Ali Kamwe (-)Ali Kamwe (-)
  • Yanga SC imekomalia saini ya Balla Conte kiungo anayetajwa kuwa kwenye rada za Simba SC.
  • Simba SC vs Yanga SC kwenye vita nyingine kuwania saini za wachezaji wapya kwa msimu wa 2025/26.
  • Mohamed Hussen Zimbwe Jr anatajwa kuingia rada za Yanga SC baada ya kumaliza mkataba wake Simba SC.

Yanga SC imekomalia saini ya kiungo wa CS Sfaxien ya Tunisia Balla Conte ikiwa ni vita yao na mtani wa jadi Simba SC. Inaelezwa kuwa ni Yanga SC walianza kuulizia huduma ya mchezaji huyo ambaye ana mkataba wa mwaka mmoja na timu yake kisha wakafikia makubaliano na timu. Hii ni vita nyingine wanaingia watani hawa wa jadi nje ya uwanja baada ya msimu wa 2024/25 kukamilika.

Baada ya Conte Yanga yatua kwa Tshabalala wa Simba SC Tetesi usajili Ligi Kuu NBC
Conte kiungo anayetajwa kuwaniwa na Yanga SC vs Simba SC.

Soma hii: Simba SC waivuruga Yanga SC dili la Balla Conte

Vuna mamilioni sasa

Vuna mamilioni ukicheza Aviator ni rahisi. Unapaisha Kindege kikiwa hewani unavuna mkwanja. Ushindi unakusubiri wewe, cheza upate mgao wako.

SEO Banner LV

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC aliweka wazi kuwa kila kitu kuhusu usajili kinafanyika kwa umakini mkubwa. Kamwe aliongeza kuwa kwa zama hizi ni ngumu Yanga SC kuibiwa mchezaji kama ambavyo tetesi zinaeleza kuwa Conte ameibiwa na Simba SC juu kwa juu. Ni Julai 22 Yanga SC wanatarajiwa kuanza kutambulisha wachezaji wapya na wale ambao wataachana nao.

“Tumejipanga kufanya vizuri kuelekea kwenye dirisha kubwa la usajili. Kipindi cha usajili kinahitaji umakini mkubwa ukizingatia timu nyingi zipo sokoni. Ili kupata wachezaji bora na wenye nguvu za kupambania ubingwa ni lazima tuwe na fedha hivyo mashabiki waendelee kuchangia tofali la ubingwa mazuri yanakuja,” alisema Kamwe.

Wachezaji watakaochwa na Yanga SC

Clatous Chama

Chama Jr
Chama Jr kiungo wa Yanga SC 2024/25. Source: Yanga SC.

Soma hii: Clatous Chama kiungo wa Yanga SC kusaini Zesco United

Kiungo mshambuliaji Clatous Chama anatajwa kuwa kwenye rada za Azam FC na Zesco United ya Zambia. Chama mkataba wake na Yanga SC umeisha tayari na hajaongezewa mkataba. Taarifa zinaeleza kuwa Simba SC kwa sasa hawana mpango wa kumrejesha kiungo huyo.

Jonas Mkude

Kiungo mkabaji wa Yanga SC mkataba wake umeisha. Inaelezwa kuwa hataongezewa kandarasi nyingine. Kuna uwezekano akawa mchezaji huru.

Kennedy Musonda

Mshambuliaji Kennedy Musonda anatajwa kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi msimu ujao. Musonda mkataba wake naye umeisha. Inaelezwa kuwa hataongezewa mkataba mwingine.

Wachezaji wanaowindwa na Yanga SC

Feisal Salum – Yanga SC

Feisal Salum, kiungo wa Azam FC anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC. Kiungo huyo mshambuliaji aliibuka Azam FC akitokea Yanga SC. Imekuwa inaelezwa kuwa huenda akarejea kwa mara nyingine Jangwani.

Taarifa zinaeleza kuwa mbali na Yanga SC kuiwinda saini ya kiungo huyo Simba SC nayo inaiwinda saini ya Feisal. Nyota huyo bado ana kandarasi ya mwaka mmoja na Azam FC. Ni pasi 13 za mabao alitengeneza na kufunga mabao manne msimu wa 2024/25 katika kikosi cha Azam FC kwenye NBC.

