- Pacome kiungo mshambuliaji wa Yanga SC ameongeza mkataba wa miaka miwili kusalia kwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2024/25.
- Simba SC walikuwa wanatajwa kuwania saini ya kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa kutumia miguu yote miwili.
- Yanga SC yatamba baada ya kuwa na uhakika wa kubaki naye kwa mara nyingine tena.
Pacome Zouzoua yupo Yanga SC baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili. Kiungo huyo alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC amba oni watani wa jadi wa Yanga SC. Ni uhakika kwa sasa atakuwa na uzi wa njano na kijani kwa msimu wa 2025/26.

Soma hii: Pacome Zouzoua mkataba umeisha Yanga SC
Vuna mamilioni leo hii
Ni rahisi sana kuvuna mamilioni ikiwa utacheza Aviator. Unapaisha Kindege, kikiwa hewani wewe unashinda. Kila siku kuna mgao, wahi na ucheze sasa.

Rekodi za Pacome 2024/25 ndani ya Ligi Kuu Bara ya NBC
Alifunga jumla ya mabao 12 na pasi 10 za mabao ndani ya ligi Pacome. Mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia ambao ulifunga mabao 7 ule wa kushoto mabao manne kwa pigo la kichwa ni mchezo mmoja dhidi ya Coastal Union. Alitengeneza jumla ya pasi 10 za mabao kati ya mabao 83.
Alihusika kwenye jumla ya mabao 22 akiwa ni chaguo la kwanza katika Yanga SC 2024/25. Mechi ambazo alicheza ni 26 alitumia dakika 1,626. Mkononi ana tuzo ya mchezaji bora ndani ya ligi Juni na alitwaa chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ambaye naye alichaguliwa kuwa kocha bora kwa Juni.
Nyota huyo anainga kwenye rekodi za kuifunga Simba SC mzunguko wa pili Juni 25 2025. Katika mchezo wa Kariakoo Dabi, Pacome alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao kwa Clement Mzize. Alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.
Tambo za Wananchi baada ya kumtambulisha

Soma hii: Pacome wa Yanga SC na Jean Ahoua wa Simba SC vita yao waliimaliza kibabe
Kwa kuwa alikuwa akitajwa kuwa kwenye rada za Simba SC, watani zao wa jadi Yanga SC hawakuacha kutamba wakati wakimtambulisha kuwa atasalia Jangwani. Kwenye picha waliyopandisha katika ukurasa rasmi wa Instagram ya Yanga SC hawakuacha ujumbe mwepesi. Ujumbe huo ulisomeka namna hii Julai 24 2025 : “Wa kwetu tayari anabaki, bado wakwenu.”
Hawa asilimia kubwa watabaki Yanga SC
Dickson Job

Dickson Job kuna asilimia kubwa akaongeza mkataba ndani ya Yanga SC. Mara baada ya msimu wa 2024/25 kukamilika naye mkataba wake ulisha. Inaelezwa kuwa amepewa kandarasi ya miaka miwili kusalia Jangwani.
Beki huyo yupo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayojiaanda na CHAN. Tanzania itakuwa na mchezo Agosti 2 2025, Uwanja wa Mkapa. Tanzania itacheza na Burkina Faso, ukiwa ni mchezo wa ufunguzi.
Maxi Nzengeli
Ipo wazi kuwa 2024/25 alifungua pazia la kufunga mabao ndani ya ligi. Maxi alifunga bao hilo kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba. Baada ya dakika 90 ilikuwa Kagera Sugar 0-2 Yanga SC mchezo wa NBC.
Maxi alifunga bao hilo kwa pasi ya Pacome kwenye mchezo huo. Nyota huyu mkataba wake naye umeisha. Inaelezwa kuwa ni kandarasi ya miaka miwili ataongeza.
Orodha ya wachezaji wanaotajwa kuachwa Yanga SC
Jonas Mkude
Kiungo mkabaji Jonas Mkude kandarasi yake imeisha. Aliongezewa mkataba wa mwaka mmoja kusalia Jangwani. Inatajwa kuwa Singida Black Stars wanahitaji huduma yake.
Khalid Aucho
Khalid Aucho raia wa Uganda kandarasi yake imeisha. Inaelezwa kuwa alitarajiwa kupewa mkataba wa mwaka mmoja, Ujio wa Balla Conte umesitisha kubaki kwake. Hivyo kwa sasa ni mchezaji huru.
Kennedy Musonda
Mshambuliaji Kennedy Musonda anatajwa kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi msimu ujao. Musonda mkataba wake naye umeisha. Inaelezwa kuwa hataongezewa mkataba mwingine.
Dennis Nkane
Kiungo mshambuliaji Dennis Nkane bado hajawa chaguo la kwanza ndani ya Yanga SC. Inatajwa kuwa huenda akasajiliwa na Singida Black Stars. Nyota huyu mzawa alifanya kazi na Miguel Gamondi ambaye kwa sasa yupo Singida Black Stars.
Tetesi za wachezaji wanaowindwa na Yanga SC
Feisal Salum – Yanga SC
Feisal Salum, kiungo wa Azam FC anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC. Kiungo huyo mshambuliaji aliibuka Azam FC akitokea Yanga SC. Imekuwa inaelezwa kuwa huenda akarejea kwa mara nyingine Jangwani.
Taarifa zinaeleza kuwa mbali na Yanga SC kuiwinda saini ya kiungo huyo Simba SC nayo inaiwinda saini ya Feisal. Nyota huyo bado ana kandarasi ya mwaka mmoja na Azam FC. Ni pasi 13 za mabao alitengeneza na kufunga mabao manne msimu wa 2024/25 katika kikosi cha Azam FC kwenye NBC.
Mohamed Hussen Zimbwe Jr-Yanga SC

Soma hii: Simba SC yakata tamaa kuhusu Zimbwe Jr
Beki huyu wa upande wa kushoto tayari amewaaga mashabiki wa Simba SC. Julai 19 Zimbwe Jr alibainisha kuwa hatakuwa ndani ya kikosi hicho. Ni miaka 11 alidumu kwenye maisha ya kutimiza majukumu ndani ya kikosi cha Simba SC.
Taarifa zinaeleza kuwa atajiunga na Yanga SC. Inaelezwa kuwa beki huyo kasaini dili la miaka miwili. Hivyo msimu wa 2025/26 atakuwa kijani na njano.
Edmund John – Yanga SC
Huyu ni winga mzawa mwenye ambaye ni mali ya Singida Black Stars. Taarifa zinaeleza kuwa tayari mazungumzo yameanza kufanyika. Ni suala la makubaliano na kutambulishwa ndani ya Yanga SC ni jambo ambalo limebaki.
Hitimisho
Yanga SC imekamilisha utambulisho wa wachezaji wawili wapya ambao ni Offen Chikola na Moussa Balla Conte. Hii yote ni maandalizi kuelekea msimu wa 2025/26. Wapo wachezaji ambao wataondoka ndani ya kikosi hicho na wengine mikataba yao inaboreshwa.


