- Aishi Manula amesaini mkataba kuitumikia Azam FC akitokea Simba SC iliyocheza fainali Kombe la Shirikisho Afrika 2024/25.
- Rekodi zake akiwa na uzi wa Simba SC 2017/18 zilikuwa ni moto, Moussa Camara alipambania kuzifikia.
- Anakutana na Kocha Mkuu Florent Ibenge aliyekuwa anafundisha Al Hilal ya Sudan ndani ya Azam FC.
Aishi Manula amesaini mkataba kuitumikia Azam FC akitokea Simba SC mpaka 2028. Kipa huyo alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi hao wa Azam FC kwa muda mrefu hatimaye dili lake limejibu. Anarejea katika timu yake ya zamani aliyokuwa akiitumikia kabla ya kusajiliwa na Simba SC.

Soma hii: Aishi Manula anaondoka Simba SC, Fei Toto atajwa Yanga SC
Vuna mamilioni sasa hivi

Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege. Kwa kila anayepaisha kindege ana nafasi kubwa kushinda. Ni muda wako kuvuna pesa sasa na Aviator, cheza kila siku.
Manula na Azam FC
Manula amerejea ndani ya kikosi cha Azam FC akitokea kwa waajiri wake Simba SC akiwa mchezaji huru. Mkataba wa Manula na Simba SC ambao aliongeza ulikuwa unafikika mwisho Julai 2025. Kipa huyo yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachojiandaa na CHAN.
Kwa msimu wa 2025/26 atakuwa ndani ya Azam FC, matajiri wa Dar. Julai 5 2025 mabosi wa Azam FC walimambulisha kocha mpya ambaye ni Florent Ibenge. Hivyo Ibenge ataanza kufanya kazi na ingizo jipya kwenye eneo la kipa ambaye ni Manula.

Soma hii: Mdaka mishale Diarra kabadili upepo, rekodi zake hizi hapa – SportPesa Tanzania
Manula ni miongoni mwa makipa wenye uwezo mkubwa kwenye eneo la kulinda lango. Alikuwa kwenye kikosi cha Simba SC ambacho kilitinga hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika. Simba SC ilipoteza mbele ya RS Berkane licha ya kwamba hakuanza langoni bado historia itamkubuka.
Ikumbukwe kwamba Air Manula alikuwa ndani ya kikosi cha Azam FC 2012-17. Anarejea nyumbani kuendelea na majukumu yake upya. Simba SC alidumu kutoka 2017-2025 akiwa ni miongoni mwa makipa waliofanya kazi katika mechi za kitaifa na kimataifa.
Manula ndani ya Simba SC 2024/25
Msimu wa 2024/25 akiwa ndani ya Simba SC hakupata nafasi kucheza mchezo hata mmoja wa ligi namba nne kwa ubora. Manula alipata nafasi kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan alitumia dakika 45 pekee. Timu ya Al Hilal kwa wakati huo ilikuwa inanolewa na Ibenge kwa ambaye kwa sasa ni kocha wa Azam FC.
Kipa namba moja kwa Simba SC msimu wa 2024/25 alikuwa ni Moussa Camara. Kwenye mechi 30 za ligi Camara alikaa langoni mechi 28. Mechi mbili langoni alikaa Ally Salim ambaye huyu ndani ya dakika 180 hakufungwa.
Rekodi yake yafikiwa na Camara

Soma hii: Simba SC kuachana na makipa wote kuelekea 2025/26
Moussa Camara kipa namba moja wa Simba SC aliifikia rekodi ya Aishi Manula katika kukusanya hati safi ndani ya uwanja. Manula alipokuwa kipa namba moja wa Simba SC alikuwa kwenye ubora wake na alijenga ufalme kwa kukomba tuzo na kuwa kwenye kikosi cha kwanza.
Alitwaa tuzo ya kipa bora msimu wa 2017/18. Rekodi yake alikusanya hati 19 safi akiwa langoni. Rekodi hiyo ilifikiwa na kip awa msimu wa 2024/25 ndani ya Simba ambaye ni Moussa Camara.
Camara, Juni 22 2025 alianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar. Kwenye mchezo huo ambao ulikuwa ni wa 27 kwake aliokoa hatari mbili zilizokuwa zinakwenda langoni mwake ya kwanza ilikuwa dakika ya 24 ni Momo wa Kagera Sugar jaribio lake akiwa ndani ya 18 liliokolewa.
Dakika ya 42 Mahundi alifanya jaribio ambalo liligotea kwenye mikono ya Camara ambaye alipiga shuti lililolenga lango. Mwisho ubao wa Uwanja wa KMC Complex ukasoma Simba SC 1-0 Kagera Sugar bao la Steven Mukwala dakika ya 17. Mchezo huo Camara akafikisha hati 19 ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika.
Ni hati safi 19 alifikisha Camara akiwa anaongoza katike eneo hilo huku anayemfuatia ni Djigui Diarra wa Yanga mwenye hati safi 17 msimu wa 2014/25. Mchezo wake wa 28 Camara alikwama kuipindua rekodi ya Manula kwa kuwa aliokota mabao mawili. Baada ya dakika 90 Juni 25 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 2-0 Simba SC.
Camara alifikia rekodi ya Aishi Manula ambaye atakuwa chini ya Ibenge msimu wa 2025/26. Manula aliiandika rekodi hiyo msimu wa 2017/18 alipokuwa kipa namba moja wa Simba SC. Kwa sasa Manula atakuwa ndani ya Azam FC. Rekodi yake itakumbukwa na kutunzwa na mabosi wake wa zamani.

Soma hii:Aishi Manula anaondoka Simba SC, Fei Toto atajwa Yanga SC
Hitimisho
Mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC unatajwa kuwa miongoni mwa siku mbaya kazini. Kwenye mchezo huo. Ilikuwa Novemba 5 2023 ubao ulisoma Simba SC 1-5 Yanga SC. Langoni alikaa Aishi Manula ambaye alikuwa amekaa nje ya uwanja kwa muda zaidi ya siku 99 kwa kuwa hakuwa fiti.


