- Mo Dewji aibua jambo Simba SC baada ya kupishana na mataji manne ya Ligi Kuu Bara NBC wakiambulia patupu.
- Bilioni 87 zatajwa, kazi ipo msimu wa 2025/26 kwenye msako wa ushindi kitaifa na kimataifa.
- Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini bado yupoyupo ndani ya Simba SC akiwa kwenye majukumu makubwa.
Rais wa heshima wa Klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji (Mo) ameweka wazi kuwa timu hiyo haitashikika msimu wa 2025/26. Mo Dewji ameibua jambo hilo Simba SC ikiwa ni msimu wa nne unakwenda bila taji la ligi kabatini. Ipo wazi kuwa 2024/25 Simba SC iliambulia patupu katika mataji iliyokuwa inapambania. Ni Kombe la Shirikisho Afrika, Ligi Kuu Bara na CRDB Federation Cup.

Shinda mamilioni sasa hivi
Una nafasi kushinda mamilioni muda huu na rahisi sana. Unachotakiwa kufanya ni kucheza Aviator mchezo wa kupaisha kindege. Wakati upo angani, mkwanja unaingia mfukoni.

Kwa mataji ya ndani Simba SC ilishuhudia Yanga SC inayodhaminiwa na SportPesa ikiyatwaa yote. Kwenye anga la kimataifa ni nafasi ya pili iliishia mabingwa wakiwa ni RS Berkane ya Morocco. Simba SC kwenye ligi iliishia nafasi ya pili vinara wakiwa ni Yanga SC.
Jambo la Mo Dewji
Mo Julai 16 aliandika ujumbe kwa mashabiki wa Simba SC ulimwenguni kote kubainisha kuwa furaha inakuja. Aliongeza kuwa licha ya kuwa kwenye kuijenga timu walifanikiwa kufika fainali Kombe la Shirikisho Afrika. Kwa maana hiyo chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids wanaamini msimu ujao hawatazuilika.
“Tulia. Tathmini. Panga upya. Nimefurahi kuwa na mazungumzo ya maana na kocha Fadlu katika msimu wake wa kwanza. Akiwa na kikosi kipya na benchi jipya la ufundi, ameiongoza Simba SC kufika fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.
“Chini ya kocha Fadlu Davids, Simba imefika fainali ya CAF Confederation Cup, fainali ya pili ya kimataifa katika historia ya klabu. Msimu huu ulikuwa wa kujenga timu. Na bado tukafika fainali, licha ya upinzani mkali. Simba haitazuilika msimu ujao,”.
Julai 15 2025, Mo Dewji alizungumzia kuhusu suala la uwekezaji ndani ya Simba SC. Ilikuwa inaelezwa kuwa Mo hatoi hela jambo ambalo alilipinga kwa kubainisha kuwa wanaosema hatoi hela ni fitina. Kiasi cha Bilioni 87 alibainisha kuwa kilitumika katika maeneo mbalimbali ikiwa ni usajili, kambi, mishahara ya wachezaji na huduma za dharula.
Simba SC na Fadlu Davids

Soma hii: Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC asilimia ndogo kubaki
Fadlu mwenye umri wa miaka 44 ni kocha aliyekiongoza kikosi cha Simba SC kwa mafanikio. Kwenye mechi 30 za ligi ambazo ni dakika 2,700 timu hiyo ilipoteza mechi mbili. Sare ilikuwa katika mechi tatu huku ikiambulia ushindi kwenye mechi 25.
Ilimaliza msimu wa 2024/25 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo. Timun amba mbili kufunga mabao mengi ambayo ni 69. Mbali na kufunga mabao mengi ni timu namba mbili kufugwa mabao machache ambayo ni 13.
Timu ambazo alifundisha Fadlu Davids
2016 alitangazwa kuwa kocha wa muda ndani ya kikosi cha Maritzburg United. Fadlu alicheza katika timu hiyo 2007-12 akiwa ni mshambuliaji. Rekodi zinaonyesha kuwa alifunga jumla ya mabao 18.
2017 alitangazwa kuwa kocha mkuu wa Martzburg United ya Afrika Kusini. Hivyo alikabidhiwa majukumu yote kwa ajili ya kuwapa mbinu wachezaji wat imu hiyo. Ana uzoefu na soka la Afrika kutokana na kuwa mchezaji kwa muda mrefu na kocha kwenye timu kubwa.
Kocha huyo aliwahi kuifundisha pia Orlando Pirates ya Afrika Kusini. Hiyo ilikuwa ni 2019-21 akiwa ni kocha msaidizi. Raja Casablaca alifanya kazi hapo 2023/24 akiwa ni kocha msaidizi. Aliajiriwa na Simba SC 2024. Ni Julai 5 2025 alitangazwa kuwa kocha mkuu wa Simba SC.
Mkataba ambao alisaini Simba SC ni miaka miwili. Tayari mwaka mmoja umekwisha hivyo ana mwaka mmoja kusalia ndani ya kikosi hicho kilichoishia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi. Ni pointi 78 kilikusanya baada ya mechi 30.
Ishu ya kuondoka Simba SC

Soma hii: Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC anatajwa Raja Casablanca
Fadlu Davids alikuwa anatajwa kuwa kwenye hesabu za kurejeshwa Raja Casablanca. Mbali na Raja ilikuwa inaelezwa kulikuwa na mvutano ndani ya Simba SC kuhusu kocha huyo abaki ama aondoke. Licha ya timu kutinga fainali Kombe la Shirikisho Afrika na kuishia nafasi ya pili.
Kupoteza mechi tatu mbele ya Yanga SC kulikuwa kunatajwa kuwa sababu ya kocha huyo kutopewa kipaumbele. Ipo wazi kwamba katika mechi tatu ambazo ni dakika 270, Simba SC ilipoteza mbele ya Yanga SC msimu wa 2024/25. Katika Ngao ya Jamii hatua ya nusu fainali, Simba SC ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Ni mechi mbili za ligi Yanga SC ilipata ushindi nje ndani.Mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba SC 0-1 Yanga SC na mzunguko wa pili ilikuwa Yanga SC 2-0 Simba SC. Pacome na Mzize Clement walifunga mabao kwenye mchezo wa pili.
Licha ya Fadlu kandarasi yake kuwa imesalia mwaka mmoja hakuwa na uhakika kama atabaki ndani ya Simba SC. Katika mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Yanga SC alibainisha kuwa kuhusu yeye kubaki itafahamika baadaye.
Hitimisho
Fadlu akiwa na Simba SC msimu wa 2024/25 kwenye ligi alipoteza mechi mbili pekee kati ya 30 na zote ilikuwa dhidi ya Yanga SC. Simba SC kwenye anga la kimataifa ikiwa katika Kombe la Shirikisho iliishia nafasi ya pili. Ilipoteza mbele ya RS Berkane kwa jumla ya mabao 3-1.


