- Yanga SC wamegomea kuzungumza na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) sakata la zawadi ubingwa wa CRDB Federation Cup 2023/24.
- TFF yakomelea msumari suala lipo palepale katika kukamilisha jambo hilo lazima wakae mezani na nyaraka zote.
- CEO wa Yanga SC ashikilia msimamo kile wanachotaka ni zawadi yao hakuna kingine kwa kuwa walishashinda ubingwa.
Yanga SC wamegomea kuzungumza na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kuhusu Sakata la kudai hela za zawadi ubingwa wa CRDB Federation Cup 2023/24 mara baada ya kufika makao makuu mapema Juni 11 2025 baada ya kupokea wito.

Soma hii:Sakata la Yanga SC na hela za ubingwa CRB Federation Cup 2024 lazua balaa
Cliford Ndimbo, Ofisa Habari wa TFF amesema kuwa Yanga SC wamegoma kuongea walipoitwa kwa wito maalumu kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa masuala ya fedha zaidi ya kuacha barua, licha ya Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao kumuita Mtendaji Mkuu wa Yanga SC, Andre Mtine aligomea wito huo.
Ikumbukwe kwamba Juni 9 2025, Yanga SC kupitia kwa Ofisa Habari Ali Kamwe walibainisha kuwa hawatacheza mchezo wa fainali ya CRDB Cup 2024/25 mpaka watakapolipwa hela za ubingwa wa msimu wa 2023/24 ambazo walidai kwa muda mrefu.

Soma hii: Yanga SC wametoa matakwa manne yakitimizwa Kariakoo Dabi kuchezwa
Katika taarifa ya Yanga SC walibainisha kuwa hawatacheza mchezo wa fainali ya CRDB Federation Cup unaotarajiwa kuchezwa Juni 28 Uwanja wa Amaan Zanzibar ikiwa hawatalipwa hela zao za ubingwa. Baada ya taarifa hiyo Juni 10 2025 CRDB walitoa taarifa kuhusu kukamilisha malipo yote yaliyokuwa yanahitajika kwa mujibu wa mkataba hivyo wao wanaamini kwamba hawadaiwi kitu chochote kwa kuwa walishakamilisha taratibu zote.
TFF walitoa taarifa kuhusu suala hilo kwa kubainisha kuwa kulikuwa na makubaliano maalumu kati ya Yanga SC na TFF zawadi za ubingwa na kuwaita Yanga SC wafike ofisini kufanyaukaguzi wa fedha hizo. Juni 11 2025 saa 4 asubuhi.
Huyu hapa Ndimbo Ofisa Habari wa TFF
“Baada ya kuona taarifa mitandaoni kuhusiana na kwamba kuona Yanga SC wameeleza kwamba wanaidai TFF na sisi tuliwaandikia barua kuhusiana na kile ambacho tunakifahamu. Mpaka tunatoa taarifa hiyo jana, (Juni 10 2025) tayari tulikuwa tumewaandikia barua Yanga SC kuwaomba kwamba waje na mtu wao wa fedha ili tuone wapi wanadai na baada ya kufika wameleta barua na kuacha barua na kuweka wazi kuwa hawapo tayari kwa mazungumzo.
“Klabu ya Yanga wamefika wameleta barua na kuondoka na wamesema hawana chochote cha kuzungumza, Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao alipotaka kuzungumza na CEO wa Yanga SC Andre Mtine alikataa.
“Wao wanataka kuona kwamba tunaandikiana barua. Hizi ni taasisi kubwa haiwezekani kuishi kwa kuandikiana barua. Jambo dogo ni kwamba kama wewe unadai ama unadaiwa ilikuwa ni jambo rahisi kufika TFF ni jambo la muda mfupi na rahisi sana.

Soma hii: Mechi Yanga SC vs Singida Black Stars Juni 28 2025: Wananchi wasisitiza ‘Dawa ya deni ni kulipa’
“Na sio kila jambo tunapaswa kuandikiana barua maana yake jambo lilikuwa wazi na ilikuwa wafike TFF na kujadiliana sasa hatuwezi kuendelea kuwa tunaandikiana barua kama tunatoa posa. Haiwezekani kufanya hivyo, hizi ni taasisi kwa hiyo wameondoka na wamesema kuwa hawapo tayari kwa ajili ya kufanya jambo hilo wameondoka na wameacha barua tu. Barua ambayo wameandika bado jambo lao lipo vilevile hivyo mwisho wa siku jambo lipo palepale wafike TFF.
“Tumesema kwamba tunawadai Yanga SC hivyo utaratibu upo vilevile wanapaswa waje TFF. Kwa kuwa tayari tuliwataka mtu wa fedha afike na vielelezo vingine ili tupitie hesabu kwa pamoja kuona wapi ambapo wanasema wanadai nasi tuseme wapi ambapo tunadai.”
Huyu hapa CEO Yanga SC
Mtendaji wa Yanga (CEO), Adre Mtine alifika TFF Juni 11 2025 baada ya kufika hapo taarifa zinaeleza kuwa aliacha barua na kuondoka bila kufanya mazungumzo na uongozi. Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kutoka ofisi za TFF alisema:”Sisi hatutaki chochote zaidi ya zawadi yetu ya ubingwa kama kuna jambo lolote watuwasilishie kwa njia ya maandishi ila kwasasa hatuhitaji jambo lolote zaidi ya zawadi yetu ya ubingwa.

“Wewe umeshawahi kuona wapi duniani kote hela ya madeni ikakatwa kwenye hela ya zawadi za ubingwa? Ikiwa tumeshinda ubingwa basi ni haki yetu kupewa zawadi ya ubingwa hilo lipo wazi na ambacho tunahitaji ni fedha zetu za ubingwa.
“Unajua thamani ya fedha za ubingwa? Na taarifa mliziona wapi? Kuna taarifa rasmi kuhusu zawadi ya ubingwa kwa suala la ubingwa? Ni kipi ambacho kinafanyika kuna gharama za uendeshaji ambazo zipo hivyo kila hatua tutaibainisha. Ikiwa umepata ushindi kinachotakiwa ni zawadi ya ushindi. Ikiwa kutakuwa na jambo lingine basi watawasiliana nasi kwa maandishi ili kujua kipi ambacho kinafuata.”

