changamoto mpya.

Sowah

Sowah Mnyama
Sowah mshambuliaji mpya Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Soma hii: Jonathan Sowah atoa ahadi nzito Simba SC 2025/26

Jonathan Sowah alitambulishwa Simba SC, Agosti Mosi 2025. Msimu wa 2024/25 alikuwa Singida Black Stars alifunga mabao 13.

Bajaber

Agosti 2 2025 Simba SC ilimtambulisha Mohamed Bajaber. Kiungo mshambuliaji alikuwa anacheza Polisi ya Kenya. Nyota huyu ana uwezo wakufunga na kutengeneza nafasi ndani ya uwanja.

Mligo

Antony Mligo beki wa kushoto alitambulishwa ndani ya Simba SC Agosti 5 2025 alikuwa Namungo FC. Kandarasi ya miaka mitatu. Beki huyo ni mrithi wa mikoba ya Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye yupo ndani ya kikosi cha Yanga SC.

Hawatakuwa Simba SC msimu wa 2025/26

Ngoma

Fabrince Ngoma wa Simba SC alitoa Thank You Juni 29 2025. Mkataba wake wa miaka miwili ulikuwa umeisha. Hakuongeza mkataba mwingine.

Simba SC walimpa Thank You Ngoma Julai 12 2025. Hivyo nyota huyo atakuwa kwenye changamoto nyingine. Ngoma alikuwa ni imara kwenye eneo la ukabaji na kutoa pasi za uhakika akiwa na uzi wa Simba SC.

Omary Omary

Nyota huyu ametolewa kwa mkopo kuelekea Mashujaa FC ya Kigoma. Julai 12 taarifa ilitolewa na Simba SC kuwa hatakuwa ndani ya kikosi hicho. Nyota huyo hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza ndani ya Simba SC

Air Manula

Alipewa Thank You na Simba SC, Julai 12 2025. Ni kipa ambaye hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza msimu wa 2024/25. Msimu ujao atakuwa na uzi wa Azam FC.

Valentino Nouma

Nouma alipewa Thank You Julai 12 2025 huyu ni beki wa kushoto. Alisaini dili la miaka miwili akitokea St Eloi Lupopo ya DRC Congo. Ni raia wa Burkina Faso na alisaini dili la miaka mitatu walifikiana makubaliano kusitisha mkataba huo.

Hussen Kazi

Beki Hussen Kazi alipewa Thank You rasmi na Simba SC Julai 13. Hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza msimu wa 2024/25. Kwa sasa ni mchezaji huru.

Agustine Okejapha

Okejapha alipewa Thank You rasmi na Simba SC Julai 13 2025. Alisaini dili la miaka miwili akitokea Rivers United ya Nigeria. Makubaliano ya pande mbili yalifikiwa kusitisha mkataba wake.

Kelvin Kijili

Alipewa Thank You Julai 13 2025 alitangazwa ndani ya Singida Black Stars. Hivyo tayari yupo kwenye changamoto mpya. Msimu wa 2025/26 atakuwa kwenye uzi wa Singida Black Stars.

Mavambo

Deborah Mavambo alipewa Thank You Julai 19 2025. Kiungo huyu alianza vema msimu lakini alipoteza nafasi kikosi cha kwanza. Alikuwa anavaa jezi namba 17 utambulisho wake uwanjani.

Mohamed Hussen Zimbwe Jr

Zimbwe Kapten
Zimbwe Jr beki mpya wa Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Soma hii: Mohamed Hussen Zimbwe Jr ni Yanga SC

Nahodha Mohamed Hussen Zimbwe Jr aliwaaga Simba SC rasmi Julai 19 2025. Zimbwe alibainisha kuwa miaka 11 ilikuwa yenye furaha na huzuni akiwa na Simba SC hivyo anaondoka akitambua mchango wa timu hiyo. Beki huyo wa kushoto ambaye alikuwa nahodha 2024/25 akiwa na uzi wa Simba SC ni mali ya Yanga SC.

Che Malone

Aliwaaga Simba SC Julai 30 2025. Na Simba SC walimpa Thank You Julai 30 2025. Kwa sasa yupo USM Alger ya Algeria.

Hitimisho

Fadlu Davids yupo na timu nchini Misri kwa maandalizi ya msimu mpya. Camara anaungana na wachezaji wengine kambini kwa kazi kwa msimu ujao. Nyota huyo anatajwa kuwa na uwezo mkubwa kwenye kutumia mguu wa kushoto.

sportpesa jackpot
Share this: