- Uganda imeshinda Niger 2-0 na kuwa vinara kwenye kundi C CHAN 2024
- Tanzania, Kenya na Uganda ambao ni wenyeji wa CHAN 2024 ushirikiano wao umejibu mpaka katika kuwa vinara wa makundi waliyopo.
- Timu hizi mbili za taifa zimeweza kukutana mara 9 tangu mwaka 2007, Uganda wakishinda mara 5, Niger wakishinda mara 3.
Uganda imeshinda 2-0 dhidi ya Niger kwenye mchuano wa Kombe la Mataifa ya Afrika Kundi C. Mchezo huo ulichezwa Agosti 11 2025. Pointi tatu muhimu ziliwapandisha kuwa wakwanza kwenye kundi hili.
Mamilioni yanakusubiri, paisha Kindege na SportPesa
Ushindi upo siku zote kwa marubani wanaopaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa Aviator uvune mamilioni sasa hivi.

Hawa hapa wafungaji

Soma hii: Tanzania 2-1 Senegal CECAFA 2025 Arusha
Allan Okello nyota wa timu ya taifa ya Uganda alifungua ukurasa wa magoli kwenye mchezo wa CHAN 2024. Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa kwa kila timu kutafuta pointi tatu. Goli la Okello ilikuwa dakika ya 25 ya mchezo. Huku, goli la pili likifungwa na Joel Sserunjogi dakika ya 57. Wenyeji wa Michuano ya CHAN 2024, Kenya, Tanzania na Uganda wamekuwa kwenye mwendo mzuri katika hatua ya makundi.
Matokeo mengine ya CHAN 2024
Afrika Kusini 2-1 Guinea
Afrika Kusini walivuna pointi tatu mbele ya Guinea. Ilikuwa Afrika Kusini 2-1 Guinea. Magoli ya Afrika Kusini yalifungwa na Neo Gift Maema dakika ya 10 na Thabiso Simon Kutumela dakika ya 54. Goli la Guinea lilifungwa na Moussa Moise Camara dakika ya 37.
Wenyeji ni vinara kwenye makundi waliyopo

Soma hii: CHAN 2024: Kenya 1-0 Morocco
Wenyeji wa michuano ya CHAN 2024 ni vinara katika makundi waliyopo. Uganda ni Kundi C wanaongoza. Kenya wao ni Kundi A wanaongoza. Tanzania ipo Kundi B inaongoza.
Hii ni michuano mikubwa Afrika na inafanyika kwenye kanda za Afrika Mashariki. Tanzania, Kenya na Uganda. Ushirikiano wao umewapa nguvu kuandaa mashindano haya makubwa kwa pamoja.
Msimamo wa Kundi C ulivyo kwa sasa
Uganda wanaongoza kundi C wakiwa na pointi 6 baada ya mechi tatu. Algeria nafasi ya pili wana pointi 4. Afrika ya Kusini nafasi ya tatu wana pointi nne. Guinea nafasi ya nne pointi tatu huku Niger wakiwa nafasi ya tano hawajavuna pointi katika mechi mbili walizocheza.
Tazama msimamo wa Kundi B

Soma hii: Tanzania 2-1 Madagascar Mzize afunga magoli mawili
Timu ya taifa ya Tanzania inaongoza Kundi B na pointi 9 baada ya kucheza mechi 3. Mauritania nafasi ya pili ina pointi 4 baada ya mechi tatu. Burkina Faso nafasi ya tatu ina pointi 3 baada ya kucheza mechi tatu. Madagascar nafasi ya nne ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi mbili.
Jamhuri ya Kati haijakusanya pointi baada ya kucheza mechi mbili. Mchezo wake wa Agosti 9 2025 ilipoteza pia. Hivyo ipo inaburuza Kundi B.
Msimamo wa Kundi A
Kutoka Kundi A ni Kenya inaongoza Kundi baada ya mechi 3 imekusanya jumla ya alama 7. Angola ni nafasi ya pili ikiwa na pointi 4 kibindoni. Congo Dr ipo nafasi ya tatu ina pointi tatu.
Nafasi ya nne ni Morocco ikiwa na pointi tatu ilizokusanya. Ni mechi mbili imecheza ambazo ni dakika 180. Zambia inaburuza mkia baada ya mechi mbili haijakusanya pointi.
Zambia mchezo wake uliopita ilipoteza pointi tatu jumla. Baada ya dakika 90 ilikuwa Zambia 1-2 Angola. Hivyo katika pointi 4 za Angola, tatu ilivuna kwa Zambia.
Wakali wa Kundi D kazini leo
Kundi D leo Agosti 12 litakuwa kazini kwenye msako wa pointi tatu. Wakali hawa watakuwa Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar. Wakati wakushuhudia msako wa pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.
Ni mechi za raundi ya pili ambapo mabingwa watetezi, Senegal watakuwa kibaruani dhidi ya Congo Brazzaville. Mchezo wa leo ni muhimu kwa kuwa mabingwa watetezi wanasaka ushindi utakaowapeleka robo fainali. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kuanzia saa 11:00 jioni.
Baada ya mchezo huo kuna kazi nyingine nzito itakuwa. Nigeria waliopoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Senegal, watakuwa na kazi dhidi ya wabishi wa Sudan. Wababe hawa wote watakuwa wakisaka ushindi wa kwanza. Hiyo ni baada ya Sudan kutoka sare dhidi ya Congo.
Hitimisho
Uganda imeshinda 2-0 dhidi ya Niger kwenye mchezo wa CHAN 2024. Nyota Okello alikuwa kwenye ubora wake akishirikiana na wachezaji. Mechi ijayo ya Uganda dhidi ya Afrika Kusini itaamua kama itatinga hatua ya robo fainali.


