LassineLassine
  • Lassine Kouma mrithi wa Khalid Aucho Yanga SC msimu wa 2025/26 baada ya kutambulishwa kuwa Mwananchi.
  • Jezi namba 8 iliyokuwa ni utambulisho wa Khalid Aucho Yanga SC msimu wa 2024/25 ipo mikononi mwake.
  • Orodha ya wachezaji waliosajiliwa Yanga SC inazidi kupaa ikiwa ni maboresho kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC.

Lassine Kouma ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga SC kuelekea msimu wa 2025/26. Kiungo huyo ni mrithi wa mikoba ya Khalid Aucho kwa kuwa amekabidhiwa jezi namba 8. Ikumbukwe kwamba 2024/25 jezi hiyo ilikuwa inavaliwa na Aucho raia wa Uganda ambaye mkataba wake umeisha.

Lassane na Yanga SC

Kouma
Kouma ingizo jipya Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii:Feisal kucheza Simba SC Yanga SC au Azam FC Ligi Kuu NBC 2025/26? Ishu yake iko hivi

Aviator banner

Inatajwa kuwa mabosi wa Yanga SC waliingia sokoni kumfuatilia kiungo huyo kwa muda. Kutokana na Aucho mkataba wake kuisha hivyo walikuwa wanahitaji kupata kiungo mwenye nguvu eneo la ukabaji. Lassane akafikia makubalianao na Yanga SC na kusaini dili ambalo litamfanya msimu wa 2025/26 awe ndani ya kikosi hicho.

Lassane alitambulishwa rasmi Julai 25. Ni raia wa Mali. Msimu wa 2024/25 rekodi zinaeleza kuwa alifunga jumla ya mabao 7 na kutoa pasi 6 za mabao alipokuwa ndani ya Stade.

 Anakuja kujiunga na mabingwa mara 31 wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC. Yanga SC walitwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2024/25 wakiwa na pointi 82 baada ya mechi 30. Kwenye eneo la ushambuliaji walifunga jumla ya mabao 83.

Aucho na Yanga SC 2024/25

Khalid Aucho ndani ya Yanga SC, msimu wa 2024/25 alikuwa ni chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi. Kwene mechi 30 za ligi alikosekana katika mechi 8 pekee. Alicheza jumla ya mechi 22 na alikomba dakika 1,735.

Alihusika moja kwa moja kwenye mabao mawili. Alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao ndani ya mechi za ligi. Alitwaa ubingwa akiwa na kikosi hicho kilichofunga jumla ya mabao 83.

Lassane atafanya kazi na kocha mpya

Miloud Hamdi, alikuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC 2024/25. Hamdi alikutana na Thank You Julai 3 2025 hivyo hatakuwa ndani ya kikosi hicho. Yanga SC tayari wamemtambulisha kocha mpya ambaye ni Romain Folz rai awa Ufaransa.

Hivyo ni kocha mpya na kiungo mpya. Kazi kwa mchezaji huyo kuonyesha uwezo wake katika kutimiza majukumu. Msimu wa 2025/26 unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Orodha ya wachezaji wapya na walioongeza mkataba Yanga SC

Conte

Baada ya Conte kusaini ‘Tshabalala’ naye anukia Yanga SC Tetesi usajili Ligi Kuu ya NBC
Conte mchezaji mpya Yanga SC na Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Baada ya ‘Tshabalala’ na Conte Yanga SC yashusha straika Boyeli: Tetesi usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Julai 18 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea. Nyota huyu mpya alisaini mkataba wa miaka mitatu.

Mudathir Yahya

Mudathir Yahya Julai 22 2025 aliongeza mkataba wa miaka miwili. Atakuwa ndani ya Yanga SC mpaka 2027. Anaunguna na mchezaji mpya.

Offen Chikola

Kiungo mshambuliaji aliyekuwa Tabora United, Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025. Ni kandarasi ya miaka miwili. 2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo. Ni nafasi ya tano kwenye msimamo pointi 38 baada ya mechi 30 ilikusanya Tabora United.

Casemiro

 Abdulnassir Mohamed maarufu kwa jina la Casemiro alitambulishwa rasmi Jangwani, Julai 23 2025. Huyu ni mzawa ambaye atakuwa kwenye changamoto mpya. Kazi kubwa itakuwa kwenye kupambania nafasi ndani ya uwanja.

Nkane

Dennis Nkane kiungo mshambuliaji aliongeza mkataba wa miaka miwili mpaka 2027. Awali ilikuwa inaelezwa kuwa kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao wangetolewa kwa mkopo.

Nkane alitambulishwa rasmi kuongeza mkataba Ilikuwa ni Julai 25 2025. Hivyo bado mchezaji huyo ataendelea kuwa Jangwani. Ni miongoni mwa wachezaji waliovaa medali za ubingwa msimu wa 2024/25.

Pacome

Pacome saini
Pacome kiungo wa Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Soma hii:Pacome Zouzoua yupo Yanga SC asaini miaka miwili

Pacome Zouzoua aliongeza mkataba wa miaka miwili Julai 24 2025. Nyota huyu alikamilisha msimu akiwa kafunga jumla ya mabao 12 na pasi 10. Kwenye mabao hayo 12 alifunga mabao mawili kwa penati.

Pacome yupo ndani ya kikosi cha Yanga SC msimu wa 2025/26. Ni miongoni mwa wachezaji waliovaa medali kwenye mchezo wa fainali Kombe la Shirikisho Afrika. Mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia.

Hitimisho

Yanga SC wapo sokoni wakiendelea kufanya usajili kuelekea msimu mpya. Kibarua kikubwa kwa Yanga SC ni katika mechi za kitaifa na kimatafa. Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kunahitaji wachezaji wenye uwezo mkubwa na jihudi bila kuchoka.

sportpesa jackpot

Share this: