Ecua CelestinEcua Celestin
  • Yanga SC imetambulisha wapya 10 dirisha la usajili Ecua afungua Agosti Mosi 2025.
  • Benchi la ufundi kamili gado kwa kazi msimu mpya wa 2025/26 Yanga SC wakiwa ni mabingwa watetezi.
  • Mitambo ya mabao imetambulishwa Yanga SC ikiongozwa na Boyeli aliyetambulishwa Julai 31 2025.

Yanga SC imetambulisha wapya 10 dirisha la usajli la usajili huku Ecua Elastin akifungua ukurasa Agosti Mosi. Mchezaji huyo alitambulishwa usiku ikiwa ni ingizo jipya. Saa 3:30 Wananchi walitambua kwamba atakuwa Jangwani baada ya tetesi kuwa nyingi.

Mamilioni yanakusubiri rubani sasa hivi

Ni muda wa kuvuna mamilioni ukipaisha kindege hewani. Ni mchezo wa Aviator ambao unakupa ushindi haraka. Mgao upo kila siku kwa kila rubani, cheza sasa upate mgao wako.

Aviator banner

Ecua Elastin

Agosti Mosi 2025 alitambulishwa Yanga SC kwa dili la miaka miwili. Msimu wa 2024/25 alikuwa anacheza Zoman FC alifunga magoli 15 na pasi 12 za magoli. Rekodi hizo ni kwenye mashindano yote. Yeye ni raia wa Ivory Coast.

Ecua C
Ecua mshambuliaji mpya wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26: Straika mpya Yanga huyu hapa, Chama ‘Out’

Orodha ya wapya ndani ya Yanga SC 2025/26

Boyeli ilikuwa funga Julai 2025

 Julai 31 2025 Andy Bobwa Boyeli mwenye miaka 24 alitambulishwa Yanga SC. Mshambuliaji huyo alikuwa anacheza Sekhukhune United ya Afrika Kusini kwa mkopo kwa msimu mmoja. Julai 31 alifunga ukurasa kwa wachezaji waliotambulishwa ndani ya mwezi huo ambao umeisha na sasa ni Agosti.

Mkurugenzi wa ufundi ni Paul

Paul Matthews alitambulishwa ndani ya Yanga SC Julai 29 2025. Hivyo atakuwa Jangwani msimu wa 2025/26. Huyu ni Mkurugenzi wa Ufundi.

Kocha msaidizi ni Manu

Manu alitambulishwa Julai 29 2025. Huyu ni kocha msaidizi ndani ya Yanga SC. Kocha Mkuu ni Romain Folz ambaye naye ni mpya mrithi wa mikoba ya Miloud Hamdi.

Lassine Kouma

Anaitwa Lassine Kouma ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga SC. Huyu ni mrithi wa mikoba mikoba ya Khalid Aucho. Kasajiliwa Yanga SC akitokea Stade Malien.

Lassine
Lassine nyota mpya Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Lassine Kouma mrithi wa Khalid Aucho Yanga SC

Balla Conte

Ni Julai 18 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea. Nyota huyu mpya alisaini mkataba wa miaka mitatu.

Offen Chikola

 Anaitwa Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025. Ni kandarasi ya miaka miwili. 2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo.

Casemiro

 Ni Abdulnassir Mohamed maarufu kwa jina la Casemiro alitambulishwa rasmi Jangwani, Julai 23 2025. Ni mzawa ambaye atakuwa kwenye changamoto mpya. Kazi kubwa itakuwa kwenye kupambania nafasi ndani ya uwanja.

Ninju

Abubakar Nizar Othuman, maarufu kwa jina la Ninju. Huyu ni beki alikuwa Azam FC alitambulishwa rasmi Julai 27 2025. Msimu wa 2025/26 ni kijani na njano.

Kocha Mkuu Yanga SC

Ilikuwa Julai 23 2025 Kocha Mkuu wa Yanga SC Romain Folz alitambulishwa. Kocha huyo anabeba mikoba ya Miloud Hamdi aliyekuwa akikinoa kikosi hicho. Msimu wa 2025/26 atakuwa kwenye benchi la ufundi.

Orodha ya walioongeza mikataba Yanga SC

Israel Mwenda

Ilikuwa Julai 29 2025 Yanga SC ilimtambulisha Israel Mwenda kuongeza mkataba. Mwenda alitambulishwa kuongeza kandarasi ya miaka miwili Jangwani. Yupo Jangwani msimu wa 2025/26.

Mudathir Yahya

Nyota Mudathir Yahya kiungo mkabaji bado yupo ndani ya kikosi cha Yanga SC. Julai 22 2025 aliongeza mkataba wa miaka miwili. Atakuwa ndani ya Yanga SC mpaka 2027.

Dennis Nkane

Jina ni Dennis Nkane kiungo mshambuliaji wa Yanga SC aliongeza mkataba wa miaka miwili mpaka 2027. Nkane hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza msimu wa 2024/25. Kazi kubwa itakuwa kwenye kupambania namba msimu ujao kwenye benchi jipya.

Nkane alitambulishwa rasmi kuongeza mkataba Ilikuwa ni Julai 25 2025. Hivyo bado mchezaji huyo ataendelea kuwa Jangwani. Ni miongoni mwa wachezaji waliovaa medali za ubingwa msimu wa 2024/25.

Pacome

Nyota huyu alikamilisha msimu akiwa kafunga jumla ya mabao 12 na pasi 10. Kwenye mabao hayo 12 alifunga mabao mawili kwa penati. Jina ni Pacome Zouzoua aliongeza mkataba wa miaka miwili Julai 24 2025.

mMguu wake wenye nguvu kwenye kufunga magoli ni ule wa kulia. Kafunga mabao 7 kati ya 12 aliyofunga. Mguu wa kushoto katupia mabao manne. Ni pigo la kichwa alifunga bao moja mchezo dhidi ya Coastal Union.

Abuya

Duke Abuya
Duke Abuya nyota wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC 2-0 Simba SC: SportPesa, GSM watajwa kusuka mchongo huu wa ubingwa Yanga – SportPesa Tanzania

Anaitwa Duke Abuya winga wa Yanga SC ameongeza mkataba wa miaka miwili. Yupo Jangwani mpaka 2027. Julai 27 2025 alitangazwa kuongeza mkataba.

Maxi Nzengeli

Maxi Nzengeli aliongeza mkataba Julai 28 2025 wa miaka miwili. Ni njano na kijani mpaka 2027. Huyu ni mfungaji wa bao la kwanza ndani ya Yanga SC msimu wa 2024/24 alifunga dhidi ya Kagera Sugar.

Aziz Andambwile

Aziz Andambwile kiungo wa mpira bado yupo Jangwani baada ya kuongeza mkataba wa miaka miwili. Andambwile ni njano na kijani 2025/26. Rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi tano za ligi msimu wa 2024/25.

Ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wamejenga urafiki mkubwa na benchi. Hakuwa chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ambaye kwa sasa ameondoka katika timu hiyo. Ameongeza mkataba wa miaka miwili bado yupo Jangwani mpaka 2027.

Hitimisho

Mshambuliaji wa Yanga SC Clement Mzize anatajwa kuwa atauzwa. Hivyo Yanga SC ipo kwenye maandalizi kupata mbebe mikoba yake. Mzize msimu wa 2024/25 alifunga jumla ya magoli 14 kwenye ligi.

image
Share this: