Simba SC Herufi -Simba SC Herufi -
  • Simba SC yashtua na fumbo la jezi namba 6 ni Feisal au udhamini? Mashabiki wabaki gizani
  • Katika vipindi tofauti Simba SC wametajwa kuiwinda sana Saini ya Feisal, watenga dau nono.
  • Taarifa za kidukuzi pia zimeweka wazi kuwa Simba wapo mbioni kutangaza mdhamini mpya.

Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii klabu ya Simba SC imechapisha tata. Chapisho hilo ni la picha ya jezi namba 6 ikiwa na maneno “HERUFI 6”. Chapisho hilo limezua mjadala mmoja tu, kuwa Simba SC yashtua na fumbo la jezi namba 6 ni Feisal au udhamini? Mashabiki na wadau wameendelea kujiuliza swali hilo.

Shinda mamilioni na ‘Kindege’ cha SportPesa

Endelea kuhabarika na makala hii, huku pia ukicheza na kushinda mamilioni kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.

image

Kuhusu Feisal na ishu ya kusaini Simba SC

Simba SC yashtua na fumbo la jezi namba 6 ni Feisal au udhamini?
Feisal vs Simba

Taarifa za kuaminika kutoka vyanzo mbalimbali vya karibu vimethibitisha kuwa, Simba SC inapambana kumpata Feisal. Taarifa hizo pia zimeenda mbali na kuweka wazi kuwa sio Simba SC pekee, bali hata Yanga SC imeonyesha nia ya kuhitaji sahihi ya Feisal. Hii ni tangu msimu uliopita.

Lakini taarifa kutoka Azam FC zinaeleza kuwa Kocha mkuu wa timu hiyo Florent Ibenge ameweka ngumu kumuachia Feisal. Ibenge amewambia viongozi wake wasimuuze Feisal ndani ya dirisha hili. Kocha huyo amewambia wamzuie kiungo huyo kwa gharama yoyote kwani kikosi chake kipya kitajengwa kupitia Fei.

Mara kadhaa Simba na Yanga wamezungumza na kambi ya Feisal na viongozi wa Azam. Licha ya kuwepo kwa mazungumzo hayo mpaka sasa hakuna dili lolote lililokamilika. Hii ni kwa kuwa Ibenge amegoma kabisa mpango wa kumuuza Feisal.

SOMA HII ZAIDI: Feisal kucheza Simba SC Yanga SC au Azam FC Ligi Kuu NBC 2025/26? Ishu yake iko hivi

Ishu ya uzinduzi wa jezi na kumtambulisha mdhamini mpya

Simba SC Herufi -
Simba SC Herufi 6

Habari za kidukuzi zimeeleza kuwa Simba SC tayari wameachana na aliyekuwa mdhamini wao mkuu. Kufuatia hatua hiyo Simba SC sasa inajiandaa kumtangaza mdhamini wao mkuu mpya. Mdhamini huyo anakuja kuungana na Kampuni ya Jayrutty ambao ni wasambazaji wapya wa jezi za Simba.

Hivyo inaaminika kimoja kati ya haya mawili kitatangazwa Julai 29, mwaka huu. Hii itamaliza maswali mengi ambayo wadao wa soka wameendelea kuwa nayo. Kuwa je, ni Feisal au mdhamini mpya wa jezi.

SOMA HII PIA: Simba SC wamefungukia kuiwinda saini ya Feisal Salum kiungo wa Azam FC, Yanga SC nao vitani

Ishu ya usajili Simba watamba kumalizana na mashine 7 mpya

Ahmed Ally
Ahmed Ally

Kufuatia taarifa za mipango ya Simba kwenye dirisha hili la usajili. Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa Simba SC imepania kufanya usajili mkubwa kuelekea msimu wa 2025/26. Ikumbukwe kwamba timu hiyo msimu wa 2024/25 ilikosa mataji yote jambo linaloelezwa kuwapa hasira kubwa.

“Kwa sasa viongozi wa Simba SC wametapakaa kila kona kwenye nchi za Afrika. Hii ni katika kuhakikisha wanamalizia usajili wa wachezaji wapya. Huu ni usajili mwingine wa kishindo na sitaongea sana safari hii nitaacha watu waone wenyewe. Tumekamilisha usajili wa wachezaji saba na bado tunaendelea,” amesema Ahmed.

SOMA HII ZAIDI: Fei Toto kusaini Simba au Yanga? Tetesi usajili bongo, ulaya

Wachezaji walioachwa na Simba SC mpaka sasa

Ikiwa kama sehemu ya maboresho ya kikosi chao Simba tayari wameachana na kundi kubwa la wachezaji. Baadhi ya mastaa ambao wamepewa ‘thankyou’ na Simba ni Pamoja na Aishi Manula aliyeenda Azam FC. Wengine ni Pamoja na Omary Omary ambaye amepelekwa kwa mkopo Mashujaa FC.

Wengine ni, Fabrince Ngoma mkataba wake umeisha. Kelvin Kijili ametimkia Singida Black Stars. Valente Nouma naye ameachwa, nahodha Mohammed Hussein amemaliza mkataba na listi hii inatarajiwa kuongezeka. Hii ni pale Simba itakapoanza rasmi kutangaza mastaa wake.

Hitimisho huu hapa usajili mpya Simba SC

Baadhi ya majina ambayo yanatajwa kumalizana na Simba, na kuichezea timu hiyo msimu ujao ni; Sowah, kiungo Privat Djéssan Bi (21), Khadim Diaw (26), na Wilson Nangu (23). Nangu amesaini miaka miwili na Simba hivyo msimu ujao atavaa jezi nyekundu.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.