Mechi Yanga SC vs Singida Black Stars Juni 28Ali Kamwe
  • Yanga SC wametoa matakwa manne ambayo yanapaswa kukamilika kwa wakati ili wapangue mpango wa kugomea kucheza mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC ulioahirishwa Machi 8 2025.
  • Juni 15 2025 iliyopangwa kwa ajili ya Kariakoo Dabi mzunguko wa pili yakataliwa na Yanga SC wakihitaji tarehe nyingine mpya ikiwa matakwa manne yatatimia.
  • Almas Kasongo CEO wa Bodi ya Ligi, Wilfred Kidao Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kwenye orodha.

Yanga SC wametoa matakwa manne ili kucheza mchezo dhidi ya Simba SC kwa tarehe nyingine ambayo itapangwa na sio Juni 15 2025 ambayo ipo kwa sasa kwa watani hao wa jadi Yanga SC na Simba SC kukutana uwanjani.

Ateba na Diarra
Ateba wa Simba SC na Diarra kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza 2024/25. Source: Simba SC.

Soma hii:Sakata la kuyeyuka Kariakoo Dabi Machi 8 2025, sababu zipo hivi – SportPesa Tanzania

Ikumbukwe kwamba mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa Machi 8 2025 ukaahirishwa na ukapangiwa kuchezwa Juni 15 2025 ambayo Yanga SC wameweka wazi kuwa hawatacheza kwa namna yoyote ile. Mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba SC 0-1 Yanga SC.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC ameweka wazi kuwa hawatanii katika jambo hili huku akiweka wazi matakwa manne ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kucheza mchezo huo wa mzunguko wa pili namna hii:-

“Tumetoa matakwa manne. Katika haya manne matatu ni matakwa ambayo tunaamini yakitekelezwa kwa haraka klabu yetu ya Yanga SC itakuwa tayari kwenda uwanjani kucheza mechi kwa tarehe nyingine itakayopangwa.

Kamwe
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii:Yanga SC vs Simba SC iliyopangwa Juni 15 2025: Ngoma imekuwa ngumu, Yanga yatishia maamuzi magumu

 “Matatu yanahusu mchezo namba 184, tunaamini yakifanyiwa kazi hayo matatu kwanza, tutakuwa tayari kucheza mechi hiyo kwa tarehe nyingine itakayopangwa. Na takwa la nne ni la muda mrefu, kuanzia msimu ujao. CEO wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo asiudanganye UMMA kwa kuchagua kuzungumzia takwa moja tu na kuacha yanayotakiwa kushughulikiwa kwa haraka ikiwemo yeye mwenyewe kujiuzulu.

Takwa la kwanza na la pili la Yanga SC

“Takwa letu la kwanza  na la pili linahusu ukiukwaji wa kanuni uliofanyika Machi 8. Tunataka Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi pamoja na CEO wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo wawajibike kwa kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia kanuni na kuutia doa mpira wetu. Ligi yetu ni kubwa sana Afrika na inataka watu makini wenye weledi kuiongoza.

Kasongo
Kasongo CEO TPLB. Source: TPLB.

“Kuahirishwa kwa mechi ya Machi 8 tunaamini kama klabu hapakufuatwa utaratibu na kulikuwa na uvunjaji mkubwa wa kikanuni hivyo tunaamini CEO wa Bodi ya Ligi na kamati ya uedeshaji wa kamati ya ligi ilifanya hayo kwa ajili ya kuwapa favour timu fulani. Klabu ya Yanga SC haitakuwa tayari kushiriki mechi namba 184 kama kamati nzima ya uendeshaji na usimamizi wa bodi haitajiuzulu au kuvunjwa.

Takwa la tatu la Yanga SC  

“Takwa letu la tatu ni kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya maamuzi mabovu ya mara kwa mara ya waamuzi. Kamati ya waamuzi ipo chini ya TFF kwa Katibu Mkuu, unashangaa ni vipi mwamuzi mmoja anafanya makosa yakujirudia na bado anaendelea kupangwa kwenye mechi bila kuchukuliwa adhabu yoyote ile.

“Napenda kuwajuza waandishi wa Habari, yasipofanyiwa kazi matakwa yetu matatu kwa uharaka, Yanga SC hatutakuwa tayari kucheza mchezo namba 184, mechi zote mbili za Ligi zilizobaki na hatutashiri Ligi Kuu Msimu ujao. Huu ndio msimamo wetu na hatutayumba kwa lolote.

Sakata la mechi ya fainali ya CRDB Federation Cup takwa la nne

“Taarifa hii iwafikie ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF na Wadhamini wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB, kuwa hatutacheza mchezo wa Fainali wa CRDB siku ya tarehe 28, mpaka tutakapolipwa hela yetu ya Ubingwa kwa msimu uliopita. Tumevumilia dharau hizi kutoka kwa Mamlaka za Soka kwa muda mrefu sana, sasa imefika mwisho. Hii ya Zanzibar pia hatuchezi.

C Chama
Wachezaji wa Yanga SC ambayo imetinga hatua ya fainali CRDB Federation Cup. Source: Yanga SC.

Isome hii:Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali ya CRDB, Ngoma kupigwa Zanzibar 28/06/2025

“Kama wanafikiri tunatania waendelee kupuuza, katika hili Klabu ya Yanga SC tuko serious zaidi ya wanavyodhani na tuko tayari kwa lolote litakalotokea. Na kama yuko mmoja wao anadhani kupunguza pointi ya Yanga ni rahisi, na ajaribu kufanya hivyo na asuburi aone nguvu ya wananchi.”

CEO bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB)

Almas Kasongo, CEO wa TBLB amesema :”Wenzetu wamekuja na mambo manne ambayo sisi kama bodi tuna wajibu wa kupokea na kuyachakata, sio kupokea tu na kuyachakata. Azimio la kwanza kuvunjwa kwa kamati ya usimamizi na uendeshaji ya bodi ya ligi. Kuna kamati ya kusimamia na kuendesha ligi ipo kwenye kanuni.

“Jambo la pili kujiuzulu kwa ofisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, jambo la tatu kujiuzulu kwa katibu Mkuu wa TFF na jambo la nne bodi ya ligi iwe chombo huru. Itoshe kusema kuwa tumepokea lakini haya mambo yote manne yapo nje ya uwezo wa Mwenyekiti wa Bodi, mamlaka ya utendaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu ndio wana uwezo kuyafanyia kazi na tutapeleka kwenye mamlaka husika.

“Kama nilivyotangulia kusema kwa haya waliyoyaleta tumeyapokea ila yapo nje ya uwezo wetu tuna mamlaka ya kuwasilisha kwa mamlaka inayohusika ili kuyafanyia maamuzi. Kwa yale ambayo yapo ndani ya uwezo wetu ikiwa ni ratiba sisi ratiba yetu ipo kama ilivyopangwa kwa sababu chombo kinachoendesha na kusimamia ligi ni chombo kingine.

“Ratiba yetu tulisema kuwa mechi namba 184 itachezwa Juni 15 2025, sisi tuna wajibu kupeleka hoja katika mamlaka husika, ratiba ipo vilevile mpaka kamati itakapotoa taarifa nyingine. Yanga SC nafasi yao ni kwamba wangetamani haya yafanyike ili warudi kwenye mchezo, ukitazama haya yanawezekana lakini haitakuwa kwa siku moja ni mchakato ambao unahusisha kamati nyingi. Ukiyatazama maazimip yapo nje ya mamlaka ya bodi ya ligi.”

Share this: