wafungaji bora ndani ya boksi la 18Jean Charles Ahoua
  • Kariakoo Dabi Juni 25 2025 kuna vita nyingine kwa wachezaji ndani ya uwanja kwenye dakika 90 za kusaka ushindi.
  • Bingwa wa msimu wa 2024/25 atakabidhiwa taji lake baada ya dakika 90 kukamilika. Yanga SC anahitaji pointi moja abebe taji hilo Simba SC pointi tatu.
  • Pacome Zouzoua wa Yanga SC na Jean Ahoua kwenye vita eneo la kiungo mshambuliaji Kariakoo Dabi Uwanja wa Mkapa.

Kariakoo Dabi kuna vita nyingine kwa wachezaji ndani ya uwanja ukiweka kando msako wa pointi tatu muhimu. Mchezo huo namba 184 unatarajiwa kuchezwa leo Juni 25 2025 Uwanja wa Mkapa. Yanga SC ambao ni wenyeji wa mchezo wanaongoza ligi wakiwa na pointi 79 huku Simba SC wakifuata nafasi ya pili na pointi 78.

NI Pacome Zouzoua wa Yanga SC na Jean Ahoua wa Simba SC kwenye vita kubwa ya rekodi Uwanja wa Mkapa. Viungo hawa wawili wamekuwa katika ubora kwenye mechi za ushindani. Juni 25 2025 wanatarajiwa kukutana kwenye Kariakoo Dabi mzunguko wa pili 2024/25.

Baada ya Aziz Ki: Mzize na Aucho wanaondoka Yanga?
Pacome kiungo mshambuliaji wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Kizungumkuti Yanga SC vs Simba SC Kariakoo Dabi

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza Simba SC walipoteza. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 0-1 Yanga SC. Bao la ushindi kwa Yanga SC lilikuwa ni lakujifunga kupitia kwa beki Kelvin Kijili.

Mechi ipo au haipo?

Kumekuwa na mvutano mkubwa kuhusu mechi ya Juni 25 2025. Yanga SC wapo tayari kwa mchezo huo wa kufunga msimu wa 2024/25. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC alibainisha kuwa taarifa itatolewa.


Ahmed amesema: “Kiu kubwa ya mashabiki wa Simba SC ni kuhusu tarehe 25. Nichukue fursa hii kuwaambia mashabiki wote wa Simba SC kuwa kama kuna lolote la kuwaambia kuhusiana na tarehe 25, tutawaambia.”

Screenshot------------------sportpesa-co-tz

Yanga SC wapo kamili kwa kazi

Miloud Hamdi, Kocha Mkuu wa Yanga SC ameweka wazi wapo tayari kwa mchezo huo. Kocha huyo alibainisha kuwa ambacho wanahitaji ni ushindi ili watwae taji la ubingwa. Maandalizi na wachezaji wote wapo kamili.

“Tupo tayari kwa mchezo wetu wa Dabi dhidi ya Simba SC. Tunawaheshimu wapinzani wetu kwa kuwa nit imu imara.Ila kikubwa ambacho tunahitaji kwenye mchezo wetu ni ushindi ili kutwaa taji la ubingwa.”

Vita ya viungo Pacome na Ahoua ipo hapa

Kwenye eneo la viungo kuna vita kwa nyota wa Yanga SC vs Simba SC. Pacome na Ahoua wapo kwenye ubora mkubwa ndani ya uwanja. Namba zao zimekuwa zikiongea mara nyingi katika majukumu yao.

Rekodi zinaonyesha kuwa Pacome Zouzoua ndani ya Yanga SC iliyofunga mabao 81 amehusika katika mabao 20. Amefunga mabao 11 na kutoa pasi 9 za mabao. Ni dakika 1,536 kayeyusha. Kacheza jumla ya mechi 25 kati ya 29 ambazo Yanga SC imecheza.

Pacome Z (-)
Pacome kiungo wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC vs Simba sc, Juni 25 2025 kivumbi kitawaka

Pacome amekosekana kwenye mechi nne pekee kati ya 29. Ni chaguo la kwanza la Miloud kwenye mechi za ushindani za ligi. Mchezo raundi ya 28 dhidi ya Tanzania Prisons alifunga mabao mawili na alianza kikosi cha kwanza.


Kwenye mabao 11 ambayo Pacome amefunga bao moja kwa penalty. Bao hilo alifunga kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa KMC Complex mlinda mlango wa Kagera Sugar alikuwa ni Ramadhani Chalamanda.


Mbali na kufunga, Pacome ana pasi 9 za mabao. Kiungo huyo kahusika kwenye mabao 20 kati ya 81 yaliyofungwa na Yanga SC. Huenda akaanza kikosi cha kwanza dhidi ya Simba SC.

Yanga SC walikomba pointi tatu mazima kwenye mchezo huo. Ni pointi sita walivuna mbele ya Kagera Sugar msimu wa 2024/25. Mzunguko wa kwanza walipata ushindi wa mabao 2-0 Uwanja wa Kaitaba.

Kiungo Jean Ahoua wa Simba SC rekodi


Simba SC ni Jean Ahoua amehusika katika mabao 25. Simba SC imefunga jumla ya mabao 69. Ni pasi 9 kateneneza akifunga mabao 16. Ni kinara katika chati ya wafungaji kwa sasa.

Ahoua amecheza jumla ya mechi 27 kati ya 29 akikosekana katika mechi mbili ambazo ni dakika 180. Katika mabao 16 aliyofunga kafunga mabao 6 kwa penalti. Penalti yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Dodoma Jiji.

Jean Ahoua (-)
Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC.Source: Simba SC.

Soma hii: Simba SC 1-0 Kagera Sugar ni mchezo wa mwisho 2024/25

Ni Mohamed Hussen alisababisha penati hiyo kipindi cha pili. Ahoua alifunga penati hiyo kwa mguu wake wa kulia. Rekodi zinaonyesha kuwa Ahoua kafunga mabao 15 kwa mguu wa kulia na bao moja kwa pigo la kichwa.

Makipa Yanga SC vs Simba SC kwenye vita yao

Camara Moussa
Camara Moussa

Soma hii: Yanga SC vs Simba SC Juni 25 2025 matukio makubwa mawili kufanyika

Mbali na vita ya viungo, kuna vita kwenye eneo la makipa. Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza, Camara alipotezwa na Diarra. Baada ya dakika 90 mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba SC 0-1 Yanga SC, hati safi alisepa nayo Diarra.


 Camara anaongoza kwa hati safi akiwa nazo 19 kibindoni. Camara ni mechi 27 amekaa langoni akifungwa mabao 11. Mechi mbili Ally Salim alikaa langoni kwa Simba SC na hakufungwa. Amekomba dakika 2,430 Camara.

Diarra ni mechi 22 alikaa langoni ametumia dakika 1,980 ni hati safi 16 kakusanya akifungwa mabao 8. Juni 22 2025 hakuwa langoni dhidi ya Dodoma Jiji, Aboutwalib Mshery alikaa langoni. Baada ya dakika 90 ilikuwa Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji.

Mchezo wa leo Juni 25 2025 umeshikilia hatma ya ubingwa. Simba SC ili awe bingwa ni lazima ashinde kwa kuwa ana pointi 78 akiachwa pointi moja na Yanga SC yenye pointi 79. Yanga SC akishinda ama kutoa sare atakuwa bingwa.

Share this: