Dennis KibuDennis Kibu
  • Kibu Dennis mkandaji wa Simba SC anatajwa kupata timu Marekani kwa ajili ya changamoto mpya 2025/26.
  • Bosi wa Simba SC aweka bayana kuhusu mkataba wa mchezaji huyo na mahali alipo kwa sasa.
  • Mipango mizito yapangwa Simba SC kuelekea msimu mpya ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC.

Kibu Dennis mkandaji kiungo wa Simba SC anatajwa kupata timu Marekani. Nyota huyo aliongeza mkataba wa miaka miwili mwaka 2024 hivyo bado mwaka mmoja mkataba wake kugota mwisho. Ikiwa kuna timu inamuhitaji inapaswa kuzungumza na uongozi wa Simba SC.

Kibu Dennis Zanzibar
Kibu Dennis kiungo wa Simba SC kwenye mazoezi 2024/25. Source: Simba SC.
Aviator banner

Soma hii: Kibu Dennis kuikosa Fountain Gate Ligi Kuu Bara

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa wapo wachezaji ambao wanahitajika na timu nyingine. Ahmed aliongeza kwa kusema jambo hilo linatokana na ubora wa wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho. Ikiwa utaratibu utafuata watauzwa.

“Kuna wachezaji ambao wanahitajika na timu nyingine hilo lipo wazi. Ikiwa tutaona kuna umuhimu wa kumuuza tutafanya hivyo. Ila kuhusu Kibu bado ana mkataba na Simba SC na yupo Marekani na familia yake,” alisema Ahmed.

Kibu D Mkandaji (-)
Kibu D Mkandaji kwenye mchezo wa kimataifa Kombe la Shirikisho 2024/25. Source: Simba SC.

Soma hii: Mnyama Simba Kafanya yake CAF 2024/25 kwa Mkapa

Mkandaji Kibu rekodi zake kimataifa

Kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, dhidi ya Al Ahli Tripol alifunga bao moja.Ilikuwa dakika 36 Uwanja wa Mkapa. Mchezo huo ulichezwa Septemba 22 2024 alitumia mguu wake wa kushoto akiwa ndani ya 18.

Bao jingine alifunga kwenye mchezo dhidi ya SC Sfaxine ilikuwa Desemba 15 2024. Kibu kwenye mchezo huu alifunga mabao mawili na alikuwa nyota wa mchezo. Ukurasa ulifunguliwa dakika ya 7 akiwa ndani ya 18.

Wakati wapinzani wao SC Sfaxine wakiamini mchezo umekwisha, dakika ya 90 alirudi kambani kwa mara nyingine. Bao hilo la jioni alitumia pigo la kichwa zikiwa zimesalia sekunde kadhaa mchezo kuisha. Ni pasi ya Yusuph Kagoma alitumia kufunga kwenye mchezo huo.

Simba SC ilipotinga hatua ya makundi bado moto wa Kibu haukuzima. Alifunga bao kwenye mchezo dhidi ya Constantine uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Ilikuwa ni Januari 19 2025 dakika ya 61 kwa mguu wa kulia.

Ikumbukwe kwamba katika anga la kimataifa, Simba SC ilitinga hatua ya fainali. Ilipoteza kwa kufungwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya RS Berkane. Hivyo Simba SC msimu wa 2024/25 katika anga la kimataifa ni washindi wa pili Kombe la Shirikisho Afrika.

Rekodi za Kibu Dennis ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC

Kibu alifungua ukurasa wa pasi za mabao kwenye mchezo dhidi ya Azam FC. Ilikuwa Februari 24 2025 Uwanja wa Mkapa alimpa pasi ya bao Ellie Mpanzu dakika ya 25. Alitoa pasi mbili za mabao kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji.

Ni dakika ya 45 alimpa pasi ya bao Jean Ahoua na dakika ya 15 alimpa Mpanzu pasi zote alitoa kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18. Mchezo huu ulichezwa Machi 14 2025, Uwanja wa KMC Complex.

Pasi yake ya nne alifunga kwenye mchezo dhidi ya KengGold. Ilikuwa dakika ya 22 alimpa Mpanzu akiwa nje ya 18. Mchezo huu ulichezwa Juni 18 ilikuwa ni raundi ya 30 Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Mabao yake ndani ya ligi

Kibu Dennis alifungua ukurasa wa mabao kwenye mzunguko wa pili. Kiungo huyo aliyeyusha mwaka mzima bila kufunga bao kwenye mechi za ligi. Ni timu mbili alizifunga Kibu msimu wa 2024/25 na mabao aliyokuwa akifunga ilikuwa ni mwendo wa mbilimbili.

Alianza kufunga kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji. Alipachika bao la kwanza dakika ya 54 kwa pigo la kichwa. Bao la pili alipachika dakika ya 69 kwa mguu wa kulia. Balaa lake ilikuwa ndani ya 18 alipofunga mabao yote hayo mawiliMachi 14 2025 Uwanja wa KMC Complex.

Funga kazi ilikuwa dhidi ya KenGold raundi ya 30. Alifunga bao la tatu dakika ya 20. Bao la nne alipachika dakika ya 25. Ni dakika 5 ilikuwa ni tofauti ya muda wakufunga bao moja kwenye mchezo huo ambao ulichezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Mabao yote mawili kwenye mchezo wa funga kazi alitumia mguu wa kulia. Ilikuwa Juni 18 2025. Mwisho ubao ulisoma KenGold 0-5 Simba SC, pointi tatu kwenye mchezo wa NBC zilikuwa mali ya Simba SC.

Tuzo zake ndani ya 2024/25

Kibu Denis
Kibu Denis kiungo wa Simba SC akiwa na tuzo yake ya NBC. Source: Simba SC.

Soma hii: Yanga SC vs Simba SC vitani usajili wa Conte kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26. Yanga watangaza Tofali la ubingwa

Kabati la Kibu lina jumla ya tuzo mbili pekee za mchezaji bora msimu wa 2024/25. Tuzo ya kwanza aliipokea kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, alipofungua ukurasa wake wa mabao na kutoa pasi mbili za mabao. Tuzo yake ya pili alichukua kwenye mchezo dhidi ya KenGold.

Kibu kafunga msimu wa 2024/25 na mabao yake manne. Kahusika kwenye mabao 8 ndani ya Simba SC iliyogotea nafasi ya pili na pointi 78. Nyota huyo baada ya tuzo kwenye mchezo dhidi ya KenGold aliweka wazi ni furaha kwake kuwa kwenye ubora.

“Ninafurahi kuona timu inapata matokeo mazuri. Kikubwa tuzo hii ni maalumu kwa ajili ya mashabiki. Wamekuwa nasi kila wakati hili ni jambo lakujivunia.”

Hitimisho

Kibu Dennis ndani ya Simba SC ni mechi 24 za ligi alicheza. Katumia dakika 1,538 huku akifunga mabao manne na kutoa pasi nne za mabao. Simba SC imegotea nafasi ya pili kwenye msimamo ikipishana na taji la ligi.

image
Share this: