- Tuzo ya kiatu cha ufungaji bora msimu wa 2024/25 itakuwa mikononi mwa kiungo mshambuliaji wa Simba Jean Ahoua ambaye kafunga jumla ya mabao 16.
- Clement Mzize wa Yanga SC ni mshindani wake mkuu, kamaliza msimu wa 2024/25 akiwa na mabao 14 ni mzawa namba moja kwa kufunga mabao mengi.
- Aziz Ki alitwaa tuzo hiyo msimu wa 2023/24 akiwa na uzi wa Yanga SC ambao ni mabingwa wa ligi msimu wa 2024/25.
Jean Ahoua kubeba tuzo kiatu cha ufungaji bora 2024/25. Kiungo huyo mshambuliaji wa Simba SC amekamilisha msimu wa 2024/25 akiwa anaongoza chati ya ufungaj akifikisha mabao 16. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 tuzo hiyo ilikuwa mikononi mwa Aziz Ki.

Hii hapa ni orodha ya nyota waliokuwa wakiwania tuzo ya ufungaji bora. Ulikuwa ni msimu wenye ushindani mkubwa na kila mchezaji akitimiza majukumu yake. Kazi ilikuwa namna hii:-
Jean Ahoua, Simba SC-16

Soma hii: Kariakoo Dabi kuna vita nyingine kwa wachezaji
Kinara wa kucheka na nyavu ndani ya ligi ni kiungo mshambuliaji wa Simba SC Jean Ahoua. Nyota huyo kaufunga jumla ya mabao 16 ndani ya msimu wa 2024/25. Bao la 16 alifunga kwenye mchezo dhidi ya KenGold dakika ya 75.

Ahoua ana jumla ya pasi 9 za mabao na kafunga mabao 16. Kahusika kwenye mabao 25 kati ya 69 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 78 baada ya mechi 30.
Katika mabao 16 ambayo kafunga, mabao 15 kafunga kwa mguu wa kulia. Bao moja alifunga kwa pigo la kichwa dhidi ya Pamba Jiji akitumia pasi ya Ellie Mpanzu. Mabao 6 alifunga kwa mikwaju ya penati.
Clement Mzize wa Yanga SC-14
Mshambuliaji namba moja kwa wazawa ni Clement Mzize akiwa kafunga jumla ya mabao 14. Mzize ambaye ni chaguo la kwanza la Miloud kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate alichaguliwa kuwa mchezaji bora.

Soma hii: Ufungaji bora 2024/25 orodha ya waliopo kwenye vita
Alikuwa na siku nzuri kazini kwenye mchezo dhidi ya Simba SC. Katika mchezo huo aliingia dakika ya 45 akichukuwa nafasi ya Prince Dube. Alipachika bao dakika ya 87 akitumia pasi ya Pacome na kufikisha mabao 14 kwenye ligi.
Yanga SC ikiwa imefunga mabao 83, kafunga mabao 14 na kutoa pasi tano za mabao. Mechi tatu mfululizo alikuwa kwenye ubora dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji alitoa pasi za mabao kwa Clatous Chama. Kwenye Kariakoo Dabi yeye alifunga.
Prince Dube, mabao 13
Nyota wa Yanga SC, Prince Dube Juni 25 2025 alikomba dakika 45 Kariakoo Dabi. Ana mabao 13 na pasi 8 za mabao ambazo zinamfanya ahusike kwenye mabao 21 kati ya 83 ambayo yamefungwa na Yanga SC.
Ikumbukwe kwamba hakuwa fiti asilimia 100. Kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alipata maumivu. Kagotea kwenye mabao 13.
Leonel Ateba wa Simba SC-13

Soma hii: Yanga SC 2-0 Simba SC mchezo wa Kariakoo Dabi
Mbele ya Yanga SC kwenye mechi mbili alikuwa kwenye vita kubwa na Ibrahim Bacca. Hajaingia kwenye orodha ya waliofunga katika mchezo wa Kariakoo Dabi. Alianza kwa kasi ambayo ilianza kupungua taratibu mpaka mwisho wa msimu wa 2024/25.
Leonel Ateba kafunga mabao 13 na kutengeneza pasi nne. Kwenye mchezo dhidi ya KenGold alifunga bao lake la 13 na alitoa pasi moja iliyomuongezea namba mpaka kuwa na pasi nne za mabao msimu wake wa kwanza akiwa na uzi wa Simba SC.
17 ni idadi ya mabao ambayo amehusika nayo ndani ya Simba SC. Mabao 69 yamefungwa na Simba SC baada ya mechi 30. Kwenye msimamo ni nafasi ya pili ikiwa na pointi 78.
Steven Mukwala wa Simba SC-13
Steven Mukwala mshambuliaji wa Simba SC kafunga jumla ya mabao 13.Nyota huyo alianza kikosi cha kwanza mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC na kukutwa mara tatu kwenye mtego wa kuotea. Bao lake la 13 alifunga kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa KMC Complex.
Pacome Zouzoua mabao 12
Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Pacome kagotea kwenye mabao 12. Alipachika bao la 12 kwenye Kariakoo Dabi dakika ya 66 kwa mkwaju wa penati. Alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo huo.
Ni pasi 10 za mabao anazo ndani ya msimu wa 2024/24. Kwenye mchezo dhidi ya Simba SC alitoa pasi ya bao kwa Clement Mzize. Kahusika kwenye mabao 22 kati ya 83 yaliyofungwa na Yanga SC.
Hitimisho
Mchezaji mwenye mabao mengi kwa wazani ni Clement Mzize ambaye kafunga 14. Nyota huyo bao lake la 14 alifunga kwenye mchezo dhidi ya Simba SC. Pasi ya Pacome ilitosha kuimaliza Simba SC kwa kufunga bao hilo na kufanya ubao wa Uwanja wa Mkapa, Juni 25 2025 kusoma Yanga SC 2-0 Simba SC.

