Feisal kucheza Simba SC Yanga SC au Azam FC Ligi Kuu NBC 2025/26Feisal
  • Feisal kucheza Simba SC, Yanga SC au Azam FC Ligi Kuu NBC 2025/26? Ndio ubuyu wa moto mjini.
  • Ni kweli kuwa Simba SC na Yanga SC katika nyakati tofauti zote zimeonyesha kuhitaji sahihi ya Feisal.
  • Kocha mpya wa Azam FC, Florent Ibenge ametoa msimamo mzito ishu ya Feisal.

Kuna tetesi nyingi za usajili zinaendelea kwenye majukwaa tofauti ya michezo hapa nchini. Lakini kubwa ya yote ni swali kuhusu Feisal kucheza Simba, Yanga au Azam Ligi Kuu NBC 2025/26.? Hii ni baada ya kuwepo kwa taarifa ya vigogo hao wa Kariakoo kutaka kumng’oa Chamazi.

Shinda mamilioni na ‘Kindege’ cha SportPesa

Endelea kuhabarika na makala hii, huku pia ukicheza na kushinda mamilioni kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.

image

Feisal kucheza Simba SC Yanga SC au Azam Ligi Kuu NBC 2025/26? Ishu ikoje?

Feisal kucheza Simba SC Yanga SC au Azam FC Ligi Kuu NBC 2025/26
Feisal

Ni kweli kuwa Simba na Yanga katika nyakati tofauti zote zimeonyesha kuhitaji sahihi ya Feisal. Taarifa za wakubwa hao kumtaka zilianza tangu mwishoni mwa msimu ulipita. Kwa sasa tetesi hizo zimekuwa kubwa kiasi cha kuwaacha mashabiki na maswali mengi juu ya hatima ya kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania.

SOMA HII PIA: Fei Toto kusaini Simba au Yanga? Tetesi usajili bongo, ulaya

Kocha Ibenge atoa msimamo mzito kuhusu Feisal

Kufuatia michakato hiyo ya kumng’oa Feisal Chamazi. Kocha mpya wa Azam FC, Florent Ibenge amewambia viongozi wake wasimuuze Fei Toto ndani ya dirisha hili. Kocha huyo amewambia wamzuie kiungo huyo kwa gharama yoyote kwani kikosi chake kipya kitajengwa kupitia Fei.

Mara kadhaa Simba na Yanga wamezungumza na kambi ya Feisal na viongozi wa Azam. Licha ya kuwepo kwa mazungumzo hayo mpaka sasa hakuna dili lolote lililokamilika. Inaelezwa Ibenge amegoma kabisa mpango wa kumuuza Feisal japo Simba hawajakata tamaa.

Feisal kuondoka huru Azam?

Ikumbukwe mpaka sasa, Feisal amebakiza mwaka mmoja tu ndani ya kikosi hiko cha Azam FC. Hivyo kama watafanikisha kumbakisha basi mwakani mwezi wa Sita atakuwa mchezaji huru. Hii itamfanya kuwa huru kujiunga na timu yoyote atakayofikia makubaliano nao.

Ishu ya Sowah na Simba SC mwenyewe athibitisha

Jonathan Sowah rasmi asaini Simba SC
Jonathan Sowah Simba

Aliyekuwa straika wa zamani wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah ameonyesha viashiria vya wazi vya kuthibitisha kusaini Simba SC. Sowah kupitia akaunti yake ya Instagram ameposti picha ikimuonyesha akiwa na jezi ya Sima. Ikumbukwe Sowah msimu uliopita akiwa na Singida aliifungia mabao 13.

SOMA HII ZAIDI: Jonathan Sowah rasmi asaini Simba SC: Ahmed atangaza mashine 7 mpya  tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Sowah kuchukua nafasi ya Ateba dili la Simba

Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika vimethibitisha kuwa Simba imemalizana na straika wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah. Imeelezwa Sowah anakuja kuchukua nafasi ya straika Lionel Ateba ambaye anatarajiwa kutimkia uarabuni. Imethibitishwa kuwa Simba walikamilisha dili la Sowah usiku wa kuamkia leo Jumatano.

“Usiku wa Jumanne Simba SC wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah. Usajili umetokea baada ya Sowah kuridhishwa na mpango wa Simba SC. Ni rasmi sasa, Sowah aliyemaliza msimu na mabao 13 atavaa jezi ya Simba msimu ujao,” ilieleza taarifa hiyo.

Semaji Ahmed afichua kuwa mashine 7 mpya zimesaini Simba

Ahmed Ally
Ahmed Ally

Kufuatia taarifa za mipango ya Simba kwenye dirisha hili la usajili. Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa Simba SC imepania kufanya usajili mkubwa kuelekea msimu wa 2025/26. Ikumbukwe kwamba timu hiyo msimu wa 2024/25 ilikosa mataji yote jambo linaloelezwa kuwapa hasira kubwa.

“Kwa sasa viongozi wa Simba SC wametapakaa kila kona kwenye nchi za Afrika. Hii ni katika kuhakikisha wanamalizia usajili wa wachezaji wapya. Huu ni usajili mwingine wa kishindo na sitaongea sana safari hii nitaacha watu waone wenyewe. Tumekamilisha usajili wa wachezaji saba na bado tunaendelea,” amesema Ahmed.

SOMA HII PIA: Aishi Manula anaondoka Simba SC, Fei Toto atajwa Yanga SC, tetesi kuelekea 2026/26

Wachezaji walioachwa na Simba SC mpaka sasa

Kama sehemu ya maboresho ya kikosi chao Simba tayari wameachana na kundi kubwa la wachezaji. Baadhi ya mastaa ambao wamepewa ‘thankyou’ na Simba ni Pamoja na Aishi Manula aliyeenda Azam FC. Wengine ni Pamoja na Omary Omary ambaye amepelekwa kwa mkopo Mashujaa FC.

Wengine ni, Fabrince Ngoma mkataba wake umeisha. Kelvin Kijili ametimkia Singida Black Stars. Valente Nouma naye ameachwa, nahodha Mohammed Hussein amemaliza mkataba na listi hii inatarajiwa kuongezeka. Hii ni pale Simba itakapoanza rasmi kutangaza mastaa wake.

Hitimisho: Hawa wanatajwa kuwa wachezaji wapya wa Simba

Baadhi ya majina ambayo yanatajwa kumalizana na Simba, na kuichezea timu hiyo msimu ujao ni; Sowah, kiungo Privat Djéssan Bi (21), Khadim Diaw (26), na Wilson Nangu (23). Nangu amesaini miaka miwili na Simba hivyo msimu ujao atavaa jezi nyekundu.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.