- Yanga SC yatambulisha mashine mpya nne kuelekea msimu mpya wa 2025/26 wa Ligi Kuu Bara ya NBC.
- Benchi la ufundi la Yanga SC ni balaa zito kutokana na kutambulishwa wengine watatu wapya kikosini.
- Ni mabingwa watetezi walitwaa mbele ya Simba SC kwenye Kariakoo Dabi, Uwanja wa Mkapa kwa ushindi wa mabao 2-0.
Yanga SC yatambulisha mashine mpya nne ikiwa ni maandalizi kuelekea msimu wa 2025/26. Katika dirisha hili la usajili mkubwa, Yanga SC haitaki utani kutokana na kazi inayoendelea. Benchi la ufundi la Yanga SC ni balaa zito kutokana na kutambulishwa watu wa kazi.
Kindege ukipaisha unavuna mamilioni sasa hivi
Ni rahisi sana ukipaisha kindege kuna mamilioni yanakusubiri. Marubani hawafeli kwa namna yoyote ile. Cheza Aviator uvune mkwanja.

Ubingwa wao mbele ya Simba SC

Soma hii: Yanga SC 2-0 Simba SC mchezo wa Kariakoo Dabi
Ubingwa wa Yanga SC walichukua mbele ya watani zao wa jadi Simba SC. Katika mchezo wa Kariakoo Dabi uliochezwa Juni 25 2025. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 2-0 Simba SC.
Yanga SC ilifikisha pointi 82 baada ya mechi 30. Watani zao wa jadi Simba SC wakasalia na pointi 78. Kwenye mchezo huo wa funga kazi Simba SC ilipaswa kushinda ili kutwaa ubingwa na Yanga SC wao walipaswa kupata ushindi ama sare.
Mabao ya Yanga SC yalifungwa na Pacome kwa mkwaju wa penati. Clement Mzize alianzia benchi alifunga bao la pili. Mzize alitumia pasi ya Pacome ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye Kariakoo Dabi.
Wapya wanne watambulishwa kuwa mali ya Yanga SC
Yanga SC Julai 29 2025 imetambulishwa wapya wanne. Katika wapya hao wapo waliopo kwenye benchi la ufundi na mchezaji mmoja. Ni Tshephang Mokaila huyi ni fitnes coach.
Mkurugezi wa ufundi atambulishwa
Mpya mwingine wa pili ni mkurugenzi wa Ufundi. Anaitwa Paul Matthews alitambulishwa ndani ya Yanga SC Julai 29 2025. Hivyo atakuwa Jangwani msimu wa 2025/26.
Manu Rodriguez
Manu alitambulishwa Julai 29 2025. Huyu ni kocha msaidizi ndani ya Yanga SC. Kocha Mkuu anaitwa Romain Folz ambaye naye ni mpya mrithi wa mikoba ya Miloud Hamdi.
Israel Mwenda

Soma hii: KVZ FC vs Yanga patachimbika huko Muungano Cup 2025
Usiku saa 10:30 Julai 29 2025 Yanga SC ilimtambulisha Israel Mwenda. Mwenda alitambulishwa kuongeza kandarasi ya miaka miwili Jangwani. Anatimiza orodha ya wapya wanne Jangwani.
Orodha ya wachezaji wengine waliotambulishwa Yanga SC
Lassine Kouma
Lassine Kouma ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga SC. Huyu ni mrithi wa mikoba mikoba ya Khalid Aucho. Kasajiliwa Yanga SC akitokea Stade Malien.
Balla Conte

Soma hii: Balla Conte amesaini rasmi Yanga SC na kutambulishwa kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26
Julai 18 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea. Nyota huyu mpya alisaini mkataba wa miaka mitatu.
Mudathir Yahya
Mudathir Yahya Julai 22 2025 aliongeza mkataba wa miaka miwili. Atakuwa ndani ya Yanga SC mpaka 2027. Ni uhakika kuwa Jangwani msimu ujao.
Offen Chikola
Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025. Ni kandarasi ya miaka miwili. 2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo.
Casemiro
Anaitwa Abdulnassir Mohamed maarufu kwa jina la Casemiro alitambulishwa rasmi Jangwani, Julai 23 2025. Ni mzawa ambaye atakuwa kwenye changamoto mpya. Kazi kubwa itakuwa kwenye kupambania nafasi ndani ya uwanja.
Dennis Nkane
Kiungo mshambuliaji Dennis Nkane aliongeza mkataba wa miaka miwili mpaka 2027. Nkane hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza msimu wa 2024/25. Kazi kubwa itakuwa kwenye kupambania namba msimu ujao kwenye benchi jipya.
Kiungo huyu alitambulishwa rasmi kuongeza mkataba Ilikuwa ni Julai 25 2025. Hivyo bado mchezaji huyo ataendelea kuwa Jangwani. Ni miongoni mwa wachezaji waliovaa medali za ubingwa msimu wa 2024/25.
Pacome
Nyota huyu alikamilisha msimu akiwa kafunga jumla ya mabao 12 na pasi 10. Kwenye mabao hayo 12 alifunga mabao mawili kwa penati. Jina ni Pacome Zouzoua aliongeza mkataba wa miaka miwili Julai 24 2025.
Kiungo huyu mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia. Kafunga mabao 7 kati ya 12 aliyofunga. Mguu wa kushoto katupia mabao manne. Ni pigo la kichwa alifunga bao moja mchezo dhidi ya Coastal Union.
Ninju
Abubakar Nizar Othuman, maarufu kwa jina la Ninju. Nyota huyu alikuwa Azam FC. Ni beki alitambulishwa rasmi Julai 27 2025.
Abuya
Duke Abuya winga wa Yanga SC ameongeza mkataba wa miaka miwili. Yupo Jangwani mpaka 2027. Julai 27 2025 alitangazwa kuongeza mkataba.
Maxi

Maxi Nzengeli aliongeza mkataba Julai 28 2025 wa miaka miwili. Yupo hapo mpaka 2027. Huyu ni mfungaji wa bao la kwanza ndani ya Yanga SC msimu wa 2024/24 alifunga dhidi ya Kagera Sugar.
Hitimisho
Yanga SC imeachana na baadhi ya wachezaji waliokuwa kikosi cha kwanza. Khalid Aucho ambaye ni kiungo mkabaji hatakuwa na uzi wa Yanga SC. Mbali na Aucho kiungo Clatous Chama aliyesajiliwa kwa kandarasi yam waka mmoja naye hatakuwa katika kikosi hicho msimu ujao.