Mohamed Hussen Zimbwe Jr-Yanga SC

Zimbwe Jr
Zimbwe Jr nahodha wa Simba SC 2024/25. Source: Simba SC.

Soma hii:Mohamed Hussen Zimbwe Jr amefuta utambulisho wa Simba SC

Nahodha wa Simba SC, Mohamed Hussen Zimbwe Jr kwa msimu wa 2024/25, mkataba wake umeisha hivyo kwa sasa yupo huru. Jina lake linatajwa kuwa katika hesabu za Yanga SC. Mabosi wa Simba SC wanaendelea na mazungumzo na beki huyo huku Yanga SC nao wakitajwa kuivizia saini yake.

 Edmund John – Yanga SC

Huyu ni winga mzawa mwenye ambaye ni mali ya Singida Black Stars. Taarifa zinaeleza kuwa tayari mazungumzo yameanza kufanyika. Ni suala la makubaliano na kutambulishwa ndani ya Yanga SC ni jambo ambalo limebaki.

Jonathan Sowah- Yanga SC

Mshambuliaji wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC. Sowah aliwahi kuweka wazi kuwa timu ambayo anaipenda ni Yanga SC. Ilikuwa inaelezwa kuwa Simba SC nao walikuwa wanamfuatilia mshambuliaji huyo. Yanga SC inapewa nafasi kubwa kuipata saini ya mchezaji huyo rai awa Ghana. 

Wachezaji ambao wataongezewa mikataba hawa hapa:-

Dickson Job wa Yanga SC

Job
Job Dickson nyota wa kikosi cha Yanga SC, 2024/25. Source: Yanga SC.

Soma hii:Dickson Job kusaini mkataba mpya

Dickson Job beki chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Yanga SC anatarajiwa kuongezewa mkataba mpya. Mkataba wa beki huyo ambaye alikuwa katika orodha ya kikosi bora msimu wa 2023/24 umegota mwisho. Kwa sasa ni mchezaji huru.

Job yupo na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars nchini Misri. Stars inajiandaa na CHAN ambayo inatarajiwa kuanza Agosti 2. Tanzania itacheza na Burkina Faso, Uwanja wa Mkapa ukiwa ni mchezo wa ufunguzi.

Mudathir Yahya

Kiungo mkabaji ambaye ni kiraka huyu anatajwa kuwa ataongeza mkataba mpya. Mudathir mkataba wake umeisha na mazungumzo yanatajwa kufikia sehemu nzuri. Kiungo huyo ambaye mguu wake wenye nguvu zaidi ni ule wa kulia huenda akaongeza mkataba wa miaka miwili.

Pacome Zouzoua

Kiungo mwenye mabao 12 na pasi 10 za mabao ndani ya ligi Pacome. Mkataba wake umeisha na mazungumzo yanaendelea. Alionyesha kiwango bora Juni alipocheza mechi tatu na kufunga mabao matatu. Miongoni mwa timu ambazo alizifunga ni Simba SC Kariakoo Dabi.

Mkononi ana tuzo ya mchezaji bora wa NBC kwa Juni. Inatajwa kuwa ni mkataba wa miaka miwili atapewa nyota huyu. Hivyo ni suala la kusubiri kutangazwa.

Maxi Nzengeli

Mfungaji wa bao la kwanza ndani ya msimu wa 2024/25. Maxi alifunga bao hilo kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba. Baada ya dakika 90 ilikuwa Kagera Sugar 0-2 Yanga SC.

Alitumia pasi ya Pacome kwenye mchezo huo. Nyota huyu mkataba wake naye umeisha. Inaelezwa kuwa ni kandarasi ya miaka miwili ataongeza.

Khalid Aucho

Kiungo mkabaji Khalid Aucho rai awa Uganda kandarasi yake imeisha. Inaelezwa kuwa dili jipya ambalo atasaini ni mwaka mmoja. Ikiwa watafikia makubalianao mazuri atabaki Jangwani.

Hitimisho

Yanga SC kwenye usajili kuelekea msimu wa 2025/26 wamebainisha kuwa watafanya maboresho kidogo kutokana na wachezaji walionao. Malengo makubwa kuelekea 2025/26 ni kufanya vizuri katika mashindano ya ndani na nje. Ni Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga SC ambao ni mabingwa watashiriki.

image
Share this: